Matumizi mabaya ya majina ya Idara nyeti kitaifa yadhibitiwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matumizi mabaya ya majina ya Idara nyeti kitaifa yadhibitiwe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by zaleo, Apr 15, 2012.

 1. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Nilipopita pale Muhimbili majuzi tu, kwa mng'arisha viatu, nilikuta jamaa mmoja anatamba kwamba anataka kuwafunga madaktari wa Muhimbili sababu walimzuia kutibu wagonjwa wanaodaiwa hahusiki nao, yeye mwenyewe baadaye niliambiwa ni daktari wa meno. Inadaiwa alienda mapokezi idara ya dharura akawa anatibu pale. WAlipomuuliza wewe nani akadai ni daktari. Walimwambia hawamjui pale idarani atoe kitambulisho, akawa anajibu hovyo. Walichukuwa faili alilokuwa nalo kuzuia asiendelee kutibu. Lakini yule bwana anadai ndani ya faili kulikuwa na kinasa sauti alichopewa Ikulu ili arekodi madaktari wakati wa mgomo na anadai katika purukushani hiyo kilipotea.

  Nilipodadisi zaidi nikagundua jamaa ndio zake hizo, kujidai yeye ni msalama wa Taifa na yuko kwenye pay roll Ikulu. Anatumia mbinu hiyo kuwatisha madaktari miaka mingi sasa, wengine aliwasababishia kuundiwa tume ya haki za binadamu na wengine Blandina Nyoni katibu Mkuu wa Afya wa zamani na Mtasiwa wake walimkingia kifua sana huyu bwana. Inasemekana Mkurugenzi Mtendaji wa MNH aliyeondoka aliwahi kumfukuza aondoke MNH kwa kuvuruga amani pale lakini Nyoni na Mtasiwa wakamrudisha kwa nguvu kuendeleza vurugu zilezile kama kawa. Sijaona barua lakini inadaiwa ameshaandika na kutawanya nakala hata kwa Rais wa nchi na kila mahali akilialia kutaka kufukuzisha watu kazi kwa sababu zilezile, kwamba aliajiriwa na Ikulu alipookotwa Malawi??? kwa ubingwa wake. Sijui ni bingwa wa nini, lakini kwa sasa kuna sokomoko pale Emergency linaendelea. Kuna madaktari wengine ili awanase amewachomekea rushwa na halafu anawapeleka PCB. Karibuni inadaiwa (kutoka vianzo vya walioko karibu naye) alienda Baraza la mitihani kutaka wamsaidie kufoji cheti cha msichana wake mmoja aliyegundulika kafoji cheti, waliomgundua ni walewale wa Baraza la mitihani. Nako alienda akitumia kofia ya Ikulu na usalama wa Taifa.

  Kitu kimoja kinashangaza, hivi ikulu na Usalama wa Taifa wanaruhusu upuuzi huu kutumika chini ya majina yao? Nao madaktari wa Muhimbili, kumbe ni waoga kiasi hicho kwamba mtu mmoja anawaendesha hivyo na hamna kauli? Au tuseme hamna masikio na afanyayo hamsikii wala kuona? Nilimuona kwa macho yangu yule jamaa nikakerwa sana baada ya kutafuta ABC zake kiasi. Usiombe ukaingia mikononi mwake akutibu. Lakini utajuaje ni huyo ndiyo sekeseke lingine. Inadaiwa wanamuuliza aseme ni bingwa wa nini lakini anasema "mimi dentisti". Sikujua hiyo ni ubingwa, kwani kila dentist ni bingwa? Anaweza kutibu kila mahali hata kuzalisha waja wazito? Jamaa yule mwisho sana.

  hebu tupeni zaidi watu mlioko Muhimbili, tujue ukweli.
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  huwezi jua labda ndio kazi yake aliyopangiwa
   
 3. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Baraza la madaktari Tanzania MAT wanapaswa kushughulika naye, ni nyoka ndani ya jumuiya ya madaktari mwenye sumu mbaya sana. Kwani kama serikali ikirekebisha mafao ya madaktari yeye huyo jamaa atakataa kupokea? Wanapogombania wenzake mambo ya wote anatangulizaje tumbo lake mwenyewe? Nadhani madaktari watakuwa wanamjua vizuri, labda wanaogopa nguvu yake. Hebu Muhimbili mtafuteni nyoka huyo na shughulika naye kabla hajachafua hewa zaidi. Anzia Dental na Emergency ambako kumetajwa kuhusika kwake, atajulikana tu. I tell you ooo!
   
 4. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo na UWT wanatumia mbinu chafu namna hii kufanya uchunguzi?.
   
 5. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Gama, mbona sijakuelewa? Umeandika kitu kisichofanana na mada, labda ni kwa bahati mbaya.
   
 6. J

  Juma123 Senior Member

  #6
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 193
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35

  nadhani wew ndiye hujaelewa, uwt ni usalama wa taifa, na si umoja wa wanawake tanzania !!!!!
   
 7. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  teh teh teh teeeeeeeh! vifupi ndio madhara yake mkuu! kumbe ndio uwt? teh teh teeeeeeeeeh!
   
Loading...