Matumizi mabaya ya simu zetu

kikale

JF-Expert Member
Oct 14, 2012
455
574
Habari za asubuhi wakuu.Poleni na machovu ya usingizi wenye madhila kwa wale waliolala hali ya kuwa miili yenu ingali na maumivu.Pia hongera kwa kuamka salama kwa wale tulio amka pasi na matatizo ya afya...Yote ya yote,tumshukuru mungu kwakuwa ni Matakwa yake..Narudi kwenye Mada......
Watanzania tubadilike,tuwaheshimu na kuwathamini ndugu zetu wanaopata ajali, leo yeye kesho wewe,haiwezekani watu wanapata ajali wewe unaconcetrate kupiga picha. watu wamejeruhiwa na wengine kupoteza maisha wewe unakazana kupiga vipicha vyako badala ya kutoa msaada, roho hii tunatoa wapi...?

Niliwahi sikiliza speech ya Mkongwe wa uandishi wa habari Jenerali Ulimwengu siku ya tuzo za waandishi wa Habari akieleza namna siku hizi habari zinavyopotoshwa kwa Maneno na Picha, akasema kutoa picha ya Mtu aliyekufa ama kupata ajali mbaya hadharani si maadili ya uandishi wa habari. Sasa wewe na mimi ambaye si mwandishi wa habari ambaye unataka ufanye kazi ya uandishi wa habari unajua hilo ni kosa...? binafsi yangu niliguswa na maneno yake, nmejifunza na nimeacha, wew je...?

Ikikumbwe mtu anapokufa kuna kudhalilika, kunaaibu sasa wewe na kasimu kako Mtu hajasitiriwa wewe upo tu, nadhani kunahaja ya TCRA kuangazia jambo hili, kwa sababu naamini hata wew ukifia ucngependa udhalilishwe ivo? Jenerel Ulimwengu anasema japo Marekani ndo teknolojia ilipo hawafanyagi upuuzi huu, huwezi kuta Maiti ya kimarekani imedhalilishwa kwenye mitandao kiasi hicho wanaheshimu Utu wa Mtu.

Plz mnaofanya ivo muache mnasababisha maumivu kwa ndg wa marehemu lakini pia kitendo hichi kinaondoa ubinadamu wetu.
 
Back
Top Bottom