Matumizi ya neno ''Mheshimiwa'' kwa viongozi wenye nyadhifa

1. Catherine Magige.
2. Vicky Kamata.
3. Juma Nkamia.
3. Livingstone Lusinde.
4. John Komba.
5. Mwigu Lameck Nchemba.
WANAJF. HAWA SIWAONI KAMA NI WAHESHIMIWA.


mwigulu nchemba ndio kabisaaa hana sifa hata moja ya uheshimiwa
 
Mzee ruksa huyo. Alihalalisha wengine waitwe waheshimiwa na yeye Akajiita Mtukufu. nakumbuka kipindi kile, mtukufu rais Daniel Arap Moi, Mtukufu Rais Mwinyi were very famous phrases. BWM ndo alikuja kukataa jina la utukufu. Sasa hawa ambao mpaka tunawatuhumu ni wala rushwa hili jini haliwafai. Na je? wakitoka kwenye ubunge hiyo hadhi ya uheshimiwa to the eyes of the public inakuwaje? mbona wanakuwa wakawaida na wengine mufilisi kabisa? nenda Dodoma uangalie matendo yao nje ya bunge. Huu ubwanyenye ndo unawafanya wajione wako juu na matokeo ndo kupitisha kitawachowahusu hawa na hiki kitatuhusu sisi. mafao ya kujitoa saga
 
Moderators, si mngechanganya hii post na ile ya Synthesizer ili kusiwe na haja maoni sehemu mbili juu ya topic moja?
 
.... Sijui kuachwa kwa matumizi ya hili neno "ndugu' kama kunahusiana na kufa kwa sera ya ujamaa au vipi?

Nashauri tuachane na neno hili na turudi kuitana ndugu kama zamani. Ndugu Mkapa, Ndugu Dk Slaa, Ndugu Rais Kikwete, Ndugu Zitto. Nauliza ni wapi huu utamaduni ulifia?...
.

Tofauti ya kipato na line za vipato ni sababu mojawapo. Of coz, wakati wa ujamaa matajiri walikuwepo lakini hawakuwa na nafasi ktk siasa na uongozi kwa ujumla.

Lakini tujiulize kuitana tu ndugu wakati tunaumizana kiuchumi kutakuwa na maana kweli?
Tuanze upya kwa kuweka maadili na misingi mipya ya uongozi; kuanzia ngazi ya familia, mitaa, mashuleni na vyuoni. Kwa sasa wanasiasa wengi hawana uzalendo na nchi hii tena, ni wazealendo kwenye maslahi yao na ya vyama vyao tu. Kwangu mimi mchakato unaonedelea wa katiba ni "ajua"; lazima tuwe na mchakato mwingine mpya na wa tofauti ili tutengeneze katiba mpya ya ukweli mara baada ya uchaguzi wa 2015, na huko tutaweka misingi mizuri ya kujenga na kulinda uadilifu kwa viongozi ngazi zote
 
Tofauti ya kipato na line za vipato ni sababu mojawapo. Of coz, wakati wa ujamaa matajiri walikuwepo lakini hawakuwa na nafasi ktk siasa na uongozi kwa ujumla.
Lakini tujiulize kuitana tu ndugu wakati tunaumizana kiuchumi kutakuwa na maana kweli?
Tuanze upya kwa kuweka maadili na misingi mipya ya uongozi; kuanzia ngazi ya familia, mitaa, mashuleni na vyuoni. Kwa sasa wanasiasa wengi hawana uzalendo na nchi hii tena, ni wazealendo kwenye maslahi yao na ya vyama vyao tu. Kwangu mimi mchakato unaonedelea wa katiba ni "ajua"; lazima tuwe na mchakato mwingine mpya na wa tofauti ili tutengeneze katiba mpya ya ukweli mara baada ya uchaguzi wa 2015, na huko tutaweka misingi mizuri ya kujenga na kulinda uadilifu kwa viongozi ngazi zote

Mindset ni kitu muhimu sana, tuanzie hapo kwanza ili wote tuwe ground zero halafu mambo mengine ndo yataenda. Kitendo cha mtu kuitwa Mh. automaticaly kinamfanya ajione ni excption, na matatizo yooote yanapoanzia.
 
Ukiniita 'ndugu' alaf media zikarusha na madem zangu,vimada na maswaiba wakaskia nakushusha cheo na ikibidi nakufukuza kaz!
 
