Matokeo ya Maalim Seif Kumtambua Karume

Maalim yupo Mtoni si kwa hisani ya SMZ bali ni sheria kabisa unajuwa kuwa Maalim ni waziri kiongozi mstaafu wa SMZ,na anapata haki zote za ustaafu wa nafasi hiyo kama wanazopata Bilali na Ramadhani Haji Faki?
Kwa hiyo ni kweli kabisa anaijuwa vizuri kwa kuwa ameshakuwa kiongozi wake na anaijuwa CCM na SMZ vizuri zaidi kuliko hata Shamsi Nahodha na Hamza
Kijumba chake pale mtoni hakina kibali cha ujenzi...
 
Kwa hakika hawa jamaa wawili ningekuwa na muda wakuongea nao ningewaambia... as leaders wamefeli... kutatua mgogogoro ambao sio wa wananchi bali wa viongozi.
 
Kijumba chake pale mtoni hakina kibali cha ujenzi...

Vile viota vya waheshmiwa mafisadi wa SMZ; kule mbweni, chukwani, kiembe samaki na kwa mchina, vina vibali??

Kwa mtazamo wangu, Maalim ni mtu muadilifu sn na ni muungwana sn na hana makuu; ndio maana amejijengea kijumba cha kawaida sn.

Kibs, jamaa zako wapoje? si ndio wale kila mahala "hapa pangu"???
 
Uzuri Maalim Madevu anajua ni nini SMZ, otherwise asingekuwepo Mtoni leo hii!
.Zile ndevu zake kabadilisha siku hizi (kama nilivyoona katika picha). Haweki ndevu za kibedui tena bali anaweka ndevu za Maulama (zile za kidevuni hasa -goatee). Nafikiri Maalim anabadilika sasa.
 
Mkutano wa wawili hao umezungumzia kushirikiana katika kupinga mambo ya muungano! Hiyo poa lakini the looser will be Maalim Seif. Karume has nothing to loose maana kipindi cha utawala wake ndio hicho kinayoyoma ila anamkabidhi Triger bwana Shariff. Kwa wale wanaopenda muungano ni lazima waanze kusikitikia working relationship nzuri ya CUF na CCM, lakini wale wanaotaka Muungano uvunjike ni lazima wafurahie maendeleo haya.
If i were JK, ningehakikisha hakuna amani kati ya wawili hawa ili muungano usije ukavunjikia mikononi mwangu na ningehakikisha wanavurugana kila siku ili wote waone umuhimu wangu waniombe kuingilia kusaidia kutuliza presure wanazo peana.
Sijui kama JK na wasaidizi wake wanaliona hili.
 
....If i were JK, ningehakikisha hakuna amani kati ya wawili hawa ili muungano usije ukavunjikia mikononi mwangu na ningehakikisha wanavurugana kila siku ili wote waone umuhimu wangu waniombe kuingilia kusaidia kutuliza presure wanazo peana.Sijui kama JK na wasaidizi wake wanaliona hili.

Wazenji wakisema Wabara wamewafanya kuwa ni Znz ni KOLONI lao mnapinga; ila mawazo yenu je, mbona yamekaa ki-ukoloni ukoloni???

CCM bara watalitolea kauli siku si nyingi hili la kukutana wawili hawa, maana wao ndio King maker wa madhila yote wayapatayo Wazanzibar kipindi cha chaguzi zote tangu kurudi kwa mfumo wa vyama vingi; tusubiri.
 
Karume na Sharif kuwa pamoja ni jambo jema kwa kuleta ummoja kwa wanzazibari lakini ni pigo kwa CCM bara.Wakiungana wawili hao basi ujue muungano uko mashakani.
 
Leo Zanzibar imefungua ukurasa mpya katika siasa za Zanzibar, baada ya Chama cha CUF kutangaza rasmi kumtambua Rais Karume kama rais halali wa Zanzibar, hii ikiwa ni hatua kubwa ya kwanza kuelekea muafaka wa kweli kuhitimisha uhasama wa kisiasa kati ya vyama hivi viwili.

Tangazo la utambuzi huo limetolewa na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Shariff Hamad, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kibanda Maiti jioni ya Leo.
Source: TBC News.

Utambuzi huu unafuatia kikao cha faragha cha wawili hawa. Uamuzi huu, utaleta tumaini jipya kwenye visiwa hivi vya karafuu. Mambo yafuatayo yatafuatia wiki ijayo
1. Karume atamteua Maalim na Juma kuingia Barazani.
2. Cuf watarudi mezani mazungumzo ya Muafaka
3. Muafaka kutekelezwa baada ya Uchaguzi 2010.
progress.gif
 
Haya ni maandalizi kama wanavyo yaita wao wenyewe ya kuwa na Nchi ya Zanzibar . Hii ndiyo siri kubwa juu mkutano huu . Lakini sasa wacha tuone Maalimu anavyo wachezea Wapemba na wana CUF . Mazungumzo ya 2 tu then maamuzi yanatangazwa . CUF mwisho wake . Je wale walio mwaga damu na kuzikwa inakuwaje ?Unamtumbua Karume usiku badala ya asubuhi ?
 
