Matokeo ya darasa la 7 ni kituko na ni aibu kwa taifa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,331
33,141

MATOKEO YA DARASA LA 7 NI KITUKO NA NI AIBU KWA TAIFA

MCHAMBUZI: IMORI MARK

MATOKEO YA DARASA LA 7 NI KITUKO NA NI AIBU KWA TAIFA TOFAUTI NA ILIVYOWAKILIWASHWA KWENYE VYOMBO VYA HABARI NA WAZIRI HUSIKA.

WAZIRI ALISEMA IDADI YA WALIOENDA SEKONDARI IMEONGEZEKA UKILINGANISHA NA MWAKA JANA LAKANA JE WAJUA UFAULU WAO???

WALIOPATA:
A - 3,087,
B - 40,683,
C - 222,103
CHUKUA A+B+C = 265,873

WALIOCHAGULIWA KWENDA KIDATO CHA KWANZA NI560,706.

KWA HIYO WATAHINIWA 294,833
WAMECHAGULIWA KUTOKA DARAJA "D"
.......WAKATI DARAJA LA UFAULU KWENDA

SEKONDARI NI KUANZIA "C" ....
YAANI ALAMA 101/250.

ZAIDI YA 51% YA WALIOCHAGULIWA NI KUTOKA DARAJA "D" YAAN CHINI YA ALAMA 100/250.

JE, KTK HAWA 294,833 TUTAKOSA WASIOJUA KUSOMA NA KUANDIKA VIZURI?

--------------------------------------------------

UPDATE:
Mroki Mroki aka Father Kidevu wa mrokim blog anasema:
"Taarifa zinasema kuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inawataka Wazazi, Walezi na wanafunzi kufika katika Ofisi za Elimu Mkoa au Wilaya zao ndipo majina ya Wanafunzi na Shule walizopangiwa yanapatikana."

chanzo. http://freebongo.blogspot.com/2012/12/matokeo-ya-darasa-la-7-ni-kituko-na-ni_26.html?utm_source=feedburner&utm_medium=feed&utm_campaign=Feed%3A+Mpekuzi+%28MPEKUZI%29​

Hii ndio Tanzania hakuna Nchi kama hii na haitatokea.
Si unaona hata N/Waziri mwenyewe hajui Muungano uliotoa jina la Tanzania.........naamini hata yeye alikuwa kwwnye kundi la D au F.
Anyways tutegemeee miujiza kuwa hao nao watakuwa wanafunzi wazuri
 
Nasubiri malamiko ya waalimu wa sekondari hapo baadaye kidogo. Kuna watu wanaongea hadharani huku wemevaa tai na suti, kumbe wanalidanganya Taifa kwa makusudi.
 
Nasubiri malamiko ya waalimu wa sekondari hapo baadaye kidogo. Kuna watu wanaongea hadharani huku wemevaa tai na suti, kumbe wanalidanganya Taifa kwa makusudi.

Walimu walalamike nini badala ya kupeta na inshu zao
 
zamani wakati tunacheza chandimu (football ya mchangani), tulikuwa tunaweka vijigoli vidogo kama vile vya handball au hockey.

ikifika mahali timu zetu zinashindwa kufungana tulikuwa tunaamuaga kupanua magoli.

shukuru kawambwa & co wanacheza chandimu!!
 
halafu ulikuwa ni mtihani wa multiple choice mpaka hesabu!!
 
Na hii ina chain impact kwa vizazi mpaka na vizazi
ivi D toka lini ikawa ni kufaulu!
 
kwani A inaanzia ngapi na B vilevil kadhalika C

A= 81-100
B= 61-80
C=41-60
D=21-40 kwa Primary, na Secondary zote
Kwa higher learning
A=70-100
B+=60-69
B=50-59
C=41-49
D and E ni fail kwa University Undergraduate na kwa Postgraduate mwisho ni B, C and below ni fail!!!

