Watanzania toka usingizini...meli inazama??? ndiyo kabisa wanapata usingizi mnono!
Matokeo yanasikitisha, je nini Kifanyike? Mara nyingi watanzania wamekuwa ni wengi wa lawama kuliko kutoa suluhisho. Si kwa maoni tu, bali hata kwa vitendo. Tanzania itaimarishwa na sisi wenyewe....watanzania wenyewe...ila kinachoonekana sasa ni lawama kuliko suluhu.
Kila aliyeko nje ya mfumo...hapa namanisha katika kutoa maamuzi ya utekelezaji wa sera kama mawaziri n.k anaonekana kulalamika. Wazazi pia badala ya kusaidia kujinasua na matatizo ya namna hii nao pia wanalalama. Mifumo ya kufundishwa ili wajibu mitihani na si kuelewa hasa huko sekondari inapelekea matatizo katika vyuo vikuu...wanafunzi hata vyuoni hawaonekani kusoma vitabu wenyewe wanataka "spoon feeding" hali hii inasikitisha.
Hata hao waliofuhulu wakifika vyuoni mambo ni yale yale...unashindwa kujua hata wamepitaje huko masekondari..wanakuja na hayo matokeo mazuri ya kujivunia, wengi wanatoka shule zinasifika kwa kufundisha kwa kiingereza nyingine zimejaa walimu toka jirani...lakini inawawia vigumu kufuatilia masomo ambayo hata hivyo yako kwa lugha ya Kiingereza..sasa nani wa kulaumiwa. elimu ni biashara kwa sasa.
Inapendeza mtoto wako akisoma shule inayofahulisha sana na akafahulu kwenye hizo grade nzuri tunazoziona, na kwa kuzingatia hivyo hakuna mwenye shule atakayependa kuona matokeo yanakuwa mabaya...kwa vile anataka kuvutia wazazi walete watoto wao katika shule hiyo na pia anaweza kupandisha ada anayotaka...waliosoma uchumi mnajua "supply and demand" Naomba nieleweke vema, hapa sisemi shule hizi zote zina matatizo au upungufu wa namna hiyo...huduma inayotolewa katika mashule haya pia inaridhisha kwa wazazi. Lakini ni asilimia ngapi ya shule za namna hii, na ni watanzania wangapi wanaweza kugharimia watoto wao katika shule hizi kuanzia mchakato wa kufanya usahili wa kuingia katika mashule haya...gharama ni kubwa, na je shule hizi ziko wapi? mjini au vijini?
Mweleke wa Elimu Tanzania ni hupi??? wazazi wanachangia haya, silaumu sana wazazi kwa vile baadhi yao hawana uelewa wa kutosha na wengi wao wanasukumwa na utajiri walionao, na pia sasa Tanzania inabadilika tunarudi katika mfumo wa Kibepari bila kujitambua, je mnasubiri Katiba ya nchi ibadilishwe ndiyo mjue kuwa sasa Tanzania ni nchi ya kibepari. Wenye nacho wataendelea kuwa nacho na pia wataendelea kutawala hii nchi hata kama uwezo wao wa kufikiri na kuchanganua mambo ya kusaidia maendeleo ya Taifa ni mdogo. Hili hatutalikwepa, majina ya viongozi, wakurugenzi, makatibu wakuu nk yatabaki kujirudia rudia rudia. Si elimu tu, watato wangapi wa "vigogo" wanasoma katika mfumo wetu, vigogo wangapi wanatibiwa katika hospitali za serikali? mengi yamesemwa!
Huu ndiyo mfumo, wanasayansi wamepungua, vijana na hata wazazi hawataki kusikia watoto wao wanasoma haya masomo ya sayansi..sababu zinajulikana...hakuna maslahi na serikali haijatilia mkazo..utashangaa serikali yaweza kuazima wasomi kutoka nje ya nchi..wanahitwa watalaam...madaktari, walimu hata vyuo vikuu..kisa hatuna wataalamu wa kutosha..wanalipwa pesa za kutosha...je ni wapi tumejikwaa? na je tuna mipango ya muda mrefu ya kuokoa taifa kutokana na utegemezi wa namna hii au mambo yataendelea kuwa kama yalivyo hadi lini? na hii ndiyo tunasema ni ufisani kila mtu anajitazama mwenyewe..
Wizi wa mitihani ni tatizo kubwa, linahitaji suluhu lakini hili linawezekana? sijui ni watu wangapi waliohusika wamefikishwa katika vyombo vya sheria na kuhukumiwa..nasikia mara vijana/wanafunzi wamekamatwa na paper...wanazitoa wapi? paper kuvuja kumeanza lini? na je wahusika ni akina nani? wazazi wanahusika pia...sasa mfumo huu utabadilishwa na nai????
Mimi ni mwalimu pia, utashangaa unawauliza wanafunzi maswali ambayo unafikiri kwa upewo wao wanaweza kuyajibu...wanakwambia wao wamefundishwa maswali na mjibu na si kufikiri na kutoa majibu kutokana na wanavyofikiri wa pia...mtihani ukifika wanakuuliza tusome wapi? ukiwambia wakasoma kwenye maktaba na kuwaeleza ni vitabu gani wakasome...hawana muda. wengine wanajichora pia kwenye viganja vya mikono, kuweka makaratasi vyooni n.k...ubaya zaidi mfumo wa elimu wa Tanzania kuanzia shule ya msingi ni kuangalia mwanafunzi amepata maksi ngapi..aliyepata nyingi ndiye mwanafunzi bora, hili ni tatizo, huku kwa wengine, mtihani wa mwisho unakuwa na maksi kidogo...mahudhurio, michango ya mijadala madarasani inapewa umuhimu pia....
Vyuo vikuu vilianzisha majaribio kabla ya kuingia kwenye vyuo hivyo...je hii ni biashara au kweli inachuja wanafunzi? mimi bado naona sasa imekuwa kama mazoea na "deal" kwa vyuo husika...na hawa kesho wanalalamika ni wanafnzi gani hawa wametoka wapi? wanatilia mashaka necta? mimi sijui...lakini utakuta mwanafunzi hawezi kujieleza darasani lakini mwanafunzi huyu amefahulu NECTA, amefahulu ENTR EXAMINATION za vyuo, ukiwa naye darasani hapo vyuo vikuu utashanga..tunaelekea wapi? ni nani wa kufungwa jiwe shingoni na kutupwa baharini??? Hii haiishii hapo vyuoni, waajiri nao wanafanya usahili ili kupata wafanya waajiriwa bora...utasikia wanaulizana kweli huyu katoka chuo kikuu? na tena kile tunachojua kuwa ni bora? waandishi wa habari anoa pia wako katika mkumbo huu....walimu pia. Viongozi hao usiseme! VIHIYO wataisha Tanzania au angalau kupungua????
Kazi kwetu.
Jasson
Korea Kusini