- Pasco, una maana hizi siku zote CUF walikuwa hawamtambui Karume? Are you serious mkuu wangu au?

- Una maana walikuwa hawaendi bungeni au kwenye Baraza la Wawakilishi ambako Karume ni makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar?

Respect.

FMEs!
 
Mi nilijua tu ile kahawa ya juzi kati ya Maalim na Karume si bure!
 
Haya ni maandalizi kama wanavyo yaita wao wenyewe ya kuwa na Nchi ya Zanzibar . Hii ndiyo siri kubwa juu mkutano huu . Lakini sasa wacha tuone Maalimu anavyo wachezea Wapemba na wana CUF . Mazungumzo ya 2 tu then maamuzi yanatangazwa . CUF mwisho wake . Je wale walio mwaga damu na kuzikwa inakuwaje ?Unamtumbua Karume usiku badala ya asubuhi ?

Upo sahihi kabisa.

Sasa Zanzibar kutetea maslahi yao ndani ya muungano bila kujali itikadi na kwa nguvu sana. Kinachofuata? Maalimu anakuwa kiongozi wa Upinzani ndani ya Baraza la Wawakilishi na kupewa hadhi zote za Ofisi hiyo kama Hamad Rashid katika Bunge la Muungano. Kisha Maalim Seif anakuja Bunge la Muungano katika nafasi 5 za Baraza la Wawakilishi.

Patamu sana........................................... what unfolds? Huu ni wakati ambao Zanzibar itapata kila itakacho maana CCM bara ipo hoi kwa magomvi na hawana umoja. Sikilizia
 
- Pasco, una maana hizi siku zote CUF walikuwa hawamtambui Karume? Are you serious mkuu wangu au?

- Una maana walikuwa hawaendi bungeni au kwenye Baraza la Wawakilishi ambako Karume ni makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar?

Respect.

FMEs!

CUF hawajawahi kumtambua Karume kama Rais wa Zanzibar wala serikali yake. Kaka Rais wa Zanzibar siku hizi sio makamu wa Rais. Ilifutwa hiyo toka mwaka 1995 ndio maana kuna Shein pale
 
- Pasco, una maana hizi siku zote CUF walikuwa hawamtambui Karume? Are you serious mkuu wangu au?

- Una maana walikuwa hawaendi bungeni au kwenye Baraza la Wawakilishi ambako Karume ni makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar?

Respect.

FMEs!

Wanadai walikuwa wanamtambua "de facto" tu lakini sasa wameamua kumtambua rasmi "de jure!" Anyway, kadri muda utakavyokuwa unaenda tutajua hii "u turn" ya CUF inamaanisha nini!
 
Mwanzo mzuri.Labda Tanganyika yetu na sisi itarudi.Wacha tuje tukabane makoo wenyewe kwa wenyewe!
 
Upo sahihi kabisa.

Sasa Zanzibar kutetea maslahi yao ndani ya muungano bila kujali itikadi na kwa nguvu sana. Kinachofuata? Maalimu anakuwa kiongozi wa Upinzani ndani ya Baraza la Wawakilishi na kupewa hadhi zote za Ofisi hiyo kama Hamad Rashid katika Bunge la Muungano. Kisha Maalim Seif anakuja Bunge la Muungano katika nafasi 5 za Baraza la Wawakilishi.

Patamu sana........................................... what unfolds? Huu ni wakati ambao Zanzibar itapata kila itakacho maana CCM bara ipo hoi kwa magomvi na hawana umoja. Sikilizia

Mkuu Zitto heshima mbele,

Hapo ndo tunasema hapa kuwa upinzani mlitakiwa kuseize hii opportunity na kumobilise umma tayari kwa 2010.

wakati CCM wakiparurana huko, hapa tulitegemea alternatives kama Chadema muwe mitaani mkiwaeleza watu kinagaubaga ni nini kinaendelea nchi hii na incompetence ya huu utawala uliopo. Maana si wananchi wengi wenye access ya habari/taarifa kama ilivyo hapa JF.

Lakini, ndio kwanza Maalim yupo Ikulu anaweka mambo yake sawa na mh Karume, huku mkuu kama wewe tunayekutegemea bungeni nasikia upo Jordan kwenye mkutano, sijasikia viongozi wengine wa Chadema wanasemaje kwenye hili!

Mi nilidhani hii ni a golden window of opportunity kwa upinzani Tanzania kuonyesha makali yake!
 
Jamaa wamekumbuka- Ndugu wakigombana shika jembe ukalime...watakapopatana - Zenji wanavuna karafuu. Hata Karume kashtuka hapa nazenguliwabora nijipange kivyangu
 
Back
Top Bottom