Hapo kuna masuala mawili mazito: kwanza afande Chacha alipenda mpaka mwisho wa moyo wake, akajitolea kumpa Ummy chochote kile atakacho ili mradi amridhishe ikiwemo kulea wazazi wake lakini akaambulia maumivu. Aliona bora afe kuliko kuishi kwa mateso ya mapenzi (ni makali, asikwambie mtu) na bora amtoe roho Ummy na wazazi wake kama adhabu ya usaliti aliofanyiwa. Jambo la pili, wazazi wa Ummy waliongozwa na tamaa wakakubali maamuzi ya binti yao bila kufikiria jinsi gani afande Chacha alijitolea kwao, hatimae wakapoteza uhai. Funzo, mabinti bora umchane mwanaume mapema kwamba humpendi kuliko kumkubali akutimizie shida yako then unamtosa kama kapi la muwa lililoisha utamu.