Matumizi ya L kwenye R

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386

Hii clip nimeshindwa kuimalizia baada ya kuona hawa waandishi wanakosea kwa makusudi matumizi ya l na r.

Kuna mchungaji mmoja redioni niliacha kabisa kusikiliza mahubiri yake baada ya yeye kutumia “l” kwenye r.

Hawa watoto wamesomea uandishi kweli?

Wanatia kichefu chefu kama sio kuharibu lugha ya Kiswahili
 
Siku utakapo kutana na bosi hajui hio r na l lakini inabidi umsikilize tu ili upate pesa ndo utajua kama hizi lugha si chochote cha muhimu ni message
 
Mwenyekiti mwenyewe anachanganya matumizi ya L na R, je humsikilizagi?
 
Mtu wa media hatakiwi kuwa na mapungufu kama hayo ya lugha.
Truth comes with pain.

Siyo matamshi pekee. Kuanzia muonekano (kuvaa, kunyoa mpaka kutembea). In-short gestures zote ni muhimu kuzingatia.

Maneno sanifu ya kiswahili kama, kuhodhi, aghalabu, usuli, mawanda mapana, mantiki, zanambiu, ubazazi, kudurusu, kasri na orodha inaendelea... hayana nafasi kabisa kwa waandishi uchwara wanaoiharibu tasnia hii kila uchwao.

Huwa siangalii, sisikilizi na kusoma Swahili new's kutokana na hayo mapungufu.

Kwa mwandishi wa habari yeyote mwenye aidha Cheti/shahada Ni un-ethical kusoma, kuandika Kwa kutozingatia 5W and 1H.
 
Cha kushangaza wapo wengi sana wa aina hiyo. Sidhani kama waajiri wao wana uelewa huo.
 
Cha kushangaza wapo wengi sana wa aina hiyo. Sidhani kama waajiri wao wana uelewa huo.
Demi, huko katika taasisi za Uandishi & utangazaji ni gulio la kizota.

Zaidi sana, kujuana na kununuana kunauzwa katika mnada wa wazi. N'nachukizwa sana na hili.

Ni hivi, mmiliki wa Chombo cha Habari anapaswa kuajiri Mkurugenzi mwenye ubobezi & ujuzi kuhusu karia hiyo. Tatizo linakuja pale ambapo mmiliki anaingilia shughuli za kitaalamu.

Utasikia mmiliki anamwambia mwenye Taaluma;- Huyu mwuite katika usaili, huyu usimuite. Usitangaze habari hii, hii tangaza. Usiajiri mtu wa sampuli hii, huyu ajiri na kedi na inda za kategori hii.

Sasa kwa hali hii utegemee nini?. I beg, japo pitia (kama hukupitia) a, b, c's za Mass comm & Journalism. Walau utabaki mdomo wazi...Au tu pitia 5w & 1H In Mass comm & Journalism.

Binafsi ni bora ku-sucrifice ethic's zangu katika lolote lile kuliko kukubali kuendeshwa na M'miliki wa chombo cha habari.

Nb; I'm not a Journalist.
 
Hili ni tatizo la dunia nzima. Kila watu kutokana na asili ya lugha zao za asili kuna hefufi ambazo hata ukimwekea mtutu wa bunduki atatamka tofauti

MFANO
1. Mjerumani hata ufanyeje Roho atatamka Hoho

2. Mchagga piga garagaza hata akae ulaya miaka 20 kwenye " Z" lazima apatamke " S"

3. Mpare kwenye "S" ataweka "th" hivyo badala ya "Musa" Mpare ataita "Mutha"

3. Kanda ya ziwa yote, Singida hasa wanyiramba, Dodoma, Mikoa Iringa na Mbeya pamoja na mikoa mingi ya pwani penye "R" wanaweka "L" na Penye "L"wanaweka "R"

4.Mhindi hata umkate kichwa badala ya kusema WEWE atasema VEVE
 
Mbona hata katika jamii zetu matumizi ya R n L tunayaharibu hadi kwenye kingereza
Practical-mtu anasema Plactical
Read-mtu anasema Lead
 
Back
Top Bottom