Matumizi ya Mitandao Jamii Kwenye Chaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matumizi ya Mitandao Jamii Kwenye Chaguzi

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Jun 17, 2010.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jun 17, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wakati ambapo Uchaguzi mkuu unakaribia Wanateknohama wanashauku ya
  kujua mambo mbalimbali kwa njia ya mtandao kuanzia kupashana habari ,
  majadiliano motomoto na masuala mengine mengi sana yanayohusiana na
  Uchaguzi mijadala hiyo itakuwa kuanzia Kwenye majukwaa ya wazi ambapo
  watu hudumia majina halisi kama www.wanabidii.net mpaka kwenye blogu
  mbalimbali nchini tembelea www.afrigator.com chagua nchi ya Tanzania
  huo ni mtandao unaoweza kutumia kufuatilia blogu mbalimbali za afrika
  lakini zilizosajiliwa kwenye mtandao huo tu .
  Unaweza kujiuliza jinsi teknohama haswa mitandao jamii inavyoleta
  mabadiliko kwenye jamii nyingi duniani haswa wakati wa uchaguzi mkuu
  kuanzia kukusanya taarifa za wanachama kwa njia ya mtandao mpaka pale
  wanachama hao wanapo changa hela kwa ajili ya wagombea wao kwa njia ya
  mtandao na hata pale watu wanapotuma matokeo ya uchaguzi kwa njia ya
  mtandao hizi zote ni hatua kubwa katika maendeleo .

  Nchi mbalimbali duniani zimeweza kutumia teknohama kwenye shuguli zao
  mbalimbali zinazohusisha uchaguzi kwa mafanikio makubwa sana hata kama
  chaguzi hizo zilileta vurugu na manunguniko kwa wale walioshindwa ,
  kuanzia kuanzisha tovuti za vyama mbalimbali vya siasa au hata blogu
  za mwanachama mmoja mmoja na kurasa zingine nyingi sana za mitandao .

  Fikiria chama kinavyotaka kupanga kampeni Fulani kwa sasa si lazima
  wote kukutana sehemu moja ambapo wanatumia gharama na muda mwingi
  kuandaa mkutano wanaweza kutumia huduma za sms kuwasiliana kwa kutumia
  namba walizozihifadhi za mwanachama wao kuwasiliana na sasa idadi ya
  wamiliki wa simu imeongezeka na watu wengi wamesajili namba zao za
  simu ni rahisi zaidi .

  Hata pale ambapo kumetokea tishio la wizi wa kura na kero zingine
  zozote watu wanaweza kutumia simu zao wa mikononi kwa ajili ya
  kupashana habari taarifa na huduma zingine haswa kwa vijana mfano
  wanaosimamia vituo vya kupiga kura .

  Na pale ambapo watu wako vijijini kabisa ambapo ni ngumu kufika kwa
  sababu kadhaa jamii hizo zinaweza kutumia simu zao za mikono kwa ajili
  ya kupashana habari na taarifa zingine moto moto .

  Tanzania ni moja ya nchi ambayo imewahi kuonja utamu wa matumizi ya
  teknohama kwenye shuguli za uchaguzi zaidi kuanzia mwaka 2005 ambapo
  vyama vya siasa viliwasiliana na wanachama wao kutumia mtandao na hata
  baadhi ya wagombea kuanzisha blogu na huduma zingine kwenye mtandao .

  Mwaka huu tunaingia kwenye uchaguzi tena baada ya miaka zaidi ya 4
  ambapo kumetokea maendeleo makubwa kwenye sekta ya teknohama kwa
  ujumla kuanzia matumizi ya simu za mkono zenye uwezo mkubwa mpaka
  kuanzishwa kwa mitandao jamii ambapo watu wanaweza kuwasiliana na
  wananchi wao moja kwa moja .

  Mitandao jamii ndio haswa imechukuwa nafasi kubwa kwenye chaguzi
  mbalimbali kwa siku za karibuni kuanzia pale raisi wa marekani
  alivyokuwa anatumia mtandao wa youtube kuwasiliana na mashabiki wake
  mpaka serikali ya iran ilivyojaribu kufunga baadhi ya mitandao jamii
  isiweze kutembelewa na raia wananchi hiyo waliokuwa ndani ya nchi .

  Kilichotokea nchini iran sio harakati mpya tu kwa njia ya mtandao pia
  ni funzo kwa jamii zingine duniani sasa kuwekeza zaidi kwenye masuala
  ya ulinzi kwenye teknohama pamoja kuwa na wafanyakazi bora kwenye
  ulingo huu wa teknohama .

