Nilikuuliza maswali unayokwepa.
Waliofanya mtihani ni 14,000+ na marks zinazoshindaniwa ni 100%. Tengeneza scenario ambayo kila mtu atapata marks za kwake peke yake. Unaweza?
Au kama vipi nakuuliza tena, je unataka wenye zero wawe 140, wenye 1 wawe 140, wenye 2 wawe 140 hivyo hivyo mpaka wenye 100 wawe 140?
Matokeo yako ya Form Four na Form 6 yalikuwaje, mlikuwa na idadi sawa kila Division? Uliwahi lalamika kwanini Div.1 ni chache ila Div. 4 ni nyingi?
Yes we think differently, nipo hapa nasubiria hiyo statistical scenario yako ambapo watu 14,000 watatofautiana marks ambazo ni 0% to 100% na pia wawe sawa kila group, wenye 10s wawe sawa na wenye 20s, 30s, .... 90s.
Mtihani umefanyia wapi, nimefanya APC na nimeshuhudia watu wametoka Nairobi kikazi, watu wamejifungua hata hawajaweza kutembea vizuri, watu wametoka Mwanza private sector wanabanwa vibaya mno kazini hawajui hata topics za kupitia wamekuja kujaribu bahati.
Mtu anafanya kazi kampuni ya Logistics anafanya overtime kila siku anatoka saa nne usiku, hajawahi soma hata siku moja.
Mtu yupo anasubiri kuingia venue anapigiwa simu za kazi na anarespond. Do you expect hawa wote wapate marks sawa na wewe?
Kwamba kati ya watu 800 wote ina maana kila mtu ana connection sijui amenunua nafasi. Na unachomaanisha wewe una akili sana hivyo hukustahili kutoitwa? Kwamba waliopita ni vilaza tu ila wewe babkubwa wamekuonea kukuacha.
Kwa mfano mkuu wewe unaamini una akili sana alafu mimi ni kilaza?
Hata kwa mwandiko, ujenzi wa hoja, mada tunazochangia humu jukwaani.
Tatizo lako ni kudhani una akili sana. You are not special my brother, na hii nchi ina watu wengi hata uwe na akili hauko peke yako. TRA haiwezi lia kisa Addons hajaitwa Oral. Jipange tena nafasi zitatajwa kazi haziishi, mbona kuna watu wameenda Oral mara mbili hawajaitwa sasa ungekuwa wewe si ungevamia ofisi na kujilipua.