Matumizi ya neno ''Mheshimiwa'' kwa viongozi wenye nyadhifa

Hata mimi nilimshangaa Nkamia kuwaita wenzake MBWA! Halafu alipoombwa kufuta kauli akasema uelewa mdogo wa Mbunge Machali, eti Kiswahili kinampa shida Machali ndo maana hajamwelewa Nkamia alimaanisha nini? Hivi Nkamia na Machali nani kaenda Shule jamani?

Naomba nikiri kwamba Nkamia nimemfuta kwenye orodha ya watu, huyo ni kiatu!!!
 
Samahani kama nilisikia peke yangu, nilimsikia Juma Nkamia akiwaita ni MBWA. Sasa nashangaa nyie hamjatilia maanani title hiyo, Mfano halisi "MBWA JUMA NKAMIA" Na mbaya zaidi alisisitiza kuwa ni MBWA alipokataa kufuta kauli hiyo, Asante Mbwa Nkamia

nimeipenda hii
 
Hata mimi nashindwa kumwita Mheshimiwa wakati mambo anayofanya ni bora hata ya SHETANI.
Kuhusu hawa jamaa kujiita MBWA ni kwa kauli zao Juma Nkamia aliwaita hivyo wabunge wenzie siyo mimi au hukuangalia bunge last week??? These people mbele za Mungu ni watu muhimu sana kwenye jamii ni
watunga sheria kwanza hawakutakiwa hata siku moja kunyosheana vidole, walitakiwa kuwa kama malaika, lakini leo nakubali yaishe kwani walishataka bunge lisionyeshwe LIVE wakiwa na nia ya kutukanana vizuri, wananchi tukalalamika kuwa lazima bunge lionyeshwe LIVE leo hii nakubali kuzima TV sitaki kuona bunge hili maana matusi yao hakua tofauti na WALEVI WA KOMONI KWENYE VILABU VYA POMBE.

Wanaubavu wa kutunga sheria? Kazi yao ni kupitisha bill of law ili iwe sheria .Hamna kitu hao.
 
Ndugu wanajamii forum viongozi wetu huitwa waheshimiwa lkn kwa MWL NYERERE naona hata watu wakimtaja ni nadra kusikia wakisema mheshimiwa ,naomba kuuliza mwenye uelewa je alikataa kuitwa au jina limekuja hivi karibuni?
 
Ndugu wana JF,

Ninapoangalia na kutafakari mienendo ya baadhi ya viongozi wa Serikali na Wanasiasa wetu, napata shida kuendelea kuwaita baadhi yao "WAHESHIMIWA". Kwa ufahamu wangu, "Mheshimiwa" ni mtu ambaye yeye mwenyewe "anajiheshimu". Hebu tutafakari haya mambo machache kwanza:

1. Wanasiasa na viongozi wa serikali ambao wanatuhumiwa kwa vitendo vya rushwa je wanastahili kuendelea kuitwa "waheshimiwa"??

2. Viongozi wanaotumia lugha chafu, za kuudhi na matusi hadharani na hata Bungeni bado tuwaite "Waheshimiwa"?

3. Viongozi wasiokuwa na uelewa wa mambo mbalimbali ya kijamii na kitaifa bado tuwaite "waheshimiwa"?

4. Viongozi wanaodhalilisha wanawake na watoto; wenye tuhuma za ubakaji bado ni "waheshimiwa"?

Kwa mtazamo wangu, hii title "MHESHIMIWA" inawafanya hawa viongozi wasiokuwa na sifa njema kuendelea kujifariji katika matendo yao maovu wakijua kwamba heshima yao bado ipo palepale. Ni vyema basi tukaliangalia kwa upya swala hili la kuwaita viongozi "WAHESHIMIWA" hasa pale ambapo wenyewe hawajiheshimu.
 
Ni kweli mkuu make unakuta kiongozi anawanawake rundo lakini kila mmoja kazaa naye kiharamu hata hajafunga nao ndoa na wengine walitenda dhambi ya uzinifu mpaka kanisani.
 
Kwa yaliyowahi kujiri ndani ya bunge na yanayoendelea kujiri ndani ya bunge,unadhani ni sahihi kwa wabunge kuitwa waheshimiwa?

Mimi binafsi nasema hapana na ninashauri litumike neno "ndugu" badala ya hili la "mheshimiwa".

Hivi katiba haiwezi kutumika kukomesha matumizi ya neno "mheshikiwa"?.
 
Kwa hiyo unataka wasiitwe tena waheshimiwa ili kuhalalisha yanayojiri huko Bungeni?
 
Ndg,wana njavini ni mda sasa nimekuwa nikitafakari na kutafakuri juu ya jina ili adimu MHESHIMIWA(Mh.)Maranyingi nimesikia kwenye vyombo vya habari,bungeni,ata sehemu yeyote ile Mbunge yeyote anapotajwa shart lianzwe neno Mheshimiwa( Mh),Je neno ili lipo kikatiba nakama ni kikatiba ni kifungu gani ili na mimi nikakisome au wabunge waliamua kujiita na sisi tukaliendeleza.
Nawasilisha kwenu wakuu.

Tanzania itajengwa na wazawa na kuliwa na wageni.
 
Ndg wana njanvini ni mda sasa nimekuwa nikitafakari na kutafakuri juu ya jina ili adimu MHESHIMIWA(Mh.)Maranyingi nimesikia kwenye vyombo vya habari,bungeni,ata sehemu yeyote ile Mbunge yeyote anapotajwa shart lianzwe neno Mheshimiwa( Mh),Je neno ili lipo kikatiba nakama ni kikatiba ni kifungu gani ili na mimi nikakisome au wabunge waliamua kujiita na sisi tukaliendeleza. Nawasilisha kwenu wakuu.
Tanzania itajengwa na wazawa na kuliwa na wageni
 
nadhani lipo kikanuni.... ila bwana na bibi yangetosha maana wengine hata heshima hawana kama vile....
ntarudi kumalizia
 
Kuna sababu gani ya mbunge kuitwa mheshimiwa, wakati hawaonyeshi heshima bungeni.neno mheshimiwa lina maana kubwa sana.
 
Kuna sababu gani ya mbunge kuitwa mheshimiwa, wakati hawaonyeshi heshima bungeni.neno mheshimiwa lina maana kubwa sana.



Hilo neno wamelifanya kichaka cha kuficha upuuzi wao,
 

Attachments

  • index.jpeg
    index.jpeg
    8.7 KB · Views: 128
Wehu tu kazi hawafanyi kutaka sifa za kijinga tu ndio maana mwlm alikuwa anapenda sana kutamka neno -------- yaani hawajielewi wapo wapo tu.
 
Baada ya uhuru Rais alikuwa anaitwa Mtukufu na wengine wote waheshimiwa. Baada ya ujamaa neno ndugu liliingia na neno mheshimiwa kupotea kabisa lakini Rais alikuwa bado anaendelea kuitwa Mtukufu na wakati mwingine Ndugu Rais. Rais Mkapa ndiye aliyekataa kuitwa mtukufu na badala yake akapendwa kuitwa Mheshimiwa. Ndipo hilo neno mheshimiwa likarudi upya.
 
Back
Top Bottom