Watanzania wa leo ni tofauti na wazamani, wa leo wameonja madaraka, walikua hawapati nafasi sasa hivi kila mtu ananafasi. kuna watu kama wa Bunge, wanasheria na madaktari wanapenda sifa sana. Usipomwita Dr fulani, anaona kama ni tusi kubwa. Mbona wenzetu waliyo tuletea elimu ni watu wakawaidatu. Hawataki kuitwa Dr x, or Honorable y. ila sisi kwa kua tulikua nyuma sana kielimu tunashobokea sana kuitwa waeshimiwa na vyeo vingi vingi eti kuonyesha heshima. cha kushangaza zaidi hakuna tunacho kifanya. Kuna jamaa yangu anafanya kazi mahakama ya wilaya muheza, nilimtembelea ofisini siku mmoja kwa kwakua ni jamaa yangu nilimuita kwa jina lake bila neno Mhe. jamaa alinijia juu, anataka nimuite Mheshimiwa, Wa Bongo bana! Mbongo ata ukimlipa 50,000 kwa mwezi na ukampa cheo cha Mheshimiwa kwake yeye pouwa tu. watu wanapenda kueshimiwa na huku hawafanyi kitu.

Subiri kazi yako ikuinue na siyo wewe mwenyewe kujiinua. Bunge la kenya linaendeshwa kwa kawaida, wanaitana Mr speaker, Mr x,y and Z lakini sisi. Mhe kila kukicha. matokeo yake inakua vigumu kuwaapproch awa wabunge. This is not Good kwa kweli.
 
ETI.jpg
 
1. Catherine Magige. 2. Vicky Kamata. 3. Juma Nkamia. 3. Livingstone Lusinde. 4. John Komba. 5. Mwigu Lameck Nchemba. WANAJF. HAWA SIWAONI KAMA NI WAHESHIMIWA.
Kweli mkuu, wapo na wengine zaidi, hawa wote hutua pumba tupu na kuwapaka ***** wapiga kura wao!. Kwao ubunge ni fadhila na tena wanaulinda kwa kujipendekeza mno!. Tusiishie kusema hawafai, tuende mbele zaidi kwa kutafuta majembe ya kuwang'oa 2015.
 
1. Catherine Magige. 2. Vicky Kamata. 3. Juma Nkamia. 3. Livingstone Lusinde. 4. John Komba. 5. Mwigu Lameck Nchemba. WANAJF. HAWA SIWAONI KAMA NI WAHESHIMIWA.
Kweli mkuu, wapo na wengine zaidi, hawa wote hutoa pumba tupu na kuwapaka ***** wapiga kura wao!. Kwao ubunge ni fadhila na tena wanaulinda kwa kujipendekeza mno!. Tusiishie kusema hawafai, tuende mbele zaidi kwa kutafuta majembe ya kuwang'oa 2015.
 
Mkuu Synthesizer nakuunga mkono. Nakumbuka wakati wanabadili sheria ati waitwe waheshimiwa, marehemu JK Nyerere alipiga kelele kukemea lakini wapi. Wakasema ati mbona wabunge wa Uingereza wanaitwa Honourable kwa nini wao wasiite waheshimiwa!Basi wakapitisha hiyo sheria yao na kuanza kuitana Mheshimiwa badala ya neno murua lisilokuwa na chembe ya majivuno wala kujikweza ambalo ni NDUGU. Ukienda Kenya bado watu wanatuita NDUGU.Nalipenda neno NDUGU. Hivi ukimuita mtu Mheshimiwa una maana wewe ni MDHARAULIWA kwa maana kama si mheshiwa basi ni kintume chake.
MIMI SIPENDI KUWAITA WATU WAHESHIMIWA NA KUANZIA LEO SIMUITI MTU AWAYE YOTE MHESHIMIWA, POTELEA MBALI.
 
Last edited by a moderator:
Wakati wa utawala wa Mwinyi tulishuhudia kujikweza kwa viongozi wetu na kutaka waitwe "Waheshimiwa", wakibadili neno lililotumiwa kwa miaka mingi kwa viongozi na watanzania kwa ujumla wote kuitana "ndugu".

Ukweli ni kwamba wengi hatujagundua kwamba toka viongozi waanze kuitwa "waheshimiwa" walianza kujiona kama tabaka la aina iliyo juu mbali na mwananchi wa kawaida, wengi wao wakawa mafisadi na kusahau shida za wanachi wa kawaida waliowawakilisha.

Kumbuka neno "ndugu" lilitumika kwa kila mtanzania, hata katika katiba nadhani, tuna misemo kama "binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja".

Tangu lianze kutumika, neno "mheshimiwa", lililopata baraka zote na viongozi wa CCM, lilimekuwa kama neno lilololeta laana kwa CCM na uongozi Tanzania.

Kwa msingi huu basi, napendekeza turudi tena kwenye matumizi ya neno "ndugu" badala ya "mheshimiwa". Na ukweli ni kwamba heshima inayohusiana na "uheshimiwa" ni jambo ambalo mtu analipata kwa matendo yake (you earn respect rather respect by default).

