Matumla ambaye alionekana dhahiri kuelemewa na mfilipino huyo katika raundi ya pili, ilimbidi aliage pambano hilo katika raundi hiyo baada ya kupewa makonde mawili mazito yaliyomdondosha chari kwa nyuma.
Matumla alijaribu kuamka bila mafanikio na refa wa pambano hilo alilimaliza pambano hilo katika raundi ya pili dakika ya 2:59.