Matokeo ya Uchaguzi Mdogo wa Jan 2017: Mbowe must go

Matokeo ya Uchaguzi Mdogo wa Jan 2017: Mbowe must go

MBOWE amefanya kazi kubwa sana chadema...lakini alipofika sasa ameshachoka..akae pembeni kama mshauri

Hana jipya tena anaweza ku offer
Propesa Libumba ndie anahitaji maelekezo yenu. Ruzuku mliyomchotea haikutosha.
 
Hii hoja ni ya kitoto, wengi wenu mnaamini Lowasa alishinda kwa hilo swali lako ina maana rais wa hii nchi kabla ya uchaguzi alikua wa chama gani na hapo unataka kuitoa hoja ya ushindi wa Seif ama Lowasa. Msipende sana mpaka mkapoteza akili zetu kwa kuichukia CCM jaribuni kuwa wakweli katika kukifufua chama ukweli ni kwamba hii CHADEMA siyo ile ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2010. CHADEMA kimekua kama mwana aliyefiwa na wazazi wake ama ametelekezwa na wazazi wake. Wazazi wanashinda kwenye mataputapu watoto hawajui nini watakula hii ndiyo CHADEMA ya sasa. Tutawakumbuka sana kina Zitto kabwe na Mzee Slaa.
Wachukueni wakamshauri one man show.
 
Buriana wewe, Mti wenye matunda ndio unaorushiwa mawe , hatushangai na siasa zenu za majitaka, zenye maudhui ya kinyumenyume na maumbile,
Mbona kuna TLP, act waz, tppp, cuf nk huongelei viongozi wake na LiCCM lenye miaka ya mbwa halijeleta mapinduzi yoyote ya kiuchumi, nenda zako tuachie kamanda wetu
Punguza povu
 
Mjinga pekee ni yule anayeamini cdm haiaminiwi na watanzania wakati anajua wapinzan wamezuiliwa kufanya siasa. Kama ccm inapendwa na watz basi waache cdm na vyama vngne vifanye siasa kwa uhuru ndio tutajua chama kipi hakipendwi.
Wananchi hawalagi maneno
 
Kwa ulivyoandika ww utakuwa ni kile chama cha mboga mboga, nadhani ushauri kama huu ungepeleka kule ungewafaa zaidi.
 
Haujanishawishi hata kidogo. Hauwezi ukaangusha lawama zooote hizo juu ya mtu mmoja bila hata kuangalia mazingira ya kisiasa kwa sasa. Mimi nilitarajia Mbowe apongezwe kwa kuendelea kuwa imara katika mazingira magumu kabisa ya siasa za upinzani kwa sasa hapa nchini. Badala yake wanaibuka waimba chorus Mbowe, Mbowe kama vijana wa ACT na Lumumba. Acha mkumbo kijana. Unaendelea kutumia hoja mfu za waraka wa MMI na MM2 uliotaka kumpindua Mbowe. Mbona waliousimamia hawajaweza kupeleka chama chao to the next level kama walivyo kuwa wakidai? Kama na wewe ni mmoja wao pole sana.
sawa mkuu inabidi nikusikilize na tuendelee kujipa moyo maana hata Fisi anajipa moyo kwamba kuna siku mkno wa binadamu utaanguka na kuwa kitoweo chake. Lakini usisahau kuwa chama kimeingiliwa na watu wabaya zaidi kuliko kina Zitto. CHADEMA hapa ilipo sitashangaa ikiishia kuwa kama NCCR - Mageuzi ya Marando na Lamwai ya mwaka 1995 na Mrema. Hizi jitihada za kubeba makapi kutoka kwa chama cha majambazi hatutafika kokote usije shangaa kina Sumaye wakakiharibu CHADEMA wakahamia ACT kama Mrema alipowaacha NCCR na kuingia TLP. tunza hizi comments tuonane mwaka 2020, lakini tusije tukageukana na kuitana wasaliti ama tumenunuliwa na CCM ama kura zimeibiwa. Me say.........
 
sawa mkuu inabidi nikusikilize na tuendelee kujipa moyo maana hata Fisi anajipa moyo kwamba kuna siku mkno wa binadamu utaanguka na kuwa kitoweo chake. Lakini usisahau kuwa chama kimeingiliwa na watu wabaya zaidi kuliko kina Zitto. CHADEMA hapa ilipo sitashangaa ikiishia kuwa kama NCCR - Mageuzi ya Marando na Lamwai ya mwaka 1995 na Mrema. Hizi jitihada za kubeba makapi kutoka kwa chama cha majambazi hatutafika kokote usije shangaa kina Sumaye wakakiharibu CHADEMA wakahamia ACT kama Mrema alipowaacha NCCR na kuingia TLP. tunza hizi comments tuonane mwaka 2020, lakini tusije tukageukana na kuitana wasaliti ama tumenunuliwa na CCM ama kura zimeibiwa. Me say.........
Hapa nimekuelewa. Una nia ya dhati ya kujenga chama.
 
wewe upo upande gani, kilicho ongelewa siyo sahihi??

Wacha Wadanganyika waendelee kuisoma namba, dhiki ni mapenzi yao wenyewe. Mimi ndg yangu anapo lalamika nampa makavu tu.
Hakuna MTU mpumbavu atakayewapa dola kama Wagombea ni hawa waliofukuzwa CCM ndio mnaokoteza! Shame!
 
Ni dhahiri sasa Mheshimiwa Mbowe hana mbinu mpya, kila anachokifanya katika chama ameprove failure. Hana Input yoyote yoyote ya kukikwamua chama kutoka chama cha kushindana na kuwa chama cha kushinda!.

1. Tamaa yake ya harakaharaka, ilipelekea kufanya maamuzi yaliyokiondolea chama falsafa ya kupambana na ufisadi.
2. Kuingilia kwake mchakato wa uchaguzi ndani ya chama, kwa mfano kumkata ndugu Sosopi kumekiondolea chama ajenda ya kupigania demokrasia nje ya chama na ndani ya chama
3.Kushindwa kwake kuisimamia operesheni UKUTA, kumekifanya chama kisinyae, kiwe kama mdondo wa kuku asiyeweza kujitetea, huku akitoa nafasi bwerere kwa CCM kujinadi peke yake nchi nzima

Athari za maamuzi haya ni
1. Wananchi kupoteza imani na Chama, na badala yake kuona social media ndo kimbilio lao

Matokeo mabaya kabisa ya chama katika uchguzi huu mdogo, ni meseji kwa Mheshimiwa Mbowe, kwamba Chama kinahitaji new Leadership, ni dhahiri hana mbinu za kukitoa chama hapa kilipo na kukipeleka hatua inayofuata. Ni bora akawa Muungwana kama Mwalimu Nyerere, aliyeona kuwa nchi imekuwa ngumu kwake akajiweka pembeni!
si ndo ufurahi kwa kuwa chama chenu ccm kimeshinda.
 
Mjinga pekee ni yule anayeamini cdm haiaminiwi na watanzania wakati anajua wapinzan wamezuiliwa kufanya siasa. Kama ccm inapendwa na watz basi waache cdm na vyama vngne vifanye siasa kwa uhuru ndio tutajua chama kipi hakipendwi.
Unataka kusema kwenye hizi chaguzi ndogo wapinzani hawakupewa nafasi ya kupiga kampeni?
 
Hapa nimekuelewa. Una nia ya dhati ya kujenga chama.
Mkuu nia siyo kujenga Chama tu ni kuijenga nchi yetu pia. Lakini hatutaweza kufikia pale tunapotaka kufika kwa kuwategemea viongozi hawa tulio nao, Mimi nilishachoka na hiyo CCM tangu mwaka 1992 tulipoanzisha vyama vingi lakini nilikata tamaa siku nyingi na upinzani, ila kama nilivyosema huko nyuma mwaka 2010 baada ya uchaguzi nilipata imani kama baada ya miaka 10 yaani mwaka 2020 hii nchi ingepata uhuru kamili. Kwa maana mwaka 2015 upinzani ungeshika bunge na hivyo kuilazimisha serikali kuleta katiba ya Warioba. Cha ajabu tukaletewa watu wale wale waliotufikisha hapa tulipo ati wawe kama Musa na wana wa Israeli. Japo namalaumu sana Slaa kwa kuiacha meri katika misukosuko lakini nilimuelewa kabisa kwanini alifanya hivyo. Na katika Nchi za wenzetu watu wanahama vyama lakini hawaitwi wasaliti. Lakini hapa kwetu Tanzania ni jambo la kawaida kwa vyama vyote halafu utasikia watu wanaongelea demokrasia. Moja ya maana ya demokrasia ni uhuru wa kuhamia chama chochote ama kufanya jambo loloye bila kuvunja sharia. Lowasa kahama CCM aliitumikia miaka kama 30 masaa machache alianz\a kutukanwa mpaka na mwenyekiti wake. Zitto kafukuzwa uanachama japo hakusema kitu chochote kibaya alianza kuandamwa na yeyote aliyemtetea akaitwa ni msaliti. Mimi sipo katika huko, maana nimeona wanasiasa katika nchi zingine nilizoishi wanaaccha chama kimoja na kujiuzuru ubunge na kujiunga na chama kingine katika uchaguzi mdogo na wanachukua jimbo bila kutukanwa wala nini ni sera tu na sababu za kuhama chama anazianika hadharani. mwanasiasa George Galloway alifukuzwa Labour Party lakini bado hasemi mabaya kuhusu Labour. Robert Jackson aliacha Conservative akajiunga na Labour Party April 2005 sababu hakukubaliana na chama chake kuhusu Education Funding, Quentin Davies alihama kutoka Conservative kwenda Labour sababu hakukubaliana na uongozi wa David Cameron lakini hakuna hata siku moja utaona wanazomewa ama kutukanwa. Tutakapofikia hapo ndipo tutaweza kufika kule tunakotaka kwenda. Si lazima tuwaige ccm kama wanafanya ujinga na sisi wengine tufanye hivyo.
 
mbowe kama Arsen wenger wa Asernal ulipo tupo hata tukishwa kwa asilimia tano no sweat
 
Nimeuliza tu "Lini mwisho wa Mbowe kuongoza CHADEMA?"

Hii ina maana nyingi sana ila inaonyesha kukataa tamaa kwa mwanachama kindakindaki anayependa kusimamia ukweli.

Naona mambo yanaenda mrama na amepoteza dira na uelekeo. Anatupeleka msituni gari linakatisha mistuni karibu tunagonga mwamba.

Lini mwisho wa Mbowe kuongoza CHADEMA?
Lini mwisho wa Mbowe kuongoza CHADEMA?
 
Teh teh teh

Naona vijana wa Lumumba mmepata ajenda sasa ya kuzungumza mitandaoni baada ya kupotezwa kisiasa hivi karibuni...

Hongereni kwani ndani ya week hii mtapotea tena.
 
Huyu ni chief wa Ufipa sijawai kusikia chief amestaafu au ameachia madaraka zaidi ya kupinduliwa au kufariki
 
Back
Top Bottom