Matumizi ya Lugha ya Kiarabu kwenye kujifunza dini ya Kiislam ni utumwa wa hadharani

Last KING Ontuzu

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
587
783
Biblia ya kwanza kuandikwa iliandikwa kwa lugha ya Kigiriki, lakini inafundishwa kwa lugha zote no limitations za lugha.

Ila sisi Waislam kwanini tujifunze dini kwa Kiarabu, yaani hii naona sio sawa hadi azana asubuhi Kiarabu wasio Waislam wanasikia makelele tu maana hamna wanachoelewa.
 
Ibada/swala ya kiislam inahusisha kusoma surah za Qur'an, ukisema usome tafsiri za surah za Qur'an kwenye swala kwa lugha yoyote ile ni dhahiri itakua vurugu, sababu ili Aya zieleweke lazima pawe na maelezo ya ziada(mabano kwenye tafsiri) lakini pia ni kwa ajili ya uhifadhi wa Qur'an yenyewe,ili ibaki katika uhalisia wake
 
Biblia ya kwanza kuandikwa iliandikwa kwa lugha ya kigiriki,lakini inafundishwa kwa lugha zote no limitations za lugha
Ila sisi waislam kwanini tujifunze dini kwa kiarabu,yaani hii naona sio sawa hadi azana asubuhi kiarabu wasio waislam wanasikia makelele tuu maana hamna wanachoelewa.
Sema wao waislam, sio sisi waislam hali ya kuwa wew sio mwislam na ungekuwa mwislam ungejua kwann unatumia hiyo lugha. Pia biblia yakwanza haikuwa ya kigriki bali ilikuwa ktk lugha ya kiebrania
 
Niliwahi kumuuliza mwalimu mmoja wa dini ya kiislamu kuhusu hilo alilonijibu ni kuwa katika kuilinda isibadilishwe ni sababu mojawapo, akaniambia tofauti na vitabu vingine Kitabu hicho tangu kimeteremshwa hakijawahi kubadilishwa japo nukta, tofauti na vitabu vingine
 
Wameamua kutumia lugha ya kiarabu maana wanaamini maneno yaliyoandikwa na Mtume hayatakiwi kubadilishwa kwenda lugha ingine ili kutofifisha maana yake na walisema ni wajibu wa kila Muislamu kujifunza quran tukufu na kuihifadhi. Ni Imani yao jamani naomba tuheshimu,
 
Ni LAZIMA, kwasababu ndio lugha aliyoichagua Allah (S.A.W), na hata kama kuna tafsiri ni lazima uabudu na kuazini kwa kiarabu.
Screenshot_20220618-172437~2.jpg
Screenshot_20220618-172107~2.jpg
 
Biblia ya kwanza kuandikwa iliandikwa kwa lugha ya kigiriki,lakini inafundishwa kwa lugha zote no limitations za lugha
Ila sisi waislam kwanini tujifunze dini kwa kiarabu,yaani hii naona sio sawa hadi azana asubuhi kiarabu wasio waislam wanasikia makelele tuu maana hamna wanachoelewa.
Sababu wewe sio Muslim itoshe kusema ivo
 
Wanazuoni wanasema alla hasikii lugha yoyote zaidi ya kiarabu.

Ngoja tusubiri wajuzi zaidi watoe muongozo.

#MaendeleoHayanaChama
Kisha hao hao wanakwambia kuwa mungu wao ana uwezo wa kutenda kila kitu, sasa inakuwaje tena hasikii lugha yoyote hata kimang'ati nakati sisi Wasandawe tunayemwabudu Mungu katika roho na kweli hata tukimwomba hivi "nthatha, thathathatha" anatuelewa?

Au huyo mungu ana chembe chembe za ubaguzi nini

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Si kweli kwamba Allah/ Mwenyezi Mungu hasikii lugha nyingine huo ni upotoshaji mkubwa Sana,iweje aliyeumba mbingu na ardhi na vyote vilivyomo awe na mapungu hayo?

Pili Qur'an imeletwa Kwa Lugha ya kiarabu Kwanza kwakuwa Mtume wake alikuwa mwarabu,ili aifahamu ili kueneza ujumbe wa Mwenyezi Mungu,na pili kiarabu ni lugha tajir mno Kwa maneno yanayo jitoshereza.

Qur'an imetafsiriwa katika lugha mbali mbali duniani ikiwemo Kiswahili,Ila lazima maneno yake original lazima yawepo pembeni ndo tafsir inafuata hii yote ni kuhakikisha kuwa maneno ya Mwenyezi Mungu hayabadilishwi tofauti na vitabu vingine,Kwa mfano biblia ilirushukwa Kwa Lugha ya Yesu kiaramanic kama sijakosea,sasa kutoka lugha hiyo mpaka kigiriki kuna maneno mengi Sana yamebadilika maana yake,n kibaya Zaidi Injili halisi iliyoshuka Kwa Lugha ya kiaramanic,maneno yake hayapo pale,kwahiyo tofauti inaongezeka kila kukicha ndo maana si ajabu kukuta kuna tofauti kubwa au mapungufu mengi Sana ktk biblia, sasa kwakujua Hilo waislamu hawakutaka kurudia makosa ambayo wengine walifanya,ndio maana Leo hii hakuna mtu ambaye anaweza ichafua Qur'an Kwa kuingiza maneno mapya au kuyapunguza yatabakia vile vile milele.

Ila katika ibada ya Swala Qur'an itasomwa vile vile kama iliyoshuka na baadhi ya dua au maumbi yatabakia Kwa lugha kiarabu.

Ila cha kufurahisha zaidi,muislamu akienda mahala popote duniani hapati tabu ya kutekeleza ibada ya swala,Kwa kuwa IPO ktk original form yake Ile ile tangu awali.

Na hoja ya kusema sijui inapigwa adhana na wasio waislamu hawaelewi hiyo sio tatizo,adhana ni Kwa waislamu wanaitwa kwenda kumuabudu Mwenyezi Mungu,na tafsir yake ni: MUNGU MKUBWA,NASHUHUDIA HAPANA MOLA APASAE KUABUDIWA KWA HAKI ILA ALLAH,NA NINA SHUHUDIA MUHAMMAD NI MTUME WA MWENYEZI MUNGU,NJOONI KWENYE SWALA,NJOO KWENYE MAFANIKIO,MUNGU MKUBWA,HAPANA MUNGU APASAE KUABUDIWA KWA HAKI ILA ALLAH ( HUWA YANARUDIWA MARA MBILI MBILI)

Kwa ufahamu zaidi inaposemwa hapana mungu apasae KUABUDIWA Kwa HAKI isipo kuwa Allah, ni kuwa duniani kuna miungu mingi inaabudiwa,wengine wanaabudu wanyama,Moto,jua,wengine wana miungu ina nafsi tatu,wengine wanaabudu binadamu basi tafarani,kwahiyo miungu yote hiyo inawekwa pembeni anaabudiwa MMOJA TU AMBAYE NDIO MUWEZA WA KILA KITU HANA MSHIRIKA KATIKA UFALME WAKE NA WALA HANA MSAIDIZI,NA AKITAKA JAMBO LOLOTE LIFANYIKE,ANASEMA KUWA NA LINAKUWA.
 
Biblia ya kwanza kuandikwa iliandikwa kwa lugha ya kigiriki, lakini inafundishwa kwa lugha zote no limitations za lugha

Ila sisi waislam kwanini tujifunze dini kwa kiarabu,yaani hii naona sio sawa hadi azana asubuhi kiarabu wasio waislam wanasikia makelele tuu maana hamna wanachoelewa.
Kwanza sidhani kama wewe ni muislamu.

Pili, achilia mbali ukubwa na upana wa lugha ya Kiarabu, pia Qur'aan imeshushwa kwa lugha hiyo sababu Mtume alikuwa anaongea lugha na watu wake wa kwanza kuwafikishia ujumbe walikuwa ni waarabu, kisha baada ya hapo akawatuma maswahaba zake kufikisha ujumbe kwa watu wengine.

Tatu, Kiarabu hakijawahi kuwa kikwazo kwa Waislamu, sababu ya ile hali aliyo tupa Allah ya ukijifunza jambo lolote lazima utaliweza.

Nne, kama wewe kweli ni Muislamu na unaona Kiarabu ni kikwazo basi kaa ukijua wewe ni mzembe usie taka kuiua dini yako.

Tano, wanadamu tumeumbwa hatujui chocbote ila kupitia kujifunza na kutoa juhudi tukayajua tusiyo yajua.

Sita, ajabu ya elimu ukisoma historia ya lugha ya Kiarabu wajuzi wa kubwa wa elimu ya Kiarabu ukiwaacha wale wa kale, hawakuwa Waarabu. Sasa tutakushangaa wewe unasema kujua Kiarabu ni utumwa wakati muda huo huo kuna Mndeleko au Muafrika toka kabila la Fulani huko Afrika ya Magharibi yupo Saudia anawafundisha waarabu Kiarabu.
 
Wanazuoni wanasema alla hasikii lugha yoyote zaidi ya kiarabu.

Ngoja tusubiri wajuzi zaidi watoe muongozo.

#MaendeleoHayanaChama
Wanazuoni gani hao ?

Allah ndiye ameumba mataifa na makabila mengi ili tuoate kujuana, maana yake lugha zote anasikia na yeye ndiyo ameziumba ila huwa anateua katika viumbe vyake kuwakilisha vingine au kutumika badala ya kingine au vingine.
 
Allah Hawezi kubonga kifipa,kihaya,kisukuma,kizulu,kisandawe,kisambaa...Allah unaubaguzi sana, AN INDIGNANT TONE-ALLAH ACHA ZAKO!
Usiwe unaandika mambo ilimradi kufurahisha nafsi yako, bali andika ya maana kwa uadilifu.

Allah anasema :

13. Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari. (al-Hujurat : 13)

Maana yake hata uwepo wa makabila na mataifa ameyafanya yeye mwenyewe yawepo. Sasa vipi uandike uongo ?
 
Back
Top Bottom