Viol
JF-Expert Member
- Dec 15, 2009
- 25,419
- 18,341
Nilipokuwa shule ya msingi kuanzia la 4 hadi la 7 maksi zangu za hesabu kwenye mitihani zilikuwa zinacheza kwenye 03% hadi 08%.
Matokeo yalikuwa yanatangazwa mbele ya darasa!yanapotangazwa mwalimu anaanza kuwaita wanafunzi kwakuanzia maksi za chini kwenda juu (0-100),kwahiyo darasa lote linajua makaratasi yakiletwa lazima niitwe kama si wa kwanza basi wa pili.
Siku moja mwalimu akaanza kuita majina,mpaka akafikia kwenye maksi 30%,40%,50%,60%,70% bado tu mi hajaniita.
Watu wakaanza kuniangalia waliokuwa karibu wakaanza kuniuliza....""eeeh umepasua hujaitwa,ilikwaje??"
Nilianza kuvimba kichwa,huku mwalimu anaendelea kugawa tu makaratasi.
Yakabaki makaratasi ya waliopata 80%-90% bado mi sijaitwa tu.
Mara akabaki na karatasi moja mkononi,darasa lote macho kwangu hawaamini kinachotokea maana bado sijapata karatasi.
Mwishoni mwalimu akaangalia juu,kisha akasema "kuna ng'omba hajaandika jina kapata 0% aje achukue karatasi yake"
Nilienda kuchukua nikiwa mpole.