Na pia, japo tunawaita viongozi na wabunge "mheshimiwa" kuna wengi sana hawastahili kabisa kuitwa hivyo. Binafsi niko radhi sana kumwita kiongozi fisadi "ndugu" kuliko "mheshimiwa".

hapo umenena, wengi ni 'waishiwa wabunge na mawazir, hamna kitu hapo'
 
Kama mtakumbuka enzi zile mtu yoyote hata awe na cheo gani alikuwa anatajwa kwa kuanza na Ndugu. Mwenye cheo kikubwa alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Baba wa Taifa alikuwa anaitwa Ndugu Julius Kambarage Nyerere.

Nachotaka kuwakumbusha hapa ni tangu wenye madaraka waanze kutaka kuitwa Mheshimiwa fulani hali imekuwa ndivyo sivyo, wanasahau kuwa cheo ni dhamana, wakubwa hawa sheria iko chini yao na ndio maana polisi na mahakama haiwahusu na kama inawahusu kesi zao zinaisha kwa siku chache ili wasisulubiwe au wakisulubiwa dhamana ni kitu cha bure kwao.

Ndugu lilikuwa jina la kutuweka karibu ya kwamba tupo sawa isipokuwa kimamlaka na kiutendaji na wanandugu waliona fahari kuwajibika kwa wengine, tangu tuanze kuitana Waheshimiwa hisia 'Mimi Mheshimiwa' zimewafanya wengi wajione wao ni wao, uzalendo haupo tena.

Ajidhaniaye amesimama aangalie asianguke kwani akianguka anguko lake ni kuu ni sauti yake ni kishindo, Waheshimiwa tendeni haki, fanyeni uzalendo fumbueni macho mtazame na kusoma alama za nyakati ili uheshimiwa usije ukawatokea puani.
 
Cheo ni dhamana.. cintotumia cheo changu kwa faida yangu.. ndugu zangu wala jamaa zangu..

Wangeishika hii tu wala wacingetaka kuitwa waheshimiwa..
 
Yaaani ni kweli kabisa hawa viongozi wamejisahau kwa ajili ya uheshimiwa!!mabosi wao tunawaangalia tuu tunasubiri wakija uchaguzi maana wengi wako kwenye majimbo ya dar as if ndiko walikochaguliwa.....kwetu wanakujavkuomba kura!! Shenzi. Type...
 
Inadaiwa "waheshimiwa" wengine wameanza kutukana mpaka matusi ya nguoni.

Mh. Serukamba mbunge wa ccm wamewdiriki kuseme neno '---- YOU' akiwa anawakatisha wabunge waliokuwa wakiingilia maongezi yake alipokua akichangia hoja juu ya swala la kesi ya rwakatale kujadiliwa bungeni.
Tusi hili la kiingereza limesikika vema na pia nina uhakika mda sio mrefu tutapata video yake dunia ijionee jinsi viongozi wetu wa taifa wanavyotukana kwenye chombo muhimu kama bunge tena hii ameongea lugha ya kimataifa itaeleweka zaidi.
 
Si haki wala si halali kwa hawa wabunge wetu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kuitwa waheshimiwa! Hakuna sababu yoyote ya msingi ya hawa watu kuitwa waheshimiwa, hata ndugu hawafai kuitwa! waheshimiwa gani wanaporomosha matusi utadhani wahuni wa kijiweni!?huku mitaani kwetu kuna watu wengi sana wasio wabunge wala viongozi ambao tunaona wana haki ya kuitwa waheshimiwa. Waheshimiwa gani hao wanaotoa maneno ambayo 'hayajavaa nguo' ndani ya bunge! mara ooh- sijui nani kaja hapa kajamba halafu kaibukia kibaha,maneno ya kitoto na kipuuzi kama hayo yanatoka kwa babu Zima lililovaa Kaunda suti na baraghashia kichwani! mwingine anatukana F.U.C.K Y.O.U bungeni akiwa katinga suti na tai yake shingoni! najaribu kutafakari hawa watu wakiwa wamevaa suti wanazungumza utumbo namna hiyo, je akiwa kavaa pajama au bukta na singlet si itakuwa balaa-hutaweza kuamini kama ni mdomo huo huo anaotumia kunyea mitusi ndio anaotumia kutafunia burger! kwa kweli wabunge hamfai kuitwa waheshimiwa na hiyo ipendekezwe kwenye katiba mpya! mnatuaibisha, mnatukera, mnatuudhi na kutukatisha tamaa, badala ya kulumbana kwa hoja za msingi nyie mnashindana kwa vijembe na mitusi! halafu mnadhani bunge litaleta ufanisi kwa mustakabali wa maendeleo wa taifa letu!? shame on you wabunge! you do not deserve to be called WAHESHIMIWA! you are too cheap for such a respect, too cheap! hebu jitafakarini na mjitathmini upya na mbadilike! hata kama wapo wabunge wengine ambao ni wastaarabu lakini wote mnabeba collective responsibility, wabunge wote walio wastaarabu wahakikishe wale wabunge wote ambao wamekosa ustaarabu wanachukuliwa hatua madhubuti zinazostahili na zitakazoleta tija ili bunge liheshimike.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom