Matumizi mabaya ya Ofisi na ubadhilifu ndani ya Ngorongoro

BITALA

Member
Jan 10, 2015
26
26
MATUMIZI MABOVU YA OFISI NDANI YA HFADHI YA NGORONGORO

Mheshimiw Rais shikamoo. Napenda kukupa pole wewe na serikali yako yote kwa ujumla kwa majukumu mazito ya ujenzi wa Taifa letu. Mwenyezi Mungu aendelee kuwapa nguvu na hekima ili tuweze kufikia malengo tuliyojiwekea kama Taifa

Watanzania wenzangu wakati Serikali ikiendelea kupambana kuhahikiksha kila mwananchi anafaidika na keki ya Taifa ila bado wapo watanzania wachache waliopewa nafasi mbalimbali za kiutumishi kuendelea kuishi maisha ya ajabu na kujiona wao hakuna wa kuwagusa na kusahau kwamba Serikali ina macho kila sehemu ya nchi hii. Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na kufanya vizuri kwa baadhi ya watendaji ila bado wengine ambao hawaelewi na wanafanya makusudi kwa kujitamba kwamba hakuna wa kuwagusa.

  • UDHAIFU WA IDARA YA UTUMISHI
Idara hii imekuwa chimbuko la migogoro isiyoisha katika hifadhi hii. Wafanyakazi walitegemea baada ya ujio wa watumishi wapya wa idara hii labda ingesaidia kutatua migogoro ya kimaslahi ya wafanyakazi iliyosababishwa na watangulizi wao lakini ndo imekuwa na uozo usioelezeka sijui ni kwanini watumishi wa idara ya utumishi wa hifadhi hii kwa miaka yote wamekuwa wakiminya maslahi ya wafanyakazi na kupendwa kunyenyekewa. Upendeleo wa mishahara na benefits nyingine umekuwa ni wa kiwango kisichoelezeka nimelizungumzia sana hili jamb kwa muda mrefu ila baadhi yao walisema kwamba ni majungu, lakini kwenye kikao cha wafanyakazi kilichofanyika makao makuu tarehe 27.01.2020 viongozi wa juu wa shirika walikiri kwamba Tume ya utumishi iliyokuja kufanya kazi libaini mapungufu makubwa kwenye mishahara ya wafanyakazi na kupelekea baadhi yao kupewa mishahara binafsi lakini mpaka leo hakuna mfanyakazi hata mmoja aliyepewa barua ya mabadiliko ya mshahara. Swali la kujiuliza hapa ina maana idara nzima ya utumishi katika hifadhi hii ilishindwa kufanya kazi mpaka iundwe tume toka utumishi kubaini madudu hayo? Mwenye nyumba unashindwa kupangilia nyumba yako mpaka jirani aje abaini mapungufu wakati wewe unalala hapo kila siku? Nilisema na ninaendelea kusema ili kuondokana na migogoro isiyo ya lazima ni vyema bodi ikatangaza ajira wakapatika watu wenye uelewa mpana na waadilifu hawa vilaza hawawezi viatu walivyopewa ni vikubwa mno. Kuendelea kuwakumbatia hawa vilaza migogoro isiyo ya lazima haitokaa iishe kwenye hifadhi hii. Hebu fikiria mfanyakazi ameajiriwa mwaka 2010 akiwa na shahada moja na mwingine anaajiriwa mwaka 2017 akiwa na diploma anamzidi mshahara unategemea upendo utakuwepo? Unakuta kwenye idara wachache ndo wanaofaidika wengi wanaachwa mnategemea maelewano yatakuwepo? Mbaya zaidi watu wakilalamika mnasema ni majungu mnawaona wabaya nia kuwatafutia adhabu mnakosea sana na mnajitafutia shida na msipobadilika msitegemee mtaachwa kuandikwa hilo mlisahau kabisa maana hilo shirika ni mali ya umma sio duka la mtu binafsi. Dr Manongi hawa watu wanakuangusha sana jitahidi kuwa mkali maana siku zote kamba hukatikia karibu na mwisho.

  • UZEMBE MAFUNZO YA JESHI USU KITUO CHA MBULULBULU
Serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii imeanzisha mafunzo malumu ya kijeshi kwa ajili ya kuongeza ulinzi katika hifadhi zetu. Kilianzishwa chuo cha mafuzo haya kilichopo Mlele mkoani Katavi ambapo wapo wakufunzi walioboboea kwenye uhifadhi kutoka TANAPA wanaoendelea kutoa mafunzo haya mazuri kwa watumishi. Ila kwa hifadhi ya Ngorongoro imekuwa tofauti kabisa baada ya kuletwa mkuu mpya wa idara ulinzi Kanali Kilugha ameamua kutowatumia wahifadhi waliobobea kwenye uhifadhi badala yake ameleta kikosi cha kijeshi. Si jambo baya lakini njia inayotumika sio sahihi. Mnapaswa mjifunze kwa wenzenu wa TANAPA walipochagua askari wa uhifadhi walio makini na kuwapeleka mafunzo ndani na nje ya nchi na waliporudi wao ndio wameendelea kuwapa mafunzo watumishi wa TANAPA. Kilugha nilshawaambia hayo mafunzo si ya kujiandaa na vita ni kwa ajili ya mbinu za uhifadhi sasa nyie mnaendelea kutoa mafunzo yasiyo na tija kwenye uhifadhi. Kwa miaka yote hao unaowaamini hawakuwepo ndani ya hifadhi je nini kilikuwa hakiendi sawa? Acheni ujuaji usio na manufaa kwa hifadhi na nchi kwa ujumla. Hicho chuo chenu cha mbulumbulu bado hakijawa na sifa kama cha Mlele katika kutoa mafunzo zaidi mnalazimisha ili mchote hela shauri yenu pesa ya serikali si ya kuchezea. Dr Manongi je una taarifa kwamba baadhi ya wakufunzi wanaotoa mafunzo kituo cha mbulumbulu si waajiriwa wa wizara ya maliasili na utalii, JWTZ wala hifadhi ya Ngorongoro na hawana sifa hata moja za kuwa wakufunzi wa mafunzo ya kijeshi? Fuatilia utalibaini hilo na kama wakibisha tutaweka majina ya wahusika hadharani. Hii yote inatokea kwa sababu mmeendelea kuwaamini na kuwatumia watu wa nje kuliko askari wenu wa ndani. Acheni kufanya mambo yasiyo kisheria mtasababishi hifadhi yenu hasara kubwa sana ikiwa watu wakiamua kufuata mkondo wa sheria. Mmeajiri vijana wa watu bila kuwaambia kuna mafunzo baada ya kuingia kazini mmewapeleka mafunzo hichao chuo cha mbulumbulu bila hata kupima afya zao kama wataweza kuvumilia na baadhi mpaka leo wanatembelea magongo. Mnatoa mafunzo ambayo mtaala wake haujapitishwa kisheria na mbya zaidi wanaotoa hawana utaalamu wa mambo ya uhifadhi. Wazo la jeshi ni zuri sana ila utaratibu mnaoutumia utakuja kuwaletea shida kubwa mno na hasara kubwa kwa shirika.Watumieni wanajeshi hao kuwapa mafunzo askari wenu wa ndani halafu hao watakaopewa mafunzo ndo wawe wanatumika kuwafundisha wafanyakazi wengine. Vilevile sitisheni kwa sasa mafunzo kwenye chuo cha mbulumbulu wapelekeni wafanyakazi wenu chuo cha mlele kwenye walimu waliobobea kwenye mafunzo ya kijeshi eneo la uhifadhi. Sasa hivi pesa zote zinaelekezwa kwenye jeshi usu na kusahau kabisa maeneo nyeti kama miundombinu ndani ya hifadhi mfano barabara.

Mheshimiwa Kigwangalla nakuomba kwa nafasi yako kama Waziri uunde tume ya kubaini chanzo cha kifo cha askari marehemu Mussa laizer ili kuhakikisha hali hii haitoendelea kujitokeza na kupoteza maisha ya watanzania wenye moyo wa kulitumikia Taifa lao.

Mwisho kabisa naendelea kuwaasa wafanyakazi wa hifadhi hii mjitahidi kuishi kwa kufuata sheria na taratibu na wenye nafasi za uongozi msibague wasaidizi wenu endeleeni kudumisha mshikamano kama anayoishi Dr Manongi. Mkifanya mambo yaliyo kinyume na utaratibu mtaendelea kuanikwa hadharani ili watanzania wajue mwenendo mzima wa shirika. Kazi ya umma haihitaji nyodo maana muda na saa yeyote unaweza kutoka ulipo na kupelekwa sehemu yeyote ya nchi.

Wabheja sana

BITALA
 
Fitna zinaandaliwa. Hapa anatafutwa Dokta Manongi tu. Ukaguzi unapofanywa na wakaguzi wa nje unakuwa na tija. Pili, askari wanyamapori kabla ya kuajiriwa lazima ithibitike kuwa afya zao ni njema. Kuumia mazoezini ni jambo la kawaida. Kumbuka Jeshi Usu ni Jeshi. Huwezi kuwa na 'wanajeshi' wanaofundishwa na sungusungu.
Acheni watu wapige kazi
 
Kaka, wenzako waliotoa taarifa za barabara mbovu wako jela now so kuwa makini
 
Mpitishie hii barua Waziri wako wa maliasili na utalii Mh. Kigwa...
 
Nilichojifunza mimi baada ya tukio la kurushwa kwa ile clip ya ubovu wa barabara ngorongoro na muitikio wa watu nilijua kua mambo mengi yanayohusu au yanayofanyika uko mahifadhini au maporini mengi hayajulikani aidha kwasababu yanafichwa au kwavile nimambo yamaporini hakuna access kubwa ya taarifa zake kutoka ila ukitazama kwa mapana utaona uko kuna mambo mengi sana ya ovyo.Mimi naamini Uko ngorongoro na Tanapa kuna ubadhirifu mkubwa sana ila ndo hivyo mambo yanaishia ndani kwa ndani. Nadhani wahusika wakufwatilia hayo uliyoyasema watalpata hizi taarifa nakuzifanyia kazi endapo zitakua kweli hatua zitachukuliwa na endapo pia wewe mtoa mada ndo utakua umetoa taarifa yauongo hatua zaweza chukuliwa pia.
 
Back
Top Bottom