Matumizi mbadala ya neti za Jakaya...

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
View attachment 57161
Katika pitapita yangu kijijini kwetu, nikabahatika kukutana na hii product mupya... Watanzania wanajaribu kuwa wabunifu ili angalau kupunguza makali ya maisha. Hii ni kamba ya kufungia mifugo kama mbuzi. Imesukwa kwa kutumia neti zile zilizogawiwa bure nchi nzima na Serikali kwa msaada wa wamarekani.
Sababu hasa iliyomfanya mwananchi huyu kuamua kubadili matumizi ya neti zile alidai ni kutokana na neti zewenye kuwa ndogo sana...

Kuna picha nyingine jamaa wanavulia samaki naitafuta hapa...
 
Jambo la kuogopesha zaidi ni hali ya afya zetu ,kwa sababu hizo neti kila ukiamuka asubui lazima upige sana chafya kwa mafua , hivi nyie wenzangu misaada ya wamarekani mnaimani nayo?angalia Iraq, Afghanistani sijui kwengine vipi Mmarekani sio watu wale
 
Tusiendekeze upungufu wa kufikiri tunadhani kila mtu hana akili..... hata wahalifu wanaotafutwa kwa kosa la kuvua samaki wadogo na nyavu ndogo (neti) kinyume cha sheria watatueleza hivyo hivyo....hapana.

Nani kasema watanzania tunalalia vitanda size moja? kama chandarua ni kidogo kuliko kitanda chako yuko mtanzania mwingine anahitaji sana chandarua hicho kwa kitanda chake kinachotosha.
 
Zile sio neti bali nyavu aisee....zimekakamaa hizo...

Msaada haulazimishwi kuna watanzania wanahitaji neti hizo kwa sababu hawakuwa na uwezo wa kununua zilizo bora zaidi muhimu ni kuzuia mbu ......

kama huzihitaji neti hizo sio lazima kuchukua ni msaada hakuna aliyezitolea fedha yake
 
Tusiendekeze upungufu wa kufikiri tunadhani kila mtu hana akili..... hata wahalifu wanaotafutwa kwa kosa la kuvua samaki wadogo na nyavu ndogo (neti) kinyume cha sheria watatueleza hivyo hivyo....hapana.

Nani kasema watanzania tunalalia vitanda size moja? kama chandarua ni kidogo kuliko kitanda chako yuko mtanzania mwingine anahitaji sana chandarua hicho kwa kitanda chake kinachotosha.

usilete porojo hapa, hizo neti hazifai, na wakati mwingine ni bora ukawa mkweli kuliko kua mnafiki kisa unakula buku mbili kutoka kwa Nape kisa umetetea CCM, unaridhika na hali ya maisha ya watanzania sasa hivi?
 
Msaada haulazimishwi kuna watanzania wanahitaji neti hizo kwa sababu hawakuwa na uwezo wa kununua zilizo bora zaidi muhimu ni kuzuia mbu ......

kama huzihitaji neti hizo sio lazima kuchukua ni msaada hakuna aliyezitolea fedha yake

Kwa hiyo msaada ndio kisingizio cha kupewa bidhaa sub standard??? Acha hizo wewe...mimi sipigi siasa zenu za CCM vs CDM hapa!!
 
Eti chandalua inatumika miaka tano bila ya kuweka dawa yeyote.

Wewe teremsha na kufua tu!
Kwa kweli hili limenipaga hofu sana na sijawahi kutumia na nimeizungushia banda la kuku.
 
Usichotolea fedha yako hata mbwa unaweza kufugia ndivyo waafrika tulivyo.....

Kwani hata kama ni kununua hizo net hazistahili kuuzwa hata kwa sh.2000.Acheni fikra mgando msaada isiwe
sababu ya kuwapa watu kitu kisichostahili ni udhalilishaji kwa wananchi.Hao wazungu wanaotuletea hizo net
kwa kisingizio cha msaada ndio hao wanaochukua madini yetu na kutuachia mashimo kwa mrahaba kiduchu.
Please think twice!!
 
mi zimenisaidia kweli nimetengenezea banda la tetere na khanga.. baada ya kugundua hazinifai kwa matumizi ya kujikinga
 
Usichotolea fedha yako hata mbwa unaweza kufugia ndivyo waafrika tulivyo.....
kwani mbwa hana haki? nani kakwambia msaada ndo uwe kitu kibovu? Neti zina mitundu mikubwa hata inzi anapita! Huo ni msaada au mateso?halafu eti zina dawa ya miaka 5 mbu akikatiza anakufa, na huyo binadamu anayevuta hiyo sumu kwa miaka 5 atakua katika hali gani? HIZI NETI SI MSAADA NI KAMPENI PUNGUZA WATANZANIA.
 
Msaada haulazimishwi kuna watanzania wanahitaji neti hizo kwa sababu hawakuwa na uwezo wa kununua zilizo bora zaidi muhimu ni kuzuia mbu ......

kama huzihitaji neti hizo sio lazima kuchukua ni msaada hakuna aliyezitolea fedha yake

misaada kila wakati inadumaza akili inawafanya viongozi wetu wanashndwa kuwa wabunifu wavyanzo vyamapato kwakuwaza misaada,miaka 50 ya uhuru bado tunomba mpaka neti!huu ni udhaifu.ssa ivi masharti ya misaada yamebadilika labda viongozi wetu watachangamsha vichwa.vinginevyo tutarajie kuona ndoa za jinsia moja.
 
Mama porojo rudi hapa tafadhali unijibu hili, KWANINI KADIRI MISAADA YA HIZI NETI INAVYOZIDI KUWAFIKIA WANANCHI NDO WANAUME WENGI WANAVYOZIDI KUPOTEZA NGUVU ZA KIUME?
 
chandalua hizi kwetu tunatengeneze wigo kwenye kitalu cha bustani kuzuia kuku wasiharibu mboga ngumu kama nyavu za kuvulia samaki
 
misaada kila wakati inadumaza akili inawafanya viongozi wetu wanashndwa kuwa wabunifu wavyanzo vyamapato kwakuwaza misaada,miaka 50 ya uhuru bado tunomba mpaka neti!huu ni udhaifu.ssa ivi masharti ya misaada yamebadilika labda viongozi wetu watachangamsha vichwa.vinginevyo tutarajie kuona ndoa za jinsia moja.

Hili taifa bwana nalenyewe dhaifu kama raisi wao

Hapa ni wavuvi wanaanikia Dagaaa

Malaria-Bed-Nets-Malawi.jpg

Wana wa Pakaya hawa nao hawako nyuma

IMG_4180.JPG

Hapa chandarua kinatumika kama pazia la chooni! Ubunifu huu

bednets1-500x375.jpg

lakini mambo haya si bongo tu soma zaidi hapa

http://www.malariajournal.com/content/pdf/1475-2875-7-165.pdf
 
Eti chandalua inatumika miaka tano bila ya kuweka dawa yeyote.

Wewe teremsha na kufua tu!
Kwa kweli hili limenipaga hofu sana na sijawahi kutumia na nimeizungushia banda la kuku.
Hii ndo point alonipa mama mmoja kutoka kijiji cha MGONGO (JIMBONI KWA MH MWIGULU) Mama huyu alisema kwamba alitumia neti hii kwa mwezi mmoja tu akawa ana mafua yasiyoisha. aliponunua neti nyingine basi mambo yakawa powa kabisa. alichofanya ni kuchukua neti hii na kuifanya fensi ya kuku wake. Nilipofika nikamuuliza why anatumia neti kama kibanda cha kuku, naye hakusita kusema kwamba hata kuku wanahitaji kukingwa dhidi ya magonjwa mengine pia. nilipoongea nae sana mambo ndo yakawa hivyooooo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom