Matumizi ya mayonise katika chakula

Hii kitu huwa situmii hata kidogo sijui test yake

Wapishi wakija watatusaidia
 
Kama ni hivyo, basi msinunuwe madukani, tengenezeni wenyewe majumbani mwenu.

Mi naipenda sana mayo hakuna mfano ni umasikini tu unanisumbuwa. Vitu mhimu katika mayonnaise ni:

  • Kiini cha yai
  • Mafuta yoyote yatakanayo na mbegumbegu (olio di semi kwa kiitaliano) (alizeti, karanga, mahindi nk)
  • Ndimu
  • Chumvi

Tatizo linakuja wapi? mayonnaise ya dukani wanaweka yai zima na siyo kiini peke yake si unajuwa biashara? pili wanatumia mayai ya kuku wa kizungu (takataka), tatu wanatumia vinegar/siki (another takataka) badala ya ndimu fresh, na mwisho NYINYI MNAKULA TU BILA KUFANYA MAZOEZI YA VIUNGO, wapi na wapi.

Bali mayo ni nzuri kiafya kwa sababu kiini cha yai ni chakula tupu yaani kiini cha YAI hakitakiwi kigusane na moto kabisa kwa sababu ni lishe tupu, kina enzyme mhimu tofautitofauti 17, kina amino asidi mhimu kabisa ambazo mwili huzihitaji kila siku hii ikijumuisha mahitaji ya ubongo, mafuta yatokanayo na mbegu ni mhimu mwilini kwa ajili ya kutengeneza nguvu na homoni mbalimbali mhimu ikiwemo homoni za kuamusha ashiki, chumvi hasa ya baharini ambayo haijachakachuliwa ndiyo kila kitu mwilini, ndimu ndo usiseme mzizimkavu atakuletea notisi za ndimu utakimbia mwenyewe.

I LIKE HOMEMADE MAYO!
 
Mwaga basi maujuzi Fadhili tusizidi kujiua na vya kwa duka.
Hii hapa:


NAMNA YA KUTENGENEZA MAYONNAISE SAUCE:

vifaa mhimu:
mayonnaise.jpg


Mayonnaise sauce:
mahitaji:
  • Viini 2 vya mayai (vema kama unapata mayai ya kienyeji)
  • Kikombe 1 cha mafuta ya kupikia yatokanayo na mbegu mbegu (alizeti, karanga, mahindi, zeituni n.k)
  • Nusu ndimu
  • Chumvi
  • Siki (siyo lazima)

Namna ya kuandaa:
Mayai, Mafuta na Bakuli lazima viwe katika joto la kawaida (environmental temperature)

Ni mhimu kuheshimu uwiano wa kati ya mafuta na idadi ya viini vya mayai, zingatia kuwa kwa viini 2 vya mayai, mafuta yasizidi wala kupungua kikombe kimoja!


  • Weka katika bakuli viini vya mayai, ongeza kiasi cha chumvi na uanze kuchanganya au kupiga taratibu bila kupumzika kwa kutumia mchapo (whisker) au planetary.
  • Nyunyiza sasa mafuta kwa matone taratibu, ikiwezekana awepo mwingine atakayekuwa anayanyunyiza hayo mafuta taratibu kama matone ya maji huku wewe ukiendelea kupiga kwa mwendelezo, zoezi hili linahitaji walau muda wa nusu saa.
  • Kisha mara moja moja na kiasi kidogo kidogo kamulia maji ya nusu ndimu (ndimu fresh - usije ukanunua ya mchina itakuwa aibu ya mwaka), kufika hapa unaweza kuongeza kiasi kidogo cha siki iliyopashwa moto kidogo kama nusu kijiko cha chai.
  • Kama itatokea mayonnaise kuwa nzito sana mwishoni unaweza kuongeza kiasi kidogo cha maji ya vuguvugu.

Mhimu: Jikoni tunaposema kikombe 1 = Robo lita (250 ml)
Mayonnaise itakuja kuwa nzuri ikiwa tu mahitaji yako yote yatakuwa katika hali ya hewa moja.

Mayonnaise hutumika kusindikizia samaki, nyama, mboga za majani (saladi), mayai ya kuchemshwa, mkate (kama blueband mubadala), Sandwich, katika chips, n.k
 
Shukrani maana hadi leo niklikuwa na hangaika na ya kununua na huku wanaziuza bei gari. Sasa watakoma maana mayai kuku asili yapo kwa wingi
 
Mayonnaise no tamu lakini madhara yake ni makubwa...nmetumia miezi 3 mfululizo nkajikuta nmeongezeka tumbo, mwili na uzito takribani kilo 8.
Niko kwenye diet na mazoezi ili mwili urudi kama zamani.
Sio nzuri sana kiafya kama unatumia mfululizo kwa kua INA cholesterol nyingi.
 
Mimi kwakweli mayo imenishinda kabisaa....labda nitie kwenye nywele.

Shoti..hongera mpaka kwenye mkate
Hahah hata mm wakati niko umri flan ilikuwa haipandi kabisaaa,.ile harufu ndio usiseme,lakini pia si mtumiaji wa hii kitu sana naweza kuitumia kwenye chakula changu kwa mwaka mara 3..si kionjo muhimu sana kwangu hiki..
 
Back
Top Bottom