kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 277
Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Jangwani, Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, kimewatimua viongozi wake wajuu kwa kosa la kushirikiana na vyama vya upinzani katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini kote Oktoba 31, 2010.
Uamuzi huo umefikiwa katika mkutano wa dharura wa Halmashauri Kuu ya Kata hiyo, kilichofanyika kwenye ofisi za Chama hicho juzi.
Waliofukuzwa uongozi ni Mwenyekiti wa Kata hiyo, Tambaza Mohamed Tambaza na Katibu wa Kata, Ali Sindo.
Wengine ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi, Gungurugwa Tambaza, Mwenyekiti wa UWT, Farma Shaban na Mjumbe wa Kamati ya Siasa, Zakaria Digosi.
Kikao hicho kiliitishwa ili kujadili taarifa za tathimni ya uchaguzi ngazi ya matawi, kuhusu uchaguzi huo.
Katika mjadala huo, viongozi wote wa matawi yanayounda Kata hiyo, walionyesha kuchukizwa na hatua ya viongozi hao kwenda kinyume na maelekezo ya Chama huku wakiwarubuni wapiga kura kutokipigia CCM.
Awali kabla ya kutolewa hoja ya kuwatimua viongozi hao, wajumbe kutoka mashina, walitishia kurudisha kadi zao za CCM kama ishara ya kunawa mikono, kutokana na kulaumiwa na wanachama.
Mwenyekiti wa kikao hicho, Ally Chuma, alisema CCM Kata ya Jangwani ilikuwa hatarini kufa baada ya kukaa miaka miwili, bila viongozi kuitisha vikao.
Uhai wa Chama chochote ni vikao, viongozi wetu wamekaa miaka miwili hawaitishi vikao, uchaguzi ulipowadia, wakawa wanavipigia debe vyama vya upinzani, wanachama wanalalamika wamebaki wakiwa, CCM Jwangwani imekuwa Kata yatima kuliko zote duniani, alisema.
Alisema viongozi hao bila kushirikiana na uongozi wa tawi, walishirikiana na wahuni kufungua shina la wakereketwa linaloitwa Bosinia na kuzusha vurugu kubwa na kukitia Chama aibu.
CHANZO: NIPASHE