Matokeo ya Arