matrekta kubeba makontena ni sawa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

matrekta kubeba makontena ni sawa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by General mex, Mar 12, 2012.

 1. General mex

  General mex Senior Member

  #1
  Mar 12, 2012
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  wanajamii forum leo wakati nakatiza maeneo ya ubungo, ghafla zikapita trekta mbili zikitokea morogoro road zikaelekea mandela road, zilikua zimebeba yale makontena marefu kabisa. Swali ni kwamba ni kwa nini mpaka trekta zitumike kubeba kontena??? Dereva wa trekta mahali alipo ni mbele kabisa ya kontena na katikati ambapo hawezxi kuona nyuma atokapo au hata pembeni! magurudumu yanayotumika yameisha mbaya kabisa mpaka nyaya zinaonekana, na nyuma sio double tyre ni gurudumu moja kila upande jambo ambalo ni hatari sana. Na hao traffic wanafanya kazi gani wanashindwa hata kutoa ushauri kwa hao wanaosafirisha kontena kwa matrekta! au ndo mpaka yaangukie watu ndio ionekane kwamba ni hatari? kwa nini watanzania hatuwezi kuchukua tahadhari kabla ya hatari? trekta ni kwa ajili ya kilimo, sasa huku mjini yanafanya nini? hata kama ni kubeba mzigo hua lina bodi ndogo na sio kontena! Ushauri wangu ni kwamba, traffic wasikubaliane na upuuzi huo kabisa wazuie hayo matrekta yakalime. hata kesho keshokutwa mtu apoteze maisha kwa kuangukiwa na kontena lililokua kwenye trekta! si kituko hicho? Au yanamilikiwa na wana magamba! maana traffic aliyapisha kama anaona scania tuu!
   
Loading...