Matumaini mapya yameanza kuchomoza - Zitto Kabwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matumaini mapya yameanza kuchomoza - Zitto Kabwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, May 24, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ZITTO KABWE:

  [​IMG]
  Matumaini mapya yameanza kuchomoza
  Zitto Kabwe

  Toleo la 240
  23 May 2012
  JUMATATU hii ya Mei 21, nimeanza ziara yangu ya mafunzo hapa Uholanzi pamoja na wabunge wenzangu pamoja na Katibu wa Kamati ya Bunge. Wabunge wenzangu Nasir wa Korogwe, Kafulila wa Kigoma Kusini na Sarah Msafiri kutoka Morogoro wameungana nami katika ziara hii.
  Malengo ya ziara yetu ya mafunzo ni kuhusu masuala ya mafuta na gesi. Wizara ya Mambo ya Nje ya Uholanzi kupitia ofisi ya Mambo ya Nje ya Tanzania wameongeza idadi ya wabunge katika ziara hii kutoka wabunge wawili walioonekana kudhamiria kujua sekta ya mafuta na gesi (ambao ni mimi na Januari Makamba). Lakini Januari ameteuliwa kuwa naibu waziri, hayupo kwenye ziara hii.
  Jopo letu hili limepata muhtasari kuhusu sekta ya mafuta na gesi hapa Uholanzi, tumeelezwa kwa jinsi gani leseni za uchimbaji mafuta zinatolewa na mapato yanavyokusanywa kwa uadilifu. Tumeelezwa kwamba Serikali ya Uholanzi hukusanya jumla ya Euro bilioni 11 (zaidi ya trilioni 22 za Tanzania, zaidi ya bajeti ya Tanzania ya trilioni 14) kama mapato kutokana na sekta hii ya mafuta na gesi.
  Wanakusanya takriban asilimia 85 ya mapato ya jumla kutoka katika mafuta na gesi, katika eneo la Groningen (ambalo ni kubwa zaidi barani Ulaya).
  Kutoka katika pato hilo, asilimia 45 ni kodi inayokusanywa kutoka katika kampuni za gesi na mafuta (kati ya kampuni kubwa zaidi ni Shell na ExxonMobil) na asilimia 40 kutoka katika ile ya asilimia 85 ni kodi na gawiwo kutoka katika kampuni ya Serikali ya gesi na mafuta ya EBN.
  Kutoka katika maeneo mengine ukiachilia mbali Groningen, Uholanzi hukusanya asilimia kati ya 40 na 65 ya mapato. Katika leseni zote isipokuwa zile za zamani tu, nchi hii imekuwa na hisa katika kampuni mbalimbali za mafuta na gesi.
  Hapa Uholanzi hakuna mikataba kama ile tuliyozoea Tanzania (yaani Production Sharing System - PSA) kwamba kampuni husika katika uwekezaji ndizo wakandarasi wakubwa. Faida kubwa ya mfumo wa PSA ni kwamba nchi inabaki kuendelea kuwa mmiliki wa rasilimali.
  Hata hivyo, katika mifumo hii iwe huu wa PSA wa Tanzania au huu wa hapa Uholanzi mambo muhimu zaidi ni uwazi na uwajibikaji katika sekta nzima.
  Tulikutana na Naibu Waziri Mkuu, MaximeVerhagen. Nimewasilisha salamu zetu za dhati kwake kwamba tungependa ushirikiano huu kati ya nchi zetu uendelee kudumu. Ni ushirikiano wenye tija kubwa sana kwa nchi hizi mbili.
  Nilimkumbusha kuhusu hazina yetu kubwa ya gesi iliyovumbuliwa ikiwa ni pamoja na uvumbuzi wa visima vitano vilivyoko chini ya kampuni za Kiingereza ya British Gas, kisima kimoja cha kampuni ya StatOil na visima vingine vidogo vya Songosongo, MnaziBay, Mkuranga na Nyuni, wilayani Kilwa.
  Nilimweleza Naibu Waziri Mkuu kuhusu dhamira yetu ya kuiona Tanzania kuwa moja ya nchi za Afrika ambayo utajiri wake unanufaisha wananchi wake. Nimemweleza katika utambulisho wangu kuwa; “ “Baadhi ya viongozi vijana Tanzania tumedhamiria kupandikiza matumaini mapya katikati ya dimbwi la msongo wa mawazo miongoni mwa vijana wenzetu.
  “Kwamba inawezekana kwa nchi za Afrika kuwa tajiri kutokana na gesi na mafuta, sambamba na kuwapo kwa ustawi bora wa utawala na demokrasia. Hiyo inawezekana kwa kutumia vizuri rasilimali za nchi.
  “Kwamba hatutaki kurudia makosa yaw engine (kama nchi za Nigeria inayopoteza mabilioni ya fedha katika uvunaji mafuta) na hata makosa yetu wenyewe katika sekta ya madini. Na kama makosa yakifanyika, basi yawe makosa mapya si kurudia ya zamani.”
  Waziri Mkuu alituahidi kuwa tayari kusaidia maendeleo ya sekta ndogo ya gesi nchini Tanzania na hasa kwa upande wa maendeleo ya rasilimali watu. Ajenda hiyo ilijadiliwa zaidi katika Wizara ya Mambo ya Nje na ikakubaliwa kuwapo kwa ufadhili kwa wanafunzi kutoka Tanzania kwa ajili ya kusomea masuala ya mafuta na gesi ili nchi iweze kuwa na watalaamu wa kutosha katika sekta hiyo.
  Alipendekeza kwamba Tanzania itumie mapato ya gesi kutengeneza miundombinu, sambamba na deni la taifa kwa maslahi ya vizazi vijavyo. Alielezea nia ya Uholanzi kuwa kitovu cha uzalishaji gesi barani Ulaya.
  Ziara yetu inaendelea kwa mujibu wa ratiba. Tumedhamiria kujifunza na kile tulichojifunza na tutakachojifunza tutakipenyeza katika sera yetu mpya ya gesi nchini na katika mpango mkuu kuhusu gesi (Gas Master Plan).
  Nina matumaini makubwa tutafanikiwa kama taifa licha ya msongo mkubwa wa mawazo unaowazonga wananchi wetu. Lazima tujenge nchi tunayoitaka.
   
 2. Chali wa Moshi

  Chali wa Moshi JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 258
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ni bwana nyepesi wewe au?
   
 3. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Na hii asilimia 4% ya kwetu wanasemaje?
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  [FONT=&quot]Netherlands[/FONT]
  [FONT=&quot]revenues: $392.1 billion[/FONT]
  [FONT=&quot]expenditures: $424.8 billion (2011 est.)[/FONT]
  85% yake ni kama $ 333.2 billion while sisi kwenye madini tunaambulia 4%
  Ivi Tz kama serikali haiwezi ata kureserve baadhi ya maeneo ili tuyafanyie utafiti sisi kama sisi na tuje kuvuna iyo gas kama Tz kwa kutumia ela ambayo tutaipata toka kwa makampuni ambayo yataanza kuvuna gas.
  Maana kwa sasa wako bize na ugawaji wa ivyo vitalu vya kutafit as if iyo gas uko chini inaisha!
   
 5. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Tatizo watanzania hatuheshimu profession za watu, wanasiasa ndio kila kitu. bahati mbaya wengi ni corrupt.
   
 6. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  badala ya serikali kutuma wahandisi na watafiti waliobobea kwenye fani hiyo ya nishati wanatuma wabunge/wanasiasa? so wanasiasa watakuja kuwafundisha wahandisi namna ya kutafuta gesi na mafuta au itakuwaje?? wastage of of public funds!!
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kuna mzee yuko ngambo kumbe walipelekwa na Nyerere enzi izo kusoma aliporudi akakuta mwalimu amefariki watawala wapya hawana mpango na taaluma yake ya madini akasepa kwa sasa ana PHD na yuko Sweden anafanya kazi.
  Ingawa mpaka leo dhamira yake inamsuta kurudi kuja tumiakia taifa ambalo lilitoa ela kumsomesha ila watawala hawalioni ilo
   
 8. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Huyo Metallurgist alikuja enzi za Mkapa lakini jamaa akamponda na hata ushauri wake ukatupwa jalalani,lakini Sweden wanamtumia at full capacity.
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kumbuka kwenye madini tunaambulia 4% kabla ya makampuni kuingiza faida na baada ya makampuni kuingiza faida tutapata hiyo 4% jumlisha na kodi ya corporate tax ambayo ni 30% na kama tuna shares zozote, nadhani kwa Tanzania tuna asilimia isiyopunguwa 15 kwenye migodi, kwa hiyo ni hivi karibuni baada ya wawekezaji kurudisha mitaji yao tutaanza kuona Tanzania ikiingiza 30% + 4% +15% = 49% kwa uchache. Indirect taxation itaingiza zingine kama 10% inakuwa 59% jumla.

  Siyo mbaya kwa nchi isiyokuwa na teknolojia yoyote. Kinachotakiwa ni kuhakikisha tu kuwa hao wawekezaji hawaibi kwenye mahesabu na kusema kuwa hawajarudisha mtaji, fikiri akiwa mchaga ndio inspector panakuwaje?

  Kuna mgodi ambao mwaka huu umeshaanza kulipa namna hiyo.
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Tatizo liko kwenye statements za izi kampuni ili kuweza kukokotoa kod stahiki!
  Wanakuwa na statements mbili tofauti ie moja for their bosses na ingine kwa watawala wetu.
  Kuna siku Lembeli aliidaka iyo genuine report akaileta bungeni Ngeleja akasema ataifanyia kazi jiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Zitto anaweza kuwa na nia nzuri, lakini ningependa kujua hii mission ni kwa niaba ya Bunge, au serikali, au CHADEMA, au kikundi gani? Nani alitoa mwaliko? au nani alituma maombi ya hii ziara?

  Pili, Kwenye hiyo team kuna wataalam wowote wa mambo ya 'extractive industry mfano wahandishi wa madini, au oil? Kafulila aliongezwa kwenye huo msafara kwa ujuzi gani kwenye mambo ya gas au oil? Au huyo mbunge mwingine wa Morogoro naye ana utaalam gani?

  Tatu, kwa upande wa CHADEMA ningependa kuamini kuwa waziri kivuli wa nishati na madini, ndugu Mnyika hakuweza kuungana na huu ujumbe wa Zitto kwa sababu ya kesi. Ningependa kuamini hivyo.

  Hata hivyo kabla hajaenda kujifunza mambo ya mafuta huko Uholanzi wangeenda Nigeria wakutane na watu wa Ogoni Land. Wataona unyama wa Shell.
   
 12. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,734
  Likes Received: 1,445
  Trophy Points: 280
  Serious? Kama alisoma muda wote Nyerere ameng'atuka hadi kufariki huyu hakuwa na nia ya kurdui, maana ni interval ya miaka 15!

  Kama ana nia basi sababu za kuja zipo, sijui uwezo wake maana umesema "mzee"
   
 13. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kula tano Zitto! I wish na wabunge wengine wangekuwa wanaenda huko nje kujifunza kama wewe sio kung'aa ng'aa macho
   
 14. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Shell hawana unyama wowote, unyama ni wa serikali ya Nigeria!
   
 15. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,419
  Likes Received: 258
  Trophy Points: 180
  Afrika na haswa tz tuna maliasili tosha achana na tunazovumbua za kuweza kututoa kwenye msongo wa mawazo anaousema zitto,hata tuvumbue cash money aridhini bado viongozi watatupiga sound ,kila anayepata madaraka anawaza yake na vizazi na ukoo wake.wamelimbikiza pesa hadi ulaya.
   
 16. F

  FJM JF-Expert Member

  #16
  May 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Ni sawa na kusema Barrick are clean, matatizo yote ni serikali ya Tanzania! Kumbuka, it takes two to tangle. Kama sio kelele za wanaharakati, shell waengelea kuziba pamba masikioni. Serikali za kiafrika zina matatizo, lakini mambo yanakuwa even worse wanapotokeza wawekezaji 'wajanja'.
   
 17. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Labda alihatarisha ulaji wa wazee. Maana hawa jamaa wanatuuza kwa bei rahisi mno kwa ulaji wao. Very uncivilized human. Selling your own people? Unajua maana ya kuiba mlima wa makaa ya mawe. Nchi nyingine shaba hadharani. Aibu kabisa kabisa.
   
 18. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nani? Ngelejaaa? Duhhh. Zittoa anamfahamu huyu jamaa vizuri.
   
 19. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #19
  May 24, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,419
  Likes Received: 258
  Trophy Points: 180
  Zitto nimewahi kumsikia clouds akielezea jinsi mlima wa makaa ya mawe ulivyouzwa kule kiwira na hii issue sijawahi kuisikia tena!
   
 20. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #20
  May 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  TAtaizo ni chama na serikali
   
Loading...