  Muda unazidi kwenda sana watu wanazidi kupata maendeleo sasa hivi
  inakadiriwa zaidi ya nusu ya watu wote duniani wanamiliki simu za
  mikononi na mitandao ya jamii inazidi kuchipukia kila kukicha pamoja
  na program mbalimbali za kutumia kwenye mitandao hiyo huku watu zaidi
  wakiunganishwa kwenye mtandao au huduma zingine za mawasiliano .

  Kwa mwendo huu wa kasi katika ukuaji wa teknohama ina maanisha huko
  mbeleni ujumbe unaweza kusambaa dunia nzima kwa sekunde tu au unaweza
  kusambazwa ujumbe kwenda kwa kundi Fulani la watu kwa sekunde tu
  serikali za sehemu hizo lazima zijue wajibu wake endapo chochote
  kitatokea .

  Utumiaji wa Teknohama haswa mitandao jamii inatofautiana haswa
  kutegemeana na vifaa vinavyotumika kwenye tovuti au anuani za mitandao
  mbalimbali mfano kwenye uchaguzi wa marekani mgombea uraisi wa
  marekani aliweka matangazo kwenye mtandao wa michezo ya kompyuta kwa
  ajili ya wachezaji wa michezo hiyo ,akaanzisha chaneli kwenye mtandao
  wa youtube .

  Hapa kwetu chama kinaweza kuanzisha channel yake kwenye mtandao wa
  youtube , inaweza kuanzisha blogu za wagombea wake kupitia tovuti ya
  chama husika na wagombea hao wanaweza kuanzisha kurasa zingine kupitia
  mitandao mingine kama facebook kwa ajili ya kuwasiliana na watu au
  twitter na mashabiki au wapenzi wao wanaweza kuwafuatilia moja kwa
  moja kutumia barua pepe au simu zao za mikono .

  Matumizi haya pia yanaweza kuleta changamoto kwa kampuni zinazozalisha
  magazeti au vyombo vingine vya habari vinavyotumia karatasi kwa ajili
  ya kuwasilisha taarifa zao kwa sababu wengi watakuwa wanafuatilia
  habari na matukio kutumia mitandao jamii ni vizuri kampuni za habari
  haswa magazeti kufungua kurasa zao za mitandao jamii ili kuweza kwenda
  sambamba na mabadiliko ya sasa .

  Kwa kumalizia naona kizazi kipya cha viongozi ambao hawashindi chaguzi
  kwa Wizi wa Kura au kutumia njia chafu bali kwa matumizi bora ya
  Teknohama haswa mitandao ya jamii ambayo wanaitumia kuwaunganisha na
  wapenzi na mashabiki wao wengine mifano iko wazi kuanzia kwenye
  uchaguzi wa marekani mpaka huu wa uingereza mwaka huu na hata raisi wa
  Venezuela anavyohangaika kwenye mtandao wa Twitter mpaka kuajiri
  wafanyakazi maalumu wa kuwasiliana na wananchi .

  Hata kama viongozi wengi hawapendi au hawana muda wa kujiunganisha
  kwenye mitandao jamii lakini wanaweza kuajiri watu kama Kiongozi wa
  Venezuela alivyofanya kuandika na kutoa huduma zingine kwenye blogu
  zao au kurasa zao za mitandao

  Kama unapenda kuingia kwenye Ulimwengu wa Mitandao jamii hizi ndio
  faida zake .

  1 - Watu wa Teknohama wanatumia muda mwingi kwenye Mtandao kuliko
  Televisheni na Radio kwahiyo una uhakika wa kunyanyuka .

  2- Huduma zake nyingi ni bure au zina unafuu na haziharibu kama
  mazingira kama mtu akiamua kubandika matangazo njiani na kutupa
  karatasi hovyo .

  3 – Huduma za Mawasiliano kwa sasa zimeshuka kutokana na sababu kadhaa
  na huduma hizo pia sasa zimekuwa na kasi kubwa pamoja na huduma hizo
  kupanuka maeneo mengi sana nchini .
  4 – Picha zinaongea zinaongea kuliko chochote unachoweza kufikiria
  wewe haswa ukipata mpiga picha mzuri na ziwekwe vizuri kwenye mtandao
  wako

  Unaweza kutembelea Anuani zifuatazo kwa uone jinsi unavyoweza
  kuzitumia kwenye shuguli zako za uchaguzi mwaka huu wa 2010

  www.youtube.com
  www.orkut.com
  www.ning.com
  www.twitter.com
  www.facebook.com
  www.blogger.com
  www.mozes.com
  www.ourmedia.com
  www.mybloglog.com
  www.othersonline.com
  www.presidentialquest.com
  www.NewsAssignment.net
  www.groups.yahoo.com
  www.groups.google.com
  www.Linkedin.com
   
Loading...