Enzi za shule ya msingi

kalipeni

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
1,533
1,242
Maisja ya shule bwana we acha tu!

Nilipokuwa shule ya Msingi enzi hizoo kuanzia Darasa la Nne hadi la Saba maksi zangu za somo la Hisabati (Hesabu) zilikuwa zinacheza kwenye 03% - 08% na kwa bahati mbaya matokeo yalikuwa yanatangazwa mbele ya Darasa.

Yanapotangazwa mwalimu anaanza kuwaita Wanafunzi kuanzia maksi ndogo kwenda kubwa kwahiyo darasa lote lilikuwa linajua Karatasi zikiletwa lazima niitwe Mwanzoni kama si wa kwanza Basi wapili toka chini.

Siku moja mwalimu akaanza kuita majina mpaka akafika maksi 50%,60%,70% Bado tu hajaniita,basi watu wakaanza kuniangalia na kuniambia 'Ee umepasua leo' Basi mimi nilianza kuvimba kichwa huku mwalimu anaendelea kugawa tu karatasi kwa wahusika.

Hatimaye yakabaki makaratasi machache 80%, 90% bado mimi sijapata tu. Mara akabaki na Moja mkononi. Hahaha! Yaani Darasa lote macho kwangu hawaamini maana bado mimi tu ndo sijapata.

Mwishoni mwalimu akaangalia juu kama Muda wa Sekunde 30 kisha akashusha Pumzi kwa nguvu akasema "Kuna NGUCHIRO mmoja hajaandika jina lake kwenye karatasi kapata 00% Aje achukue Karatasi yake".
🤣🤣🤣
 
Umenikumbusha enzi ya shule ya msingi kuna Mwalimu wetu wa hisabati akigawa mtihani kwa waliopata ziro anaanza kwa kesema "Hawa ninaowaita hapa wamepata yai viza"
 
kalipeni,
Hahahaaa 😂 😂 😂 Kuna rafiki angu alipokea mtihani wa Jografi tukiwa form 2.. Sasa mwalimu akatangaza kua yy ndio kapata 100.. jamaa kwa wenge alikua hajui kama anaweza pata maksi hizo akamridishia mwalimu mtihani yaani aliona kapata ziro afu mwalimu kasema yy ndio kapata mia (ticha alikua anakuja kalewa)

Jamaa akamwambia mwalimu hapa umenikosesha bana mwalimu kucheki hv akagundua aliyetangazwa wa kwanza ndio kapata ziro
 
Nimemkumbuka mwalimu wangu wa chekechea.

siku iyo kaingia darasani anafundisha

kwakua alikua mkali Sana wanafunzi walikua kimya wanamsikiliza, bahati mbaya akajamba wanafunzi wakacheka sanaaaa,


kwa aibu na hasira akatoka darasani wiki nzima hakuingia class

wiki iliofuata akajua watoto watakua washasahau kabla hajaanza kufundisha akauliza

MWALIMU: darasa tuliishia wapi SoMo lililopita

wanafunzi wote kwa pamoja wakajibu "palepale ulipojambaaaaa".

😂😂😂😂😂😂😂
 
Naomba kuuliza wananzengo:
Panya BUKU
Kaunta BUKU
Fesi BUKU

Hawa jamaa Wana undugu????
 
Back
Top Bottom