Matumizi mabaya ya mali ya umma

nguvumali

JF-Expert Member
Sep 3, 2009
4,923
1,325
15967_549125861790956_512865710_n.jpg
15967_549125861790956_512865710_n.jpg
1079391_549123011791241_2034649769_n.jpg

hilo ni gari la serikali linalotumiaka na kituo cha Afya Ilembo..Mbeya Vijijini limekutawa likipakia abiria.
[h=5] Hii ni hatari kwa maana Mkuu wa afya anashirikiana na dereva wake katika biashara husika.
nauli kutoka Mbalizi hadi Ilembo ni Tsh.4000.
Mamlaka husika mpo wapi? hebu njoo mpate taarifa kamili kupitia 0688076376.
[/h]
 
Kila mtu ameamua kufanya biashara kwa kamba yake. Kama biashara zinafanyika ikulu, seuze kwenye ambulance. Waongezee na magunia ya mkaa!
 
Kila mtu anakula urefu wa kamba yake, mpaka 2015 Taifa litakuwa limebaki scraper ! Mungu atunusuru
 
15967_549125861790956_512865710_n.jpg
15967_549125861790956_512865710_n.jpg
1079391_549123011791241_2034649769_n.jpg

hilo ni gari la serikali linalotumiaka na kituo cha Afya Ilembo..Mbeya Vijijini limekutawa likipakia abiria.
Hii ni hatari kwa maana Mkuu wa afya anashirikiana na dereva wake katika biashara husika.
nauli kutoka Mbalizi hadi Ilembo ni Tsh.4000.
Mamlaka husika mpo wapi? hebu njoo mpate taarifa kamili kupitia 0688076376.

natamani ningekuwa konda....manake nisingekosa hata buku 10 za futari jioni.suka mwenyewe ningempiga bao tu.
 
Maisha bora kwa kila mtanzania. Serikali corrupt haiwezi kusimamia rasilimali zake ipasavyo, haiwezi kukusanya kodi zake vilivyo. Maneno haya aliyasema baba wa taifa na ndicho kinachotokea kwa sasa
 
acha umbea mtoto wa kiume, ugomvi wenu wa kilabuni usiulete hapa, mbona picha haionyeshi kama kuna hela inakusanywa?
 
Mkubwa inawezekana kuna ukweli katika hili, ila ushahidi wa picha peke yake kama hivi sitaki kuuchukulia kwa uzito uutakao wewe, mbona ni kama gari limepigwa picha lenyewe kama lenyewe tu? Ungejaribu kuvizia wakati ngoma imekula nyomi ingekuwa na nguvu sana mkuu
 
acha umbea mtoto wa kiume, ugomvi wenu wa kilabuni usiulete hapa, mbona picha haionyeshi kama kuna hela inakusanywa?

Duuuh na wewe vipi ! nimeweka hadi namba yangu kwakua nina uhakika na nilichosema, na kwa taarifa tu nimepigiwa simu na watendaji wa Hamshauri husika na uchunguzi umeanza kubaini ukweli huo !

sijaandika lolote la Umbeya na ushahidi zaidi nimeukabidhi ofisi za Hamlshauri kwa taarifa zaidi
 
Back
Top Bottom