Matokeo ya Darasa la Saba yatangazwa rasmi

Neiwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
731
1,000
Wakuu,

Leo tuangalie upande wa shule za Msingi, matokeo kutupa picha ya mwelekeo wa elimu kama unazidi kudorola ama kuna matumaini ya kunyooka.

kaimu.jpg

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Dk Charles Msonde akionyesha moja ya karatasi za majibu ya mtihani wa darasa la saba kwa waandishi wahabari Dar es Salaam jana, wakati wa kutangaza matokeo ya mtihani huo wa mwaka huu.

Imeelezwa kuwa ufaulu wa mtihani wa kumaliza darasa la saba kwa mwaka 2013 umepanda kwa masomo yote kwa asilimia 19.89 ikilinganishwa na ilivyokuwa kwa mwaka uliopita.

Kwamba, wakati mwaka jana wahitimu waliopata asilimia 100 walikuwa asilimia 30.72, mwaka huu wameongezeka kuwa asilimia 50.61. Pia, somo ambalo watahiniwa hao wamefaulu zaidi katika mtihani wao ni Kiswahili ambapo ufaulu ni

asilimia 69.06 huku wakiwa wamefeli zaidi kwenye somo la Hisabati ambalo ufaulu upo chini kwa asilimia 28.62.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk. Charles Msonde alisema wanafunzi 427,606 walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2013 huku kiwango cha udanganyifu kikizidi kudhibitiwa hivyo kupungua.

Alisema NECTA imefuta matokeo yote ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa watahiniwa 13, ambao walibainika kufanya udanganyifu kwenye mtihani au kurudia pasipo ruhusa ya Baraza. Watahiniwa waliofutiwa mwaka jana ni 293.

Alisema kati ya wanafunzi hao, 844,938 waliofanya mtihani huo wamepata alama zaidi ya 100 katika alama 250: "Idadi hiyo ni sawa na asilimia 50.61. Kati yao wasichana walikuwa 208,227 (sawa na asilimia 46.68) na wavulana 219,379 sawa na asilimia 55.01," alisema.

Dk. Msonde alisema katika ufanyaji wa mtihani huo, pia walikuwepo watu wenye ulemavu, ambapo wasichana walikuwa 219 na wavulana 257.

Alisema matokeo hayo yatapelekwa maeneo yote husika ili mchakato wa upangaji shule ukifanyika kwa watahiniwa wote waliofaulu mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi.

Kuhusu usahihishaji mitihani, Dk. Msonde alisema ili kujiridhisha na usahihi wa zoezi la usahihishaji wa kutumia mfumo wa kompyuta (Optical Mark Reader - OMR), sampuli za karatasi 20,795 za majibu ya watahiniwa wa shule 200 kutoka wilaya 48 zilichukuliwa kutoka shule za mikoa tisa ya (Iringa, Kagera, Shinyanga, Manyara, Njombe, Mbeya, Morogoro, Katavi na Tanga) na kusahihishwa kwa mkono: "Ulinganifu baina ya alama za watahiniwa zilizopatikana kwa kusahihishwa kwa mkono na zile zilizotokana na usahihishaji wa mfumo wa kompyuta ulifanyika na kubaini kompyuta ilikuwa sahihi,"alisema.

Amesema makosa yaliyojitokeza katika karatasi zilizosahihishwa kwa mkono ni kuweka pata pale ambapo kuna kosa ama kuweka kosa pale ambapo kuna pata, makosa ambayo kwenye usahihishaji wa kutumia kompyuta hakuwepo.

Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi Tanzania (TAMONGSCO), Mahmoud Mringo alisema shule binafsi zimeongoza katika matokeo hayo kwa kila somo.

Alisema katika somo la Kiswahili, shule binafsi wamepata asilimia 98 wakati za Serikali asilimia 68, na kwa Kingereza shule binafsi asilimia 99 na Serikali 33. Kwa somo la Maarifa ya Jamii, shule binafsi asilimia 86 Serikali 52 , Hisabati shule binafsi asilimia 81 na Serikali 27 na somo la Sayansi, shule binafsi asilimia 84 na Serikali 46.

Matokeo ya dalasa la saba yaliyopachikwa hapo juu pia yanapatikana katika tovuti za:


Source: Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2013 - wavuti.com

Dar es Salaam. Zaidi ya asilimia 50 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba Septemba mwaka huu, wamefaulu. Matokeo hayo yalitangazwa jana na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde aliyesema ufaulu huo ni ongezeko la asilimia 19.89 ikilinganishwa na mwaka jana.
Alisema jumla ya watahiniwa 844,938 walifanya mtihani huo na kati yao 427,606 sawa na asilimia 50.61, wamefaulu kwa zaidi ya alama 100 kati ya 250.

Dk Msonde alisema kati ya watahiniwa hao waliofaulu, wasichana ni 208,227 sawa na asilimia 46.68 na wavulana ni 219,379 sawa na asilimia 55.01. Matokeo hayo pia yanaonyesha kuwa, wanafunzi wengi wamefanya vibaya zaidi kwenye somo la Hisabati huku wakifanya vizuri kwenye somo la Kiswahili.
Dk Msonde alisema wavulana wamefanya vizuri zaidi kwenye mtihani huo ukilinganisha na wasichana.
Alieleza pia kuwa, mwaka huu udanganyifu kwenye mtihani huo umeshuka kwa kiasi kikubwa, kwani waliofutiwa matokeo ni 13.

Dk Msonde alisema kati ya hao, watano walibainika kukariri mtihani huo jambo ambalo kisheria hawaruhusiwi na wengine walikamatwa na karatasi za majibu kwenye vyumba vya mtihani.

Ufaulu

Alisema miongoni mwa waliofaulu, wenye ulemavu ni 476, kati yao wasichana wakiwa ni 219 sawa na asilimia 46.01 na wavulana ni 257 sawa na asilimia 53.99. Dk Msonge alisema kuwa, mwaka 2012 watahiniwa waliopata zaidi ya alama 100 walikuwa ni asilimia 30.72, hivyo mwaka huu kuna ongezeko la asilimia 19.89.

Kuhusu sababu za ongezeko la ufaulu, Dk Msonde alisema baraza bado halijafanya tathmini ya kubaini chanzo cha ongezeko hilo. "Sisi tulicholetewa ni kile kilichofanyika kwenye chumba cha mtihani na haya hapa ndiy o majibu yake," alisema Dk Msonde.

Ufaulu kimasomo

Alisema mwaka huu ufaulu kwa masomo yote umepanda kwa asilimia kati ya sita mpaka 28.06, ikilinganishwa na mwaka 2012.

Somo ambalo watahiniwa wengi wamefanya vizuri ni Kiswahili ambalo ufaulu wake umefikia asilimia 69.62 na walilofeli zaidi ni Hisabati ambalo ufaulu wake ni asilimia 28.62. Takwimu zinaonyesha kuwa, mwaka 2012 ufaulu kwenye somo la Kiswahili ulikuwa ni asilimia 41.00 na Hisabati ulikuwa ni asilimia 18.74.

Kwenye somo la Kiingereza ufaulu mwaka huu ni asilimia 35.52 wakati mwaka jana ilikuwa ni asilimia 21.06, huku kwa Sayansi mwaka huu ufaulu ukiwa ni asilimia 47.49 na mwaka jana ilikuwa ni asilimia 41.48 na Maarifa ya Jamii mwaka huu ufaulu ni asilimia 53 na mwaka jana ilikuwa asilimia 28.61.
Usahihishaji wa mashine ni bora zaidi

Alisema ili kujiridhisha na usahihishaji wa kutumia Mashine Maalumu za OMR (Optical Mark Reader), sampuli 20,795 za karatasi za majibu ya watahiniwa wa shule 200 kutoka wilaya 48 za mikoa tisa ya Iringa, Kagera, Shinyanga, Manyara, Njombe, Mbeya, Morogoro, Katavi na Tanga zilisahihishwa kwa mkono.
Alisema baada ya kufanya ulinganifu wa usahihi wa karatasi zilizosahihishwa kwa mkono na zile zilizosahihishwa kwa mashine, ilibainika kuwa zile zilizosahihishwa kwa mashine zilikuwa na usahihi wa hali ya juu.

"Usahihishaji wa kutumia kalamu ulikuwa na makosa machache ya kibinadamu, makosa hayo yalikuwa ya kukosea kusahihisha swali kwa kutumia mwongozo wa usahihishaji na dosari za kujumlisha alama," alisema Dk Msonde.

Alibainisha kuwa, kati ya sampuli za karatasi za watahiniwa 20,795 zilizosahihishwa kwa mkono, 249 sawa na asilimia 1.2 ndizo zilizobainika kuwa na makosa aliyosema ni ya kibinadamu.

Mbali na usahihi wa usahihishaji, alisema pia mfumo huo umesaidia kupunguza wasahihishaji kutoka 4,000 waliokuwa wakitumika awali na kufikia 301 waliofanya shughuli hiyo mwaka huu. Alibainisha pia kuwa, OMR imepunguza siku za kusahihisha mtihani huo kutoka 30 za awali mpaka 16 zilizotumika mwaka huu.

Waliofanya mtihani

Alisema watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani huo walikuwa ni 867,982 wakiwamo wasichana 455,896 sawa na asilimia 52.52 na wavulana 412,087 sawa na asilimia 47.48. Alieleza kuwa, kati ya watahiniwa hao walikuwemo wenye ulemavu wa kuona, 597 walikuwa na uono hafifu na wengine 88 ni wasioona.

