Mauaji Arusha yakoroga Bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauaji Arusha yakoroga Bunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Feb 11, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] Kauli ya Pinda yaamsha mapya
  [​IMG] Mbunge Lema awekwa mtegoni
  [​IMG] Spika Makinda awaka, asema�  [​IMG]
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (aliyesimama), akijibu maswali ya wabunge katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo, bungeni mjini Dodoma jana. (Picha:Tryphone Mweji)  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kishindo cha mauaji ya watu watatu yaliyofanywa na polisi mkoani Arusha Januari 5, mwaka huu, jana kilifunika Bunge kwa staili ya aina yake na mwishowe kumfikisha Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, kujikuta katika mtego wa kikanuni.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Lema akiomba mwongozo wa Spika, juu ya hatua anazoweza kuchukua mbunge iwapo atagundua kwamba kiongozi mkubwa wa serikali kama Waziri Mkuu amelidanganya Bunge, alimfanya Spika Anne Makinda kuwa mkali akikemea kwamba kauli ya mbunge huyo ililenga kumdhalilisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.[/FONT]
  "[FONT=ArialMT, sans-serif]Bunge letu hili lazima liwe na adabu inayostahili maana kama tunafanya sasa unataka kusema Waziri Mkuu kwa ahadi aliyoiweka bungeni anadanganya," alisema Makinda kwa kuhamaki.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika Spika alilizungumzia kwa mara nyingine jambo hilo.[/FONT]
  "[FONT=ArialMT, sans-serif]Sasa Bunge hili linataka kukosa hata adabu napenda nitumie kifungu kinachohusika kwa maelezo naomba wote mnisikilize," alisema.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisimamia kifungu cha 63(1) cha kanuni ambacho kinasema bila kuathiri masharti ya ibara ya 100 ya Katiba yanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano katika Bunge ni marufuku kabisa kusema uongo bungeni na kwa sababu hiyo mbunge yeyote anapokuwa akisema bungeni anawajibika kuhakikisha kuwa anatoa kauli, maelezo na suala ambalo anaamini kuwa ni la kweli na sio jambo la kubuni au la kubahatisha tu.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alinukuu pia kifungu cha 63 (2), mbunge yeyote anapokuwa akisema bungeni hatachukuliwa kuwa anasema uongo iwapo anafanya rejea ya habari kuhusu jambo fulani lilotangazwa au lililoandikwa na vyombo vya habari.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Aliendelea kunukuu kifungu cha 63 (3) ambacho kinasema mbunge mwingine yeyote yule anaweza kusimama mahali pake na kutamka kuhusu utaratibu kama alivyofanya Lema.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema baada ya kuruhusiwa na Spika kuongea na kudai kuwa mbunge aliyekuwa anasema kabla yake alikuwa anatoa maelezo ya uongo kuhusu suala au jambo alilokuwa analisemea bungeni.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Baada ya kusema hayo, Makinda alimpa Lema hadi Februari 14, mwaka huu (siku tano) awe amewasilisha ushahidi wa maandishi utakaoonyesha kuwa Waziri Mkuu Mizengo, alisema uongo bungeni.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Sakata hilo lilianza baada ya kipindi cha maswali na majibu kuisha ambapo Lema alisimama na kuomba mwongozo wa spika hasa akilenga majibu ya Pinda juu ya mauaji ya Arusha.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alimtaka Lema kuandika vizuri maelezo kama Pinda amedanganya halafu watamweleza atafanya nini, kwa mujibu wa kanuni hiyo, kama mbunge atashindwa kuthibitisha kauli yake, ana mawili, moja kuomba radhi na kufuta usemi wake, au ang'ang'ane nao na kupewa adhabu ya kutohudhuria vikao vitano vya Bunge.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kabla ya kufikiwa kwa maamuzi ya Spika Makinda, wakati wa kipindi cha maswali na majibu, alisimama Mbunge wa Kibakwe (CCM), George Simbachawene na kuomba mwogozo wa spika.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Aliomba mwongozo kwa Spika mtu kama Lema ambaye ametoa kauli anayemkashifu kiongozi wa juu na kanuni zinasemaje na adhabu gani atachukuliwa.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, Spika alimtaka mbunge huyo kukaa chini kwa kuwa alipoomba mwongozo si mahali husika.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mtafaruku huo uliibuka baada ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mbunge wa Hai (Chadema), Freeman Mbowe, kumbana Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati wa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu juu ya mauaji yaliyofanywa na polisi jijini Arusha dhidi ya raia.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mbowe alimtaka Pinda aeleze kama serikali ina nia ya kuunda tume kuchunguza mauaji hayo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mbowe aliuliza kwa kuwa serikali ilipewa taarifa na polisi bila kupata taarifa za upande wa pili, ni lini itaunda tume ya uchunguzi wa kimahakama (Judicial Commission of Inquiry) ili kupata waliohusika.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katika majibu yake, Pinda alisema Serikali haiko tayari kuunda tume ya kimahakama ya uchunguzi kwa ajili ya kuchunguza na kuwabaini waliohusika na vifo hivyo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Pinda alisema kama Mbowe ana dhamira asingesubiri kumuuliza swali hilo bungeni badala ya kuwasilisha taarifa serikalini kwanza ili izifanyie kazi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Pinda ambaye alionekana kukerwa na swali hilo, alisema kuwa serikali lazima iridhike kuwa zipo sababu za kutosha ili ianzishe uchunguzi huo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katika swali la msingi, Mbowe alimuuliza Pinda kuwa pamejitokeza matukio mengi ya askari kuwapiga risasi raia na kupoteza maisha na kwamba kwa kuwa serikali haijawahi kutoa taarifa, je, inaweza kutoa tamko kwa vifo vya Arusha ikiwemo kujiuzulu kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi?[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Pinda alisema: "Serikali hii ni makini sana, ukiona jambo limetokea kama la Arusha, usikimbilie kusema serikali, bali nani amesababisha hayo."[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema Chadema kilikutana na kujadiliana na kushauriana na polisi kuwa maandamamo yao yatumie ruti moja ya barabara kutokana na ufinyu wa barabara za jiji la Arusha, lakini chama hicho kilikaidi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema kuwa baada ya Chadema kukataa ushauri huo, serikali iliamua kuzuia maandamano hayo na badala yake ilielekeza kuwa ufanyike mkutano peke yake, lakini Chadema waliendelea na maandamano.[/FONT]
  "[FONT=ArialMT, sans-serif]Baadhi yenu mlikamatwa na pale kwenye mkutano matamshi yenu hayakuendana na chama cha siasa," alisema Pinda.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema kilichosababisha watu hao kupigwa risasi ni kutokana na hatua ya wafuasi wa chama hicho kwenda kuwakomboa wenzao katika kituo cha polisi na kukisogelea umbali wa mita 50 na kwamba polisi hawakuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya kutumia nguvu na watu kupigwa risasi.[/FONT]
  "[FONT=ArialMT, sans-serif]Mngefuata ushauri haya yote yasingetokea," alisema bila kuzungumzia suala la IGP na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kutakiwa kujiuzulu.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Bunge, Lema alisema atawasilisha ushahidi huo kama alivyotakiwa na Spika.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema yeye ni mtu mzima na haogopi chochote.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Januari 5, mwaka huu Chadema waliandaa maandamano makubwa katika Jiji la Arusha pamoja na mkutano wa hadhara kwa nia ya kulaani mchakato wa kumpata meya wa Jiji hilo ambaye inadaiwa alipatikana kwa njia ambazo hazikubaliki kwa kuwa wapo madiwani waliopiga kura kinyume cha kanuni.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katika maandamano hayo ambayo awali yalikuwa yamekubaliwa na Polisi, yalibatilishwa na IGP Mwema jioni kabla ya siku ya maandamano, lakini Chadema waliendelea nayo, hali iliyosababisha mapambano baina ya wafuasi wa chama hicho na polisi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Polisi walitumia nguvu kupita kiasi kwa mabomu ya kutoa machozi, maji ya kuwasha, risasi za moto na kuua watu watatu.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Siku hiyo pia, viongozi wakuu wa Chadema, akiwamo Mbowe, Katibu Mkuu wa Chadema ambaye pia alikuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu uliopita, Dk. Willibrod Slaa; Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini; Lema; na viongozi wengine kadhaa walikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kuandamana bila kibali.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kesi hiyo bado inaendelea kutajwa katika Mahakama ya Mkoa Arusha.
  Source: IPPMedia
  [/FONT]
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Busara ya kujibu swali ni muhimu zaidi kuliko kutumia tu mbinu za kujitetea. Mheshimiwa Pinda hakutumia busara zaidi katika kujibu swali na papo hapo Spika Makinda ndio karuka jivu na kukanyaga moto. Moto utakaolipuka sasa baada ya kumruhusu Lema kuwasilisha vielele vya maafa ya Arusha Makinda kafanya bila kukusudia na huenda atakuja kujutia mambo yatakapofumuka upya.
   
 3. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Bila ushabiki nitasema kwa haki, huyu mtu kama mnategemea anything than rubish mtakuwa mmekufa, jamaa hana akili, busara, wala adabu, yeye peke yake amefanikiwa kuitukanisha CDM kwa wananchi na mataifa mengine mara nyingi zaidi kuliko mtu yeyote ndani ya CDM, tena amevunja rekodi kwa kuyafanya haya kwa muda mfupi kuliko mwanasiasa yeyote(hata mrema)
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ni busara Waziri mkuu kusema hayo?
  Spika wa Bunge kuombwa mwongozo kwake maana yake ni matusi?
   
 5. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,716
  Likes Received: 3,126
  Trophy Points: 280
  Ametukanisha Chadema how?? Ulitaka asemeje?? Akubaliane na maneno ya Waziri Mkuu? Heri yeye ambaye hana akili, busara,adabu ya kuitetea CCM lakini ana baraka za kila Mtanzania anayeililia na kuipenda Tz. na heri kwako wewe unayetetea MAFISADI. Nadhani huu ni uwiano sawia kabisa ni sawa na 1+1=11 na si vinginevyo.
   
 6. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Huna jipya ndio upeo wako.
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Feb 11, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280
  ..je, waliouawa walipigwa risasi umbali wa mita 50 toka kituo cha Polisi?

  ..raia wa Kenya pia alikuwa amekwenda kuvamia kituo cha polisi kuwatoa viongozi wa CDM waliokuwa mahabusu?

  ..majibu ya maswali hayo ndiyo yatakayobainisha muongo ni nani kati ya Pinda na Lema.
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  nasema muhimu kutumia busara katika kujibu badala ya kujibu kisiasa. Vielelezo vikiletwa kwamba waliouawa walikuwa nje na mbali ya kituo cha polisi Arusha Waziri Mkuu ataelewekaje?
   
 9. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Halafu unadhalilisha wajapan kwa kujipachika nick 'mjepu'
  hawana akili fupi kama wewe..otherwise wangekuwa mamefutika katika ramani ya dunia siku nyingi.
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Yaani hawa hawaogop ya Misri
   
 11. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mjepu,

  Tunajua huko kazini lakini wakati mwingine uwe unaona aibu kidogo!!!!!

  Tiba
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Lema atakapoleta uthibitisho wa Mkenya aliyeuawa mbali kabisa na kituo cha polisi atasemaje? Kitakapoletwa kithibitisho cha polisi kuingia mpaka makanisani kuwasaka watu kama walipoingia mpaka nyumba ya masisi karibu na Kanisa la Mt. Theresia atasima kuna kituo cha Polisi pale?
   
 13. Josephine

  Josephine Verified User

  #13
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Pamoja na mapangufu yote,unayoyaona bado ukweli utakuwa wazi Mjepu.
   
Loading...