Sasa angalia kiwango cha kufeli darasa la Saba!! Ni hatari na waalim wamejipongeza!! I tell you sekta ya ualimu na afya walisitisha mgomo na kurudi kazini but in actual facti bado wako katika mgomo!!!! Serikali watch out!! Vitisho havina tija!! Kaeni meza moja na myamalize!!
 
kinachonisikitisha na kunitoa machozi ni mtihani wa hesabu af uchague jibu sahihi tunachoandaa ni bomu la nyuklia siupendi huu mfumo hata kidogo ,rudien huu mfumo jamani wa swali,kazi au njia,jibu au majawabu napata shida kumuamin waziri mwenye dhamana kama anaitakia mema sekta ya elimu nchini,wadau nao wametulia,wazazi tupo kimnya,wabunge wametulia.NI WATOTO WETU NI JUKUMU LETU NA NI WAJIBU KUWATOA KWENYE HILI JANGA.
 
Taifa la tanzania haliwezi endelea kwa kuzingatia kigezo cha wingi wa wanafunzi darasani badala ya kuzingatia ubora wa elimu kwa wanafunzi waliopo darasani
 
kinachonisikitisha na kunitoa machozi ni mtihani wa hesabu af uchague jibu sahihi tunachoandaa ni bomu la nyuklia siupendi huu mfumo hata kidogo ,rudien huu mfumo jamani wa swali,kazi au njia,jibu au majawabu napata shida kumuamin waziri mwenye dhamana kama anaitakia mema sekta ya elimu nchini,wadau nao wametulia,wazazi tupo kimnya,wabunge wametulia.NI WATOTO WETU NI JUKUMU LETU NA NI WAJIBU KUWATOA KWENYE HILI JANGA.
hakika ni janga kuu ukizingatia na

  • ari ya ufundishaji kwa walimu ilivyoshuka,
  • mazingira ya kufundisha na kujifunza yalivyo duni,
  • uwiano walimu wa somo la hisabati kwa wanafunzi usivyoridhisha,
  • usimamizi na utawala duni wa mashule,
  • ukaguzi na ufuatiliaji dhaifu
hakika sekta ya elimu ya msingi ni jeneza linalosubiri kushushwa kaburini!
 
MATOKEO YA DARASA LA 7 NI KITUKO NA NI AIBU KWA TAIFA

MCHAMBUZI: IMORI MARK

MATOKEO YA DARASA LA 7 NI KITUKO NA NI AIBU KWA TAIFA TOFAUTI NA ILIVYOWAKILIWASHWA KWENYE VYOMBO VYA HABARI NA WAZIRI HUSIKA.

WAZIRI ALISEMA IDADI YA WALIOENDA SEKONDARI IMEONGEZEKA UKILINGANISHA NA MWAKA JANA LAKANA JE WAJUA UFAULU WAO???

WALIOPATA:
A - 3,087,
B - 40,683,
C - 222,103
CHUKUA A+B+C = 265,873

WALIOCHAGULIWA KWENDA KIDATO CHA KWANZA NI560,706.

KWA HIYO WATAHINIWA 294,833
WAMECHAGULIWA KUTOKA DARAJA "D"
.......WAKATI DARAJA LA UFAULU KWENDA

SEKONDARI NI KUANZIA "C" ....
YAANI ALAMA 101/250.

ZAIDI YA 51% YA WALIOCHAGULIWA NI KUTOKA DARAJA "D" YAAN CHINI YA ALAMA 100/250.

JE, KTK HAWA 294,833 TUTAKOSA WASIOJUA KUSOMA NA KUANDIKA VIZURI?

--------------------------------------------------

UPDATE:
Mroki Mroki aka Father Kidevu wa mrokim blog anasema:
"Taarifa zinasema kuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inawataka Wazazi, Walezi na wanafunzi kufika katika Ofisi za Elimu Mkoa au Wilaya zao ndipo majina ya Wanafunzi na Shule walizopangiwa yanapatikana."

chanzo. http://freebongo.blogspot.com/2012/12/matokeo-ya-darasa-la-7-ni-kituko-na-ni_26.html?utm_source=feedburner&utm_medium=feed&utm_campaign=Feed%3A+Mpekuzi+%28MPEKUZI%29​

Taifa lijiandae kushusha viwango vya kufaulu kwa kidato cha nne na kuendelea ........
 
uzuri wa watanzania tunaishiaga kulalamika tu... kisha upepo unapita.. Hakuna nchi rahisi kuongoza kama hii Duniani.
 
Back
Top Bottom