Matrafiki Wa Dar Hizi SIFA Zenu Mpaka Lini? Nimekosa POSHO Ya Maana Kwa Upuuzi Wenu Huu....!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,689
109,114
Siku Zote Nilikuwa Nikidhani Kuwa Hizi Foleni Nyigi Za Hapa Dar Zinatokana Na Msongamano Wa Kweli Wa Magari Badala Yake Leo Mwenyewe Nimethibitisha Kuwa Kumbe Foleni Nyingi Za Jijini Dar es Salaam Hutokana Na Msongamano Wa Uwezo Duni Wa Kufikiri Wa Askari Barabarani Wetu a.k.a Matrafiki.

ILIKUWAJE?

Nilikuwa Nipo Makumbusho Muda Kama Wa Saa 1 Iliyopita Nakunywa Juice Huku Nikikandamiza Na Egg Chop Zangu Kadhaa Na Pembeni Yangu Alikuwa Ameingia Askari Trafiki Mmoja Ambae Kimuonekano Tu Alionekana Kama Vile Leo Hajakamata Gari Na Muda Wote Uso Wake Ulikuwa Umejawa Na Hasira.

Alipokaa Tu Maongezi Yetu Yalikuwa Hivi:

Trafiki: Ebhana Mambo Vipi.
Gentamycine: Poa Tu.

Trafiki: Ebhana Unaweza Ukanisaidia Kuniongezea Tsh Mia Tano Ninywe Soda Ya Take Away?
Gentamycine: Kamwombe IGP Mangu.

Trafiki: Unasemaje?
Gentamycine: Hukusikia au?

Trafiki: Kijana Unaonekana Una Dharau Sana!
Gentamycine: Ipakae Rangi Kabisa.

Trafiki: Sasa Ngoja Nikuonyeshe Kwamba Mimi Ni Trafiki Na Njia Hii Yote Ni Yangu.
Gentamycine: Poa Tu.

Trafiki: Na Leo Utafika Kwako Usiku Kwani Nitavizia Gari Unalopanda Ujute Kunijua.
Gentamycine: Afande Yote Haya Kwakuwa Nimekunyima Jero au Kulikuwa Na Lingine?

Trafiki: Utakapofika Kwako Usiku Wa Manane Leo Ndiyo Utajua Kuna Lingine au Hapana.
Gentamycine: Anyway Yaishe Afande Naomba Radhi.

Trafiki: Kamwombe Shangazi Yako Hapa Kazi Tu.
Gentamycine: Akghaaaaaaaa Usinitishe Bhana Kwenda Zako Huo Wewe POPOMA Nini? Tena Usinizingue!

Nikaamka Pale Ktk Ule Mghahawa Na Kwenda Kupanda Gari Za Kwenda Buguruni. Kumbe Wakati Natoka Pale Huyu Trafiki Na Yeye Akatoka Pale Na Kwenda Kujibanza Mahala Kuangalia Napanda Gari La Wapi Na Alipoona Tu Nimepanda Gari Za Kwenda Buguruni Alipanda Pikipiki Haraka Haraka Na Kwenda Kunitegea Mingo Pale Karibu Kabisa Na Hospitali Ya Mwananyamala Na Hamuwezi Amini AMETUKALISHA PALE KWA MAKUSUDI ZAIDI YA SAA 3 Gari Haziendi Buguruni Huku Muda Mwingi Alipokuwa Anayaongoza Magari Ya Kuja MAKUMBUSHO Alikuwa Muda Wote Macho Yake Anaangalia Ktk Ile Gari Kama Nashuka au Bado Nimekomaa Na Kuna Wakati Nilishuka Na Kukodi Pikipiki Ili Nipite Na Nilipofika Pale Alipo Yeye Dereva Alisimamishwa. Nilipogundua Kuwa Huyu Trafiki Ana Lake Jambo Na Mimi Nikamuuliza Tena Na Maongezi Yalikuwa Hivi:

Gentamycine: Afande Mbona Hivi?
Trafiki: Kashtaki Kwa Magufuli au Lowassa.

Gentamycine: Wao Ndiyo Mabosi Zako au?
Trafiki: Unauliza Mgonjwa KIBASILA au MWAISELA?

Gentamycine: Kwahiyo Tutaendelea Kukaa Ktk Foleni Mpaka Saa Ngapi Afande?
Trafiki: Paa Angani.

Gentamycine: Kwahiyo Yote Haya Ni Kwasababu Tu Ya Ile Tsh Mia Tano?
Trafiki: Kwani Ndogo?

Nilipogundua Tu Kuwa ALIAMUA Tu Kunikomoa Na Kunipotezea Muda Wangu Vile Nikaamua Tu Kurudi Zangu Kwangu Na Alipoona Tu Nimepanda Gari Za Kuja Huku Makumbusho Na Yeye Akayaruhusu Magari Yaende. Kanisababishia Usumbufu Mkubwa Mno Na Hasara Kubwa Sana Kwani Nimekosa KIKAO Cha Kikazi Ambacho Kilikuwa Na Posho Nzuri Tu.

Kamanda Mpinga Hivi Hawa Askari Wako Wa USALAMA BARABARANI Huwa Mnawafundisha Na UJEURI, VISASI Na NYODO au? Hivi Huyu Askari Wako NINGEMTANDIKA MAKONDE Mngenilaumu? Hayo Majibu Aliyokuwa Akinitolea Ndiyo Mnawafundisha Pia Huko Vyuoni? Sasa Nimegundua Kuwa Kumbe Foleni Nyingi Za Jijini Dar Zinasababishwa Na VISASI Na CHUKI Tu Za Matrafiki Wako. Na Bahati Nzuri Nimeshamkariri Na Najua Ipo Siku Atajaa Tu Ktk FRAME. Sasa Kama Alikuwa Na Kisasi Na Mimi Kwa Kumnyima Hiyo Tsh Mia Tano ( 500/= ) Kwanini Awatese Na Watumiaji Barabara Wengine? Ni Mnene Mnene Hivi Maji Ya Kunde Na Hupenda Sana Kujificha Na Mtumbo Wake Mkubwa Utadhani Pipa La SIMTANK Pale Sayansi Ktk Yale MABOZA ( Magari ) Ya Kubeba Maji. Silaumu Kunikalisha Saa Zile Tatu Ktk Foleni Bali Nawazia Tu Mpunga Nilioukosa Leo. Anyway Leo Kashinda Na Matrafiki Wote Wa Sayansi, Makumbusho Na Mwananyamala SHIKAMOONI.

Nimeumia Sana Tu Leo.
 
Huyo askari alitakiwa akupe vibao kabisa kwa majibu uliyompa alichokosea ni kuadhibu hata wengine wasiohusika. Ila siamini ulichoandika hapa kama kina ukweli. Kwanini usimjibu tu kua huna miatano? Mambo ya IGP yanaingiaje hapo? Mi ningekua askari ungejuta kuzaliwa. Ilitakiwa iwe ni kipigo tu hamna namna nyingine tena!
 
Huyu genti ni Eddo Kumwembe.

Mtahangaika Sana Kutaka Kunijua. Wengine Mnanifananisha Na Nape Nnauye Leo Tena Edo Kumwembe Na Ipo Siku Mtanifananisha Na Rais Ajae Dr. John Joseph Pombe Magufuli. Niahidi KIPIRA PORI Chako Nitajitokeza Unijue Sawa?
 
Back
Top Bottom