"Watahiniwa 844,938 sawa na asilimia 97.34 ya waliosajiliwa walifanya mtihani huo. Wasichana walikuwa 446,115 sawa na asilimia 99.85 na wavulana walikuwa 398,823 sawa na asilimia 96.78," alisema Dk Msonde.
Alisema kuwa, watahiniwa ambao walisajiliwa na hawakufanya mtihani huo ni 23,045 sawa na asilimia 2.66, kati yao wasichana wakiwa 9,781 sawa na asilimia 2.15 na wavulana 13,264 sawa na asilimia 3.22.
Alieleza kuwa utoro na ugonjwa ni miongoni mwa sababu za wanafunzi hao kutofanya mtihani huo.
Lengo la BRN halijafikiwa.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa akizungumza katika warsha ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN-Big Results Now), kwenye sekta ya elimu iliyotolewa kwa watendaji wa elimu ngazi ya kanda, mkoa na wilaya, Agosti 14, mwaka huu, alisema moja ya lengo la mpango huo ni ufaulu kwa darasa la saba mwaka huu kufikia asilimia 60 kutoka 31 ya mwaka jana.

"Katika kutekeleza vipaumbele hivyo, kila mmoja wenu atakuwa na eneo la kutekeleza na atapimwa kutokana na utekelezaji katika eneo lake, hii ni katika kuhakikisha kuwa kuanzia mwaka huu ufaulu katika elimu ya msingi unaongezeka kutoka asilimia 31 hadi kufikia 60," alisema Dk Kawambwa.

Mara baada ya Dk Kawambwa kutangaza suala hilo, baadhi ya wadau walisema itaongeza hali ya kupata matokeo yasiyo halisi kwani hakukuwa na muda wa kuandaa mikakati ya kufikia lengo hilo, kwani mpango huo ulitangazwa Agosti na Septemba watoto wa darasa la saba walikuwa wanaanza mitihani.


Chanzo: Mwananchi

Tusiime kinara wa matokeo ya mtihani darasa la saba Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla 2013

Kwa mujibu ya matokeo yalitotangazwa na naibu katibu mtendaji wa baraza la mitihani la taifa (NECTA), Dr. Charles Msonde shule ya Tusiime imekua katika nafasi kama ifuatavyo,

Number 1 kwa wilaya ya Ilala kati ya shule 99
Number 1 kwa mkoa wa Dar es Salaam kati ya shule 486
Number 2 kitaifa kati ya shule 15656

katika wanafunzi 158 waliofanya mtihani huo, ...

157 wamepata wastani wa daraja A na mmoja daraja B
124 wamepata alama A kwa masomo yote matano (straight A)

katika wanafunzi 158,Shule imepata wastani wa alama 230.0063 kati ya 250
ambapo shule ya kwanza kitaifa yenye wanafunzi 50 imepata wastani wa alama 230.8800
191750_285929034863884_815922324_o.jpg
 

Bushbaby

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
1,592
1,500
Kulikuwa na fununu kuwa matokeo yalikuwa mabaya sana......sasa kama wameamua kuwapeleka hata wasiojua kusoma secondary ili kuepuka aibu ya 0MR itajulikana tu.....
 

Campana

JF-Expert Member
Dec 2, 2008
207
195
Na hiyo multiple choice questions hata kwenye Hisabati, watakuwa wamefaulu wabahatishaji
 

Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
14,000
2,000
Na hiyo multiple choice questions hata kwenye Hisabati, watakuwa wamefaulu wabahatishaji

Mkuu hata UDSM siku hizi nasikia eti kuna multiple choice sasa kwa primary si ndiyo kabisa? Multiple Choice kwa hesabu sikuwahi kuiona!!!! enzi zetu? Ndiyo maana graduate ukimwambia akuandikie report ni bora ukae mwenyewe uandike utamaliza haraka zaidi kuliko kusahihisha document mpaka inabidi upate kikombe cha kahawa!!
 

Mpajiji

Member
Dec 17, 2012
76
0
Leo Waziri wa Elimu,Shukuru Kawambwa ametangaza rasmi maotokeo na kueleza kuwa kiwango cha ufaulu kwa mwaka huu kimeongezeka. Amesemawaliofaulu ni sawa na asilimia 64 ya wanafunzi walioandika paper ya D7 mwaka huu

Hongera madogo wote mliofaulu wazazi wawaandae kuanza shule Za sekondari january 2013
 

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,362
2,000
Watoto wao wanasoma nje kwenye shule bora na za ndani wanaziua ili watoto wao waje kuwatawala watoto wenu[/QUOTUko sahihi kabisa, si unaona watoto wao wako TANROADS, TRA, BOT etc. kayumba atakwenda huko kweli. lakini ni wazee wetu wa vijijini ndio wanaiweka CCM madarakani, ambao watoto wao ndio victim wa upuuzi huu wa shule! eti ufaulu umeongezeka kutoka wapi? Shame upon you kawambwa!
 

Nivea

JF-Expert Member
May 21, 2012
7,457
2,000
Watoto wao wanasoma nje kwenye shule bora na za ndani wanaziua ili watoto wao waje kuwatawala watoto wenu

na huku ndiko tunakoelekea jamani inasikitisha sanasana si unawaona watoto wa MAKAMBA wewe
 

Mshuza2

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
8,248
2,000
Wamechakachua weee..wamekuja na mbinu hii ya kuongezeka kiwango cha ufaulu,laiti script zingekuwa zinarudi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom