Matumizi mabaya ya jina la JK - Taarifa toka Ikulu

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
734
Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imekuwa ikipokea mamia kwa mamia ya mialiko ya kumwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kushiriki katika shughuli mbali mbali za wananchi ziwe za maendeleo, ama za sherehe, ama za kidini ama nyinginezo.
Ofisi ya Rais inaiona mialiko hiyo kwa Mheshimiwa Rais kuwa jambo zuri na jema linaloonyesha mahusiano mazuri kati ya Mheshimiwa Rais na wananchi. Ofisi ya Rais inawaomba wananchi, taasisi na vikundi mbali mbali kuendelea kutuma mialiko yao ya kumwomba Mheshimiwa Rais kushiriki katika shughuli zao.
Kutokana na mialiko hiyo, tokea kushika uongozi wa nchi yetu Mheshimiwa Rais ameshiriki katika mamia ya shughuli zikiwamo za kufungua miradi ya maendeleo – kama vile miradi ya elimu, miradi ya afya, miradi ya barabara na miundombinu mingine, harambee za kuchangisha fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbali mbali nchini na shughuli nyingine nyingi za kuleta maendeleo ya wananchi. Miradi hiyo imebuniwa na kutelekezwa na taasisi na watu wa madhehebu mbali mbali ya kidini, Kiserikali na taasisi zisizokuwa za Kiserikali.
Ofisi ya Rais inachukua nafasi hii kuwapongeza watu ambao wamebuni na kufanikisha miradi hiyo. Ofisi ya Rais pia inapenda kuwathibitishia wananchi, kwa mara nyingine tena, kuwa Mheshimiwa Rais Kikwete anafurahishwa na ushiriki wakati wa uzinduzi wa miradi hiyo. Ataendelea kufanya hivyo bila kuchoka kwa sababu maendeleo ya wananchi ni jambo lililoko moyoni mwake na ni jadi ya imani yake ya kisiasa.
Mheshimiwa Rais kwa kadri muda na nafasi yake ilivyoruhusu amekubali kushiriki katika shughuli hizo za wananchi. Utaratibu uliopo ni kwa waombaji kupeleka barua za maombi kwa Katibu wa Rais, Ofisi ya Rais, Ikulu ama kufikisha maombi hayo kwa Katibu wa Rais kupitia Wizara husika.
Ofisi ya Rais kwa kuzingatia ratiba ya shughuli za Rais ndiyo yenye dhamana ya kutoa majibu kwa waombaji kama inawezakana Mheshimiwa Rais kushiriki katika shughuli aliyoombewa ama haiwezekani, kutegemea na nafasi ilivyo katika ratiba ya shughuli za Mheshimiwa Rais. Ni baada ya kupokea majibu na uthibitisho kutoka Ofisi ya Rais, ndipo mwombaji anaweza kutoa matangazo kuhusu kushiriki kwa Mheshimiwa Rais kwenye shughuli waliyompangia kufanya, na siyo vinginevyo.
Tunasikitika kusema kwamba katika siku za karibuni wamejitokeza baadhi ya watu na taasisi ambazo zinakiuka kwa makusudi utaratibu huo uliowekwa na hivyo kutumia vibaya fursa ya kumwomba Mheshimiwa Rais kushiriki katika shughuli zao wanazopanga kuzifanya.


Watu hao na taasisi hizo zimekuwa zikitangaza katika vyombo vya habari ushiriki wa Mheshimiwa Rais kwenye shughuli zao hata kabla ya maombi yao hayajajibiwa na Ofisi ya Rais na kupata ridhaa ya Mheshimiwa Rais. Wengine wamekuwa wanatoa matangazo yanayosema Mheshimiwa Rais atashiriki katika shughuli zao wakati hata mwaliko wenyewe haujatumwa kwa Mheshimiwa Rais au Ofisi yake.
Huu ni ukiukwaji wa taratibu na ni matumizi mabaya ya jina la Mheshimiwa Rais. Tunawasihi wanaofanya hivyo waache tabia hii mara moja na badala yake wafuate utaratibu uliowekwa. Ni makosa kutangaza ushiriki wa Mheshimiwa Rais kwenye shughuli yoyote kabla ya kupata majibu na uthibitisho wa kushiriki kwake kutoka Ofisi yake.
Hakuna shaka kuwa sote tunafahamu kwamba Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ni kiongozi anayependa sana kushiriki katika shughuli zote za wananchi zenye kuwaletea maendeleo, na ataendelea kufanya hivyo bila kusita wala kuchoka. Tunachowaomba ni kwa waombaji wa fursa hiyo ya Mheshimiwa kushiriki katika shughuli zao, kufuata utaratibu uliowekwa.

Mwisho.

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, IKULU
 
Asante kwa taarifa..kuna baa yangu hapa sakina nataka aje aifungue..nitafuata utaratibu stahiki kumpa mwaliko aje kuifungua hasa ukitilia maanani ajira kama kumi nilizotoa
 
Tatizo liko wapi? Wengi wanao mualika ni watu wa hurka yake. Usitegemee mtu kama mimi nitakapofungua mradi wangu nitamualika. Ninaamini ita-impair reputation ya Biashara yangu. Simualiki hata Ikulu wakiniomba
 
Ni vizuri utaratibu ufatwe tu!maana itaonekana kuwa mkuru anatoa ahadi ya kufika sehemu na hafiki.Fanyeni kazi watu wa ikulu.Mtu akitangaza kabla ya kupata kibali akabwe.
 
Hilo ndio jambo la muhimu la kulitolea tamko katika kipindi hiki cha kila kitu kuwa kigumu nchi hii!!
 
Mbona huwa tunampigia simu jk na tunalonga naye na kututhibitishia kuhusu availability yake, tatizo ni nini silva? Barua zinapokuja kwako ni formalities tu, maelewano tayari tunakuwa tumeshayafikia na mkuu.
 
Hilo ndio jambo la muhimu la kulitolea tamko katika kipindi hiki cha kila kitu kuwa kigumu nchi hii!!

Yaani mkuu inauma sana
mambo mengi yapo tete na yanahitaji tamko na ufafanuzi..badala yake wanatuambia mambo ya minuso!
 
Asante kwa taarifa..kuna baa yangu hapa sakina nataka aje aifungue..nitafuata utaratibu stahiki kumpa mwaliko aje kuifungua hasa ukitilia maanani ajira kama kumi nilizotoa

Hujatulia hmethod, lakini huwezi jua bwana, labda angependa kuja
 
Huku Lengijabhe umasaini tumejenga choo cha kwanza cha kisasa, maombi ya ushiriki wa raisi yanakuja kwenye kuzindua choo hiki. Ni matumaini hatatuangusha, wahisani wetu wetu nao watakuwepo.
 
ndo hivyo serikali hii mnuso mbele maendeleo nyuma wana prefer magari ya millioni 90 kwa wabunge
Yaani mkuu inauma sana
mambo mengi yapo tete na yanahitaji tamko na ufafanuzi..badala yake wanatuambia mambo ya minuso!
 
hii ndio tuite nini sasa????akward,foolish,crap,nonsense,low burget,crackmind..or wht??
 
..mara picha ibadilishwe, ile ya zamani alikuwa amechoka na mikiki ya kampeni..mara maagizo kwenye vyombo vya habari awe 'addressed 'Dr."..mara sasa maagizo ya kutuma mialiko...masuala ya msingi?!..poor our country!....nakulilia Tanzania
 
Back
Top Bottom