Matumizi sahihi ya taa za gari.

Dereva Suka

Senior Member
Sep 25, 2014
176
500
Habari zenu wana jamvi...Mi napenda sana usalama barabarani....huwa naumia sana nikisikia ajali ambayo imetokana na uzembe au kutofuata sheria za barabarani....Haya ni matumizi ya taa za gari yakiyowekwa kisheria.

Tuanze na taa za mbele ya gari ambazo kimsingi zinatakiwa ziwepo taa za aina tatu....

1: Taa kubwa za mbele ambazo hutumika kuanzia giza linapoanza kuingia mpaka giza linapoisha asubuhi pamoja na sehemu zenye tunnel na nyakati za ukungu au mvua..

Taa mbili hizi kwa haraka unaweza ukasema zina matumizi sawa lakini kila taa ina kazi yake...yaani taa ya kulia ina kazi yake na ya kushoto pia....

Taa ya kulia ambapo ndio upande wa dereva kazi yake ni kumulika kuanzia mstari mweupe wa katikati ya barabara kuelekea kushoto ili kumrahisishia dereva unaepishana nae asipate shida sana wakati mnapishana....na taa ya kushoto kazi yake ni kumulika kuanzia mstari wa njano kuelekea kushoto ili iwe rahisi kuwaona waendesha vyombo vya baridi na watembea kwa miguu......taa kubwa zina low beam(mwanga usiomulika mbali) na high beam ( mwanga unaomulika mbali)....matumiz ya low beam kisheria ni pale .....

> Unapopita katika barabara yenye taa (taa za barabarani hasa mjini)
> Unapopishana na gari nyingine ni lazima na sio ombi kutumia low beam.
> Unapotaka kulipita gari la mbele yako (over take) ni lazima kutumia Low Beam kabla hujaanza kulipita gari hilo.

Endapo utatumia high beam wakati wa kuover take basi mwanga wa taa zako utapiga moja kwa moja katika kioo cha cha gar ya mbele ( side mirror) then mwanga ule utakuwa reflected kwa dereva unaetaka kumpita na kumsababishia kuanza kuyumba na hatimaye unaweza ukakosa njia nzuri ya kumpita.

2. Kuna taa za kuegeshea gari ( parking light) ambazo hutumika ukiwa umepaka gari lako pembeni ya barabara nyakati za usiku ili liweze kuoneka kirahisi. Ni muhimu sana taa hizi.

3. Taa za kuonesha uelekeo yaani indicators lights hizi ni taa ambazo kisheria zinatakiwa ziwe mbili mbele ya gari yako..yaani kulia na kushoto utawasha ya kulia kuonesha unaingia kulia na kushoto kuonesha unaingia kushoto angalau mita 30 kabla ya kufanya kitendo hicho.

Taa hiz zinaweza kutumika pia wakati ukivunja sheria kwa kuziwasha zote mbili kwa wakati mmoja yaani HAZARD ukionesha kuwa gari yako inaweza kusababisha maafa au ajali hivyo basi watumiaji wengine kuwa makini au na tahadhari dhidi ya gari yako...kuna aina tatu ya uvunjaji wa sheria kwa kutumia HAZARD.

Moja..kama gari yako ipo kwenye mwendo wa kasi kuliko mwendo ulioainishwa katika eneo husika( labda ni eneo la mjini mwisho 50 KMH lakini wewe una dharula ya mgonjwa unamuwaisha itabidi utumie HAZARD.

pili Kama unaenda kwa mwendo wa polepole sana kiasi ambacho unaweza kusababisha ajali...mfano njia za nje ya mji magari huwa yakienda kwa mwendo wa kasi...hivyo basi kama gari ina tatizo labda imeshindwa kuingiza gia zaid ya namba moja na kukulazimu kutembea mwendo wa gia moja ni lazima uwashe HAZARD.

Tatu Kama gari yako imeharibika barabarani na sehemu hiyo huruhusiwi kuegesha gari...mfano barabara zote ambazo zina mstari wa njano pembeni huruhisi kusimama bali unatakiwa uendelee mbele tu. Ukipata tatizo katika maeneo haya basi utavunja sheria ya kutokusimama kwa kuwasha HAZARD pamoja na kuweka vibao vya tahadhari.(triangles)

Uzi huu ni kwa ajili ya taa za mbele tu....nitaandaa uzi mwingine kwa ajili ya taa za nyuma ambazo jumla yake zipo sita...ni vyema ukajua matumizi yake kuepuka/kuepusha ajali na mambo mengine. Aksante kwa kusoma.
 

Dereva Suka

Senior Member
Sep 25, 2014
176
500
Mkuu ningekuomba unielimishe maana ya kuwasha taa na kuzima mara mbili au moja
Ni mojawapo ya ishara ambazo madereva huzitumia.....japokuwa sio rasmi sana.

1. Inaweza ikawa salamu
2. lakini taa zinaongea...kwa mfano unaweza ukawasha hivyo ukimaanisha unamruhusu mtumiaji mwingine wa barabara aendelee kwenda au apite au asubiri kwanza wew upite lakini pia unaweza kuziwasha hivyo kumuomba dereva mwenzako akuruhusu kupita kwanza.

Kwa kifupi inategemea na eneo au na wakati....kwa mfano mmi huwa nafanya hivyo nikiona gari ya mbele yangu ipo mwendo wa taratibu sana hasa mjini unakuta mtu anapiga story au anachezea simu....unaweza ukamshtua kwa kupiga honi au ukawasha taa(high beam) kumshtua.

Kwahiyo inategemea unataka kumaanisha nin na madereva wazoefu watakuelewa tu.
 

Konsciouz

JF-Expert Member
Aug 12, 2015
4,826
2,000
Mkuu ningekuomba unielimishe maana ya kuwasha taa na kuzima mara mbili au moja
Inategemeana na tukio... But mara nyingi hutumika kama pass kumruhusu mtumiaji mwingine wa barabara ie wenda kwa miguu na vyombo vingine vya moto ,kuomba ruhusa ya kupenya kwenye barabara either kuingia au kutoka na nyingine ni salamu tu.
 

Dereva Suka

Senior Member
Sep 25, 2014
176
500
Mkuu ningekuomba unielimishe maana ya kuwasha taa na kuzima mara mbili au moja
Wakati wa usiku unaweza kufanya hivyo kama gari unayotaka kupishana nayo imewasha full lights na inakuwia vigumu kuona...utamkumbusha dereva huyo kwa kufanya hiyo ishara...dereva mzoefu atakuelewa tu na hatimaye anarudi katika low beam.
 

CORAL

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
2,673
2,000
Mada yako ni nzuri sana ila naona ingenoga zaidi kama ungeongelea na rangi za taa unazoainisha. Taa za gari zina rangi tofauti tofauti kwa hiyo unapozizungumzia ukitaja na rangi nadhani itakuwa poa zaidi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom