Matokeo ya Chadema Kususia Hotuba ya JK na Kuapishwa kwa Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matokeo ya Chadema Kususia Hotuba ya JK na Kuapishwa kwa Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Nov 17, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,097
  Trophy Points: 280
  Nimetumiwa Taarifa hii kutoka Dodoma ya kuwa pamoja na Mheshimiwa Pinda kuwatomasa Chadema Bungeni kuwa mbona wamemnunia na hawampigii makofi lakini hizo gheresha wabunge wa Chadema hawashtuki nazo na ya kuwa kuonyesha dhamira yao ya kupinga matokeo ya Uraisi ambao wao wanaamini kulingana na takwimu zao waliushinda Uraisi huo........hivyo hawatahudhuria hafla hiyo...........

  Wabunge wa Chadema pia walimkataa Mheshimiwa Pinda kwa kura zao zote 46 ikithibitisha ya kuwa hawatambui teuzi zozote zile zitakazofanywa na JK hadi pale mgogoro wa kura ya Uraisi utakapopatiwa ufumbuzi na Tume huru itakayoteuliwa na Bunge kuchunguza ni nani haswa alishinda kura hiyo.........wakati ushahidi wa matokeo ya kura hizo yaliyotangazwa na kuthibitishwa kwenye vituo yaonyesha tofauti kubwa na yale ambayo yaliyotangazwa na NEC
   
 2. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hiyo ndiyo dhamira ya kweli.
  Huwezi kumutambua mwizi!!! Ni sawa na kumukataa shetani lakini unakubali kazi zake

  hoja hapa ni kumukataa shetani na kazi zake!!
   
 3. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,496
  Likes Received: 2,742
  Trophy Points: 280

  Now we are talking the talking!!!
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  huu ndo mwanzo sasa MKATAE SHETANI NA KAZI ZAKE
   
 5. s

  seniorita JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Good move Chadema MP's!!!! We are with you, dont let down people who look up on you and have given you their trust
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,555
  Likes Received: 18,255
  Trophy Points: 280
  Rutashubanyuma, nadhani Chadema wanaweza wasimtambue rais, lakini haimfanyi rais asiwe rais, vivyo hivyo kumtaa Pinda pia hakumfanyi asiwe PM, ila kwa upande wa Pinda, watake wasitake, ni lazima wamtambue vinginevyo hawawezi kufanya chochote Bungeni, kwa vile PM ndiye mkuu wa shughuli za serikali bungeni, bila Pinda hakuna serikali, bila serikali, hao waunge wa Chadema, watakuwa wanafanya nini bungeni?.

  Wakiamua kesho wanaweza kutoka nje, kususia hotuba ya rais kulihutubia bunge, na akimaliza linaahirishwa mpaka January 25, ambapo Chadema lazima waingie Bungeni, na wakisusia, hatua kazi za kiutendaji zitafuata.
   
 7. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hope this is true. Kwa vile katiba imekaa kidikteta zaidi juu ya kuhoji matokeo ya rais basi hii move ni nzuri
   
 8. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #8
  Nov 17, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Nani kakwambia CHADEMA watasusia vikao vya bunge. Issue hapa ni kutuma ujumbe kwa JK kwamba ulichakachua. Kwa jinsi nilivyokufuatilia hapa JF wewe ni mwanasheria (Most likely junior) na kwa hiyo mawazo yako haya ni ya mtizamo wa kisheria na sahihi. But CHADEMA is a political party and have to handle issues politically! You probably do not know (or deliberately tend to ignore) the gimmicks and rules in this game
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  Nov 17, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Wasusie tu, mradi tu wasikose kuhudhuria vikao vitatu mfululizo, vinginevyo wataendelea kuwa wabunge
   
 10. Nipigie

  Nipigie Senior Member

  #10
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 121
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mmmmm, naona siasa bado hujazijua!!!!,
   
 11. T

  Think Tank JF-Expert Member

  #11
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 234
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kabisa!Haiwezekani umkatae mtoto eti sio wako,alafu hapohapo unapeleka matumizi?Kama wataenda!Makada wao,Wanachama wao,Mashabiki wao,Wakereketwa wao,Wafurukutwa wao!Sijui kama watawaelewa!
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Nov 17, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,555
  Likes Received: 18,255
  Trophy Points: 280
  Ngambo Ngali, nimeipenda hii, wasikose vikao vitatu mfulululizo, wakifanya hivi, itakuwa ni wabunge posho!, Chadema is more than that, wao ni wawakilishi wa wananchi, hivyo kutohudhuria vikao, itakuwa sio kuwatendea haki waliowachagua.
   
 13. T

  Tofty JF-Expert Member

  #13
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 6, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  good!
   
 14. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #14
  Nov 17, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mwanzo mzuri..ni kushinikiza mpaka hawa wezi wanyooshe mikono
   
 15. F

  Fishyfish JF-Expert Member

  #15
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 231
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Good good good.
   
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  Nov 17, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,097
  Trophy Points: 280
  Pasco hoja zako hazina mashiko kwa sababu ujumbe wa Chadema siyo kwa serikali haramu ya Jk tu bali ni kwa wapigakura ambao tuliacha shughuli zetu na kwenda kuwachagua viongozi tuwapendao.....................kwa hiyo huu ujumbe hautahusisha kutohudhuria vikao vya bunge la hasha................bali Bungeni kutawaka moto kudai uchaguzi huru na wa haki kwa kushinikiza kieleweke ni nini kilitokea kwa NEC kutotangaza matokeo waliyopewa kutoka vituoni? NEC itabidi ibebeshwe msalaba wa kutofuata sheria za uchaguzi na bila ya kuwawajibisha nchi hii itakuwa bora liende tu....................
   
 17. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #17
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Safi sana!!!!Aluta Continua!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! mpaka mizizi ya ufisadi/ushirikina/unajimu/uchawi nk ime.......!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Nov 17, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,555
  Likes Received: 18,255
  Trophy Points: 280
  Rutashubanyuma, nakubaliana na wewe kuhusu kupingana kwa hoja, na kwenye mjadala, hoja isiyo na mashiko hupanguliwa kwa hoja, sio kwa hisia au dhana, nimekukubalia kuwa kwa Chadema kutomtambua rais, hakumfanyi rais asiwe rais, kwa sheria yetu mbovu ya ajabu na kideteta ya hali ya juu, Tume ikishamtangaza mshindi, biashara ndio imeishia hapo, no more deals, negotioatis or discussions its over no matter what, hii ni sheria ya iitwayo 'the end justify the means', hata kama ulishinda kwa kuiba, hila, udhalimu, ua kwa mbinu zozote, maadam umeshinda wewe, its over. Hiki ndicho kilichotokea Kenya na Zimbabwe, hakiwezi kutokea kwetu kwa sababu Watanzania ni watu wapole, watu wa amani, watu watulivu, wavumilivu, wastahimilivu, hawapendi shari, kila wanachofanyiwa wao ni hewalla mzee, hivi ndivyo tulivyo na ndivyo tunavyoendelea kuwa.
   
 19. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #19
  Nov 17, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Huyo jamaa pasco sio kwamba hajui anachosema ila anataka kutuona na wengine kama hatujui taratibu za bunge.
   
 20. J

  JokaKuu Platinum Member

  #20
  Nov 17, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280
  Pasco,Rutashubanyuma,

  ..Chadema wanatakiwa kususia shughuli zote zile zinazoongozwa au zitakazomshirikisha Jakaya Kikwete.

  ..Hafla ya kuapishwa kwa Waziri Mkuu ni moja ya shughuli hizo.

  ..pia wanapaswa kususia hotuba ya Kikwete pale bungeni.

  ..ni vizuri Chadema waka-send a message kwamba kuna matatizo ktk tume yetu ya Uchaguzi na hawakuridhishwa na mwenendo mzima wa uchaguzi mwaka huu.

  ..siku ambayo Kikwete atakwenda bungeni kuhutubia watakuwepo Mabalozi na wageni mbalimbali muhimu, hivyo ni vizuri Chadema wakatuma ujumbe hapo hapo kwa marafiki zetu kwamba hali si shwari.

  ..nachukulia kitendo hicho kama juhudi za Chadema kushinikiza mabadiliko ktk sheria zetu za uchaguzi na utendaji wa tume ya uchaguzi kwa faida ya Watanzania wote.

  ..ni aibu kwa Tume ya Uchaguzi na serikali ya Chama cha Mapinduzi kutufikisha mahali ambapo chama kikuu cha Upinzani kinakataa kumtambua Raisi wa nchi na kususia shughuli anazoziongoza kutokana na mfumo mbovu wa uchaguzi.

  NB:

  ..kitendo cha Chadema hakimaanishi kwamba JK hatafanya shughuli zake kama Raisi. pia haimaanishi kwamba mataifa ya nje yatamsusia, Nigeria walifanya uchaguzi mchafu kuliko wa kwetu and still Ya'Ardu["baba go slow"] alitambuliwa jumuiya ya kimataifa.

  ..pamoja na hayo nakuhakikishia hakuna njia ya AMANI na KIUNGWANA ya kupinga uchaguzi na kutetea kuwepo kwa Tume huru zaidi ya hiki wanachokifanya Chadema.
   
Loading...