Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,745
CCM waliingia na gear ya usafi wakashindwa kuzoa mataka ,muda si mrefu vunjavunja nayo imefifia,mara wakabadilisha upepo viroba na madawa ,ikawa nchi imeingia kwenye kamata kamata aliekuwemo na asiekuwemo twende mbutolwe mwanawa umma utajibia polisi,wakashindwa njiani wakabadilisha tanga kazi akapewa mhusika baada ya alieshika sukani kuboronga ,kukazuka balaa la kutekwa watu,bastola njenje, ishu ikastukiziwa wahusika kuadhirika mchana kweupe,ukurasa ukadumaa,sasa kuna vyeti feki napo hapo ,wanyonge ndio wanaokandamizwa kwani kama huna atakae kushika mkono unaenda namaji.
Sasa kunatambaliwa kwenye nyumba za ibada kwa kuegemea huko mashehe na maaskofu wanakaangwa kwa mafuta yao bila kujua kinachotafutwa,hata mimi sikijui ila naliona hili nalo ni la ajabu haijapatapo kutokea tuombe liwe na mwisho mwema kwani kila utawala huu wa CCM unapojichomeka basi kila kitu huwaendea kombo ,najisemea labda Bwana Mungu hayupo pamoja nao na huwakataa kila wanapomsogelea,Maana Bwana Mungu hawakubali wanaodhulumu ,atawatenga tu labda watubie.
Anagalia Uchaguzi wa Zanzibar ,hakuna asiejua kuwa waZanzibari walibadilisha sogi,ila Uongozi wa Muungano umefumbia macho ,sasa unapomwambia Bwana Mungu kuwa wewe ni mtenda haki na una huruma,huonei huwa unamuweka Bwana Mungu kwenye fungu gani ? Hivi unategemea akuwezeshe kuwa upande wake ,Unategemea Bwana Mungu akuunge mkono,akusaidie hata kama mashehe na mapdre watakuombea basi hizo dua zitageuka kuwa laana kwa hao waombaji na wale wanaoombewa.
Ujinga wa Lipumba napo hapa panahitajika urahisi gani wa kutenda wema,Lipumba mbali ya kulipa jeshi la polisi taswira mbaya pia linaichafua serikali vibaya sana,yapo mambo serikali inaweza kuyafanya lakini kwahili la Lipumba naona anaivua nguo serikali,fedheha yajuzi ni baraka kutoka kwa bwana Mungu yule mnaemuomba nyinyi ndie huyo huyo anaewauliza na hili linawashinda na kuwapa tabu ?Yaani mngejisafisha kirahisi na kuachana nae.
Kama haitoshi ajabu ya kufungwa kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa,na hapa Bwana Mungu amezidi kuwadhalilisha kwani social media zimepata nguvu zaidi na habari zinaenea kwa sekunde tu,angalia bungelive mmezuia lakini kikianguka kitu bungeni tayari wabunge hawajatoka bungeni walioko china wameshapata habari,ni yuleyule Bwana Mungu mnaetafuta nae ushirika anawaumbua,ni bora mkafungulia mikutano na Wazanzibari wapewe punda wao mwengine
Hayo maendeleo yanayotafutwa kwa mwendo huu yatabakia ni yenye kuandikwa na kusifiwa lakini hayana uhalisia ukiziba ya treni yanatoboka ya ndege ukikarabati ya ndege kuna bomba lagesi nalo linavuja ,ukiziba bomba bandarini kunageuka pwani ,dua zitaombwa lakini jirekebisheni kwa uchafu huu wa akina lipumba na jecha Muone kama dua hazitoitikiwa,achieni mikutano namjenge uwanja wa demokrasia mwenye lake aende uwanjani aseme mpaka achoke,uwone namna Bwana Mungu atakavyowafungulia neema kwenye serikali yenu na kwenye malengo yenu ,lakini hiizi sera za kukamatana na kukamatiana bakora mwicho wake mtachapana wenyewe kwani ,Kwa Bwana Mungu hilo sio kubwa ndio kama tuonavyo namba inavyosomwa .Anaewambieni huwa anawapenda na msema kweli ni kweli mpenzi wa Bwana Mungu ,nae ataonyesha mapenzi yake kwenu,ila ka,a maneno hayaendani na vitendo basi Bwana Mungu nae atawafelisha maana hamsemi na hamuutaki ukweli,
Idumu Tz yenye Amani na upendo wa kweli kati ya Viongozi na wanaoongozwa.