Matokeo ya Necta siku hizi ya kawaida sana.

TOHATO

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
1,170
3,775
Miaka ile hakuna kitu kilikuwa cha mshtuko kama usikie matokeo.
Matokeo yakitangazwa lazima siku mbili tatu uskie wawili watatu wamejinyonga mwingine mara kanywa sumu.
Ila sa hivi hata hupati habari ya kuna aliejaribu kujiuwa.
Ni kawaida sana kipindi kile kukuta familia nzima na mwanafunzi wakilia kisa mwanafunzi kafeli au wazazi wanamfanyie sherehe kisa mtoto kafaulu ya kwenda UALIMU (four au three ya mwisho)
Ila leo hata yaezekana tanzania one kwao hapafanyiki sherehe yoyote.
 
Utandawazi..me leo nimemaliza chuo kikuu kijijini kwetu hawajui nilikuwa nimeenda wapi...mambo yanaenda kasi mambo ya kujuana juana yameisha...kila mtu anapambana na hali yake
 
Hamna wa kushtuka, maana hata walioafaulu na kumaliza vyuo wamejaa mitaani, kwa hiyo hata dogo akifeli huko, anaona hana tofauti na kaka yake au dada yake aliyemaliza chuo na kupaki bus nyumbani.:D
 
Siku hizi hasa kwenye utawala huu wa Jiwe everything is forgery ili kuwapata wajinga wajinga waamini CCM iko vizuri kusimamia elimu yetu kumbe wanazidi kuzalisha wajinga tu.
 
siku hizi wanaosumbua mitaani ni kuna diamond na hawajasoma.. na wanasema kabisa sisu hatujasoma kwenye vyombo vya habari.. madogo wanaona wabunge wanajitamba kina msukuma hawajasoma na wanajitamba.. hata madogo wanaona elimu sio muhimu sana....

zamani tuliaminishwa elimu muhimu peke yake.. mtu akifeli anajiona kafeli maisha anajiua
 
Miaka ile hakuna kitu kilikuwa cha mshtuko kama usikie matokeo.
Matokeo yakitangazwa lazima siku mbili tatu uskie wawili watatu wamejinyonga mwingine mara kanywa sumu.
Ila sa hivi hata hupati habari ya kuna aliejaribu kujiuwa.
Ni kawaida sana kipindi kile kukuta familia nzima na mwanafunzi wakilia kisa mwanafunzi kafeli au wazazi wanamfanyie sherehe kisa mtoto kafaulu ya kwenda UALIMU (four au three ya mwisho)
Ila leo hata yaezekana tanzania one kwao hapafanyiki sherehe yoyote.
Mazingira na mfumo wa elimu wenyewe mkuu. Serikali na hiyo wizara husika imekosa imani kutoka kwa jamii nzima. Miaka hii kufaulu mtoto toka la saba kwenda sekondari eti lazima,ajabu usikate ana maliza Form4 hajui kusoma(wonders),watoto wa vigogo wakifeli sana bac matokeo yana standardaiziwa asa nani anashangaa lipi na ashtuke na lipi, mtu mtoto wake hata apate ine ya 7 wala hashtuk anajua pengine kompyuta zilimark vibaya
 
Back
Top Bottom