Matokeo ya maisha ya kutaka kufurahisha watu

Mr George Francis

Senior Member
Jun 27, 2022
186
212
MATOKEO YA MAISHA YA KUTAKA KUFURAHISHA WATU.

[Somo la leo 19/11/2022]

Maisha ya kutaka kufurahisha nafsi za watu wengine mara nyingi huishia katika kuumiza nafsi zetu.

Tunaweza imani na matarajio makubwa kwao wakati huo wao wanatuchukulia kwa ukawaida sana na pengine kutokuona mchango wetu katika maisha yao.

Kuna wakati unaweza kuacha kufanya mambo yako binafsi ili ufanye kile wanachokihitaji wao ukifanye kwaajili yao. Na tunashindwa kukataa kwa kuogopa labda tutawaudhi au watajisikia vibaya.

Bila shaka utakubaliana na mimi kwamba wengi tumejikuta tunaingia katika mtego huu kutokana hasa na kitanzi cha urafiki, undugu, mapenzi au boss zetu katika kazi na kadhalika.

Lakini leo nataka mimi na wewe tujinasue katika mtego huu.

Ni muhimu kutambua kuwa kamwe huwezi kumfurahisha kila mtu kwa kila kitu.

Kamwe huwezi huwezi kufanikiwa maishani kwa kutaka kufurahisa watu na kuacha kufanya mambo yako ya msingi.

Kutaka kufurahisha watu wengine hakutabadilisha hatima bora ya maisha yako bali kutazidi kufanya uendelee kuwa mtumwa wao.

Kamwe huwezi kuwa na furaha ya kudumu kwa kutaka kuishi maisha ya kufurahisha watu wengine kwasababu matarajio yako kwao sio matarajio yao kwako.

Kamwe hutafanya vitu vya maana vinavyohitaji kujitoa bali utafanya vitu vya kawaida vilivyozoeleka kufanyika ili kutowaumiza.

NAKUHAKIKISHIA Utaendelea kusubiri sana na hali uliyonayo hadi pale utakapojinasua katika mtego wa kufurahisha nafsi za watu na kuanza kufanya mambo yako ya msingi bila kujali watu watakuchukia, watakuchuliaje au watasema nini dhidi yako.

Ndugu yangu, wakati wa kuamka ni sasa. Jiondoe katika utumwa wa kuishi maisha ya kutaka kufurahisha watu wengine. Hakuna faida yoyote utakayoipata zaidi ya kujitengezea umasikini na maisha ya kuja kulaumu watu hapo baadae.

Matokeo ya kuishi maisha ya kutaka kufurahisha watu wengine leo hii ni kuja kuishi maisha ya kulaumu watu wengine katika siku zijazo za maisha yako.

#trainyourmind

It's me
Mr George Francis
A Digital Creator
Lawyer and LifeCoach

mr.georgefrancis21@gmail.com
 
Mkuu ongezea nyama kidogo, aisee kidogo umenigusa sana baada ya kuzama kwenye penzi la mtoto mmoja. Na sasa najitahidi kufanya kila linalowezekana ili mradi niwe na furaha. Ila hanitaki tena.😭😭😭
 
Mkuu ongezea nyama kidogo, aisee kidogo umenigusa sana baada ya kuzama kwenye penzi la mtoto mmoja. Na sasa najitahidi kufanya kila linalowezekana ili mradi niwe na furaha. Ila hanitaki tena.😭😭😭
Hakuna namna, hapo ni kumove on na kufanya maisha yako tu. Mapenzi hayalazimishwi ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom