Mauaji ya Akwilina: DPP afunga jalada la kesi baada ya Jeshi la Polisi kushindwa kubaini mhusika wa mauaji

Nitayainua machoyangu niitazame milima msaada wangu utatokawapi?, msaadawangu ukatika bwana aliezifanya mbingu na nchi.

Ebwana, bwana wewe ndiwe mwenye haki na hukumuzako niza adili.
 
Wasalaam, naandika kidogo tu nikiwa na huzuni moyoni. Sina maana ya kukumbusha machungu yaliotupata baada ya mpendwa wetu ndugu akwilina kuuliwa na risasi za police, naandika kwa kudai haki juu ya marehemu Dada akwilina ufanyike uchunguzi huru kuwabaini hawa wasiojulikana maana police wamesema hawajawajua waliotekeleza ukatili huu.

DPP amefunga jalada la uchunguzi kifo cha akwilina kwa sababu kaeleza wameshindwa kumtambua muuaji hivyo watuhumiwa wa mauaji hayo ambao ni police6 wanatakiwa kuachiwa huru bila masharti. Kwa maelekezo ya DPP ina maana wale police waliotuhumiwa kuua sio walioua, tuitishe uchunguzi huru ikibidi tushirikishe wachunguzi kutoka nje ya nchi maana isijekua wauaji wa Dada akwilina ni chadema, cuf, nccr mageuzi au ccm. Tujichukuzi wote tushirikishe na wengine ili tusituhumiane au kulituhumu jeshi la police.
 
Baada ya DPP kutoa kauli hiyo tukio liliposwa kufuatia ni kuona WAZIRI WA MAMBO YA NDANI,IGP NA RPC wa mkoa wa DSM wakijiuzulu kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo! Sababu kama wameshindwa kumbaini muuaji basi tayari wameonyesha udhaifu kwa huyo muuaji na atatumia mbinu zile zile kutekeleza mauaji mengine kwakuwa anaamini hamuwezi kumpata.

Lakini kwa sababu hii ni nchi ambayo tayari ilishakufa na kuoza na ilishalaaniwa na raia wake hawajielewi suala la kujiuzulu ni haliwezekani na inaonekana kawaida.

Napata hasira sana nikiona upumbavuuu unaendelea hapa nchini.
 

DPP Biswalo Mganga amesema amefunga jalada la kesi ya mauaji ya Mwanafunzi, Akwilina Akwilini baada ya kushindwa kubaini aliyehusika na mauaji.

--------------
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga amesema, jalada la kesi ya aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini amelifunga rasmi.

Hayo ameyasema leo Aprili 20, 2018; Ikulu jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari huku akionya watu wanaovunjua amani kutofumbiwa macho wakiwamo waandishi wa habari.

Amesema jeshi la polisi linapotumia nguvu kuzuia maandamano, haliwezi kushtakiwa au hata kukitokea vurugu na kusababisha mauaji huwezi kulishtaki jeshi.

”Katika maandamano yale ya watu zaidi ya 200, huwezi kubaini nani amehusika na kumpiga risasi Akwilina na mwili wake haukutolewa risasi yoyote.”

Alipoulizwa kuhusu askari waliokamatwa baada ya kutokea kwa tukio hilo, Biswalo amesema, “kama jalada nimelifunga, kwa hiyo askari wale nao wameachiwa huru hawana hatia.”

Mkurugenzi huyo amesema moja ya jukumu lake ni kuhakikisha amani inakuwapo,”na niseme tu kuwa, mimi sina chama cha siasa, si mwanasiasa, kwa hiyo sitamvumilia mtu awe mkubwa wala mdogo, nitamshughulikia.”

“Na wanaosema wataandamana, waambieni wasifanye hivyo kwani wakiandamana watakwenda kuwasilimulia familia yake,” amesisitiza Biswalo

Pia, amevionya vyombo vya habari ambavyo vinavyoweza kuchangia uvunjifu wa amani, hatua zitachukuliwa hivyo kuvitaka kuwa makini na kutimiza wajibu wao kwa kufuata misingi ya taaluma yao.


Chanzo: Mwananchi

Pia soma
- Maandamano ya CHADEMA: Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza NIT apigwa risasi na kufariki; Polisi wakiri kuhusika

- Polisi yakiri kupiga mtu risasi maandamano ya CHADEMA

- Kamanda Mambosasa: Tunamtafuta Mbowe, pia tunawashikilia Askari 6 waliotumia silaha za moto kudhibiti waandamanaji
HII SI HAKI NA SIAMINI KAMA HAYA YANAWEZA KUTOKEA TANZANIA
DPP &IGP WAJIUZULU
 
Kujua muuaji haikuwa kipaumbele kwao,kesi ya mauaji inaisha kiaina namna hii kweli!
 
Dodoma. Mbunge wa Konde (CUF), Khatib Said Haji amehoji kwa nini upelelezi wa kifo cha aliyekuwa Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini umekamilika kwa muda mfupi huku ule wa Masheikh wa Uamusho ukiwa bado.

Akichangia bajeti ya wizara ya mambo ya ndani ya mwaka 2018/19 bungeni leo Mei 3, 2018, Haji amesema ameshangazwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kusema amelifunga jalada la Akwilina aliyeuawa Februari 16, 2018.

“Akwilina faili lale limefungwa, kwa nini hatujui, hivi upelelezi huu wa haraka haraka umekwendaje, kwa nini upelelezi kama huu hautumiki kwa wengine, kama mmetumia muda mfupi kwa nini Masheikh wa Uamusho miaka mitano mpaka sasa upelelezi bado?” amehoji Haji

“Sisi ni wazazi, miaka mitano wameshikiliwa bila kufafanuliwa, hisia za ubinadamu na Utanzania urudi. Wake wawili wa wale Masheikh wamefariki,” ameongeza

Jalada kesi ya mauaji ya Akwilina lafungwa na DPP

Akizungumza huku Bunge zima likiwa kimya, Haji amesema; “Suala la kesi ya Uamsho linatukera sana, ukimya huu hata Bunge halifurahii, haiwezekani watu wamekaa miaka mitano lakini kimya.”

“Tukio la kufa Akwilina miezi miwili ila hili la Uamusho miaka mitano kwa nini? Leo tumefikwa na nini Watanzania,” amehoji Kuhusu matukio ya utekaji, Haji amesema; “Mauaji ya kiholela, utekaji umeshamili kwa kiasi kikubwa, ukisikia leo umelala na kuamka unashukuru Mungu, vijana kule Pemba walikamatwa na kutoa taarifa ya waliokwenda kuwakamata, lakini mpaka sasa hawajakamatwa.”
 
Hata kama limefungwa still hatia hawawezi ikwepa kina Mtulia,mkuregenzi na polisi maana bila hawa watatu mauaji yasingekuwepo
 
Back
Top Bottom