Matokeo ya Bunge la Afrika Mashariki: Saba washinda, Mnyaa safi, Wagombea wa CHADEMA waangukia pua

Duh umeme umekatika, Tanesco bwana .
Ila mbowe kwanini aliweka wagombea wawili? Hana mshauri au nae ashauriki?? Angeweka hata 3 kuzuga dooh
 
Nakubaliana na pia ninawaunga mkono wagombea wetu wawili yaani Wenje na Lau Masha, ila hili la kukiuka kwa makusudi kanuni na taratibu za Uchaguzi ni Uhuni. Sitaki kuamini kuwa hakukua na wagombea wengine mmoja au wawili na kufanya idadi yao wawe wanne au watatu kisha wakapigiwa kura. Huku ni kuonyesha jinsi gani wanabebana, au ni vyeo vya kupeana.
 
Mbowe kila uchaguzi ana kula pesa sasa safari hii pesa ya Wenje na Masha imeliwa
 
Mbowe alishakula pesa ya masha na WENJE

Mazoea ya rushwa yako kwenu. Huu unaoonyeshwa hapa ni ujinga wa ccm. Hivi katika ccm nani tunaweza kumlinganisha Wenje na Masha katika uwakilishi EALC? Upumbavu ulio wajaa ndio huo unao sababisha tunadharauliwa sana ndani ya jumuia kama watu wa hovyo.
 
Niko ninaangalia mkutano wa7 wa bunge-uchaguzi wa wabunge wa EALA..wabunge wa CHADEMA na CCM wanavutana kuhusu moja ya tatu (1/3)..

Nimeshangazwa na Halima Mdee akisema kua CCM wana nafasi ya wabunge 6 kwahiyo wao moja ya tatu itapatikana ila kwa CHADEMA na CUF moja ya tatu (1/3) haiwezi patikana kwa kua CUF wana nafasi ya mbunge mmoja (1) na CHADEMA wawili (2), imenibidi nikae chini nihakikishe kweli hakuna moja ya tatu (1/3) ya 1 na 2??

(1)/. 1 *1/3 =0.3 = 0
(2)/. 2 * 1/3 = 0.7 = 1
Kwahiyo kwa hesabu nyepesi nakubaliana na CUF kama wangeweka jinsia moja, ila CHADEMA walikua na nafasi ya kuweka jinsia mbili tofauti, nilipokosea niko tayari kusahihishwa.

Kwahiyo kwa mchanganuo hapo juu naomba mnijuze, Jee wabunge wetu hawajui wanachobishania au wanatufanyia makusudi??
 
Back
Top Bottom