Matumizi ya Video Queens: Wasanii wa Bongo wanaboa

Hahahaahah nimekumbuka jamaa yangu mmoja alikuwa anampa makavu demu mmoja kajichubua balaa,alafu ni wakuringi sana mshikaji alimpa shit moja nikikumbuka uwa nacheka sana eti " uringia weupe wakati mwenzio nyani kauwekea matakoni" hahahhahaha .
 
Cku hizi rangi nyeusi imekua hadimu asilimia kubwa ya dd ztu wamejchubua unfkr ukiambiwa uchague ogii n feki utachukua ipi
 
kuna baadhi wanakimbia soo
uki shoot na mademu wa bongo
wanasingizia umetoka nao
mfano diamond na yule dada irene wa kwetu ya rayvanny
 
white supremacy imetula sana aisee,hata kichupa cha blue ft kiba,nashangaa kumuona yule mzungu ambaye ni wa kawaida sana,hana mvuto wa kuwashinda hata dada zetu wa hapahapa bongo.at least yule wa rich mavoko kwenye kichupa cha "pacha wangu" ana mvuto.
yule wa Blue eti ndo mboga saba mwenyewe asee
 
kuna baadhi wanakimbia soo
uki shoot na mademu wa bongo
wanasingizia umetoka nao
mfano diamond na yule dada irene wa kwetu ya rayvanny
Sawa basi hata wanapokwenda Sauz kushoot si kuna madem weusi tena wazuri kweli kweli kwanini wasiwachague wale na wanachagua wazungu.?
 
Nimetoka kuangalia Video mpya ya Mr bluu "mboga saba" na nasikitika kusema kwamba sijaipenda sio kwamba nyimbo ni mbaya bali ni kwa haka katabia ka wasanii wa Bongo kuwaweka kwenye video Madem weupe(waarabu,wahindi,wazungu na wale wenye muonekano wa light skins). Hii inaonesha ni jinsi gani sisi watu weusi hatujikubali wenyewe na ndo mana sishangai kuona idadi ya wanawake wetu weusi wakijichubua ngozi zao.

Kila Msanii anataka ashoot na dem mweupe. Rejea video za Diamond, Alikiba,Ommy Dimpoz,Blue,Hamonaiza na wengine kibao. Hata hao wazungu wenyewd wanatushangaa kuona jinsi tunavyowanyenyekea. Mfano yule dem alioshuti "Bado" ya Hamonaiza ilitokea ajali kidogo basi dem akagoma, Wacha majamaa wampigie magoti kisa dem mweupe mpaka akakubali na dau wakapandishiwa.

ACHENI USHAMBA WASANII WA BONGO FLEVA


Wasanii wa kibongo asilimia kubwa yao ni washamba, waonee huruma tu.
 
Hata wanamuzik Black Americans video Queens wao wengi ni chotara wanaong'aa naona ni kasumba globally
 
Asalam aleikum.

Hivi majuzi niliandika makala kuhusu wasanii wa bongo kupenda kutumia mabinti weupe ama wazungu kwenye video zao: Wasanii wa Bongo wanaboa

Nahisi watu wa karibu wa Diamond walimfikishia ujumbe wangu na kuamua kujirekebisha.

Diamond amesema kama wewe ni binti mwenye muonekano wa kiafrika mtumie DM upate nafas ya kushiriki katika video hiyo.

DIAMOND CQ.JPG


Sasa naamini kuwa JamiiForums ni zaidi ya mtandao wa kijamii kwa maana wasanii na watu mbalimbali wanapita hapa na kusoma mawazo yetu.

Haya Nipigieni Makofi tafadhali..
 
Back
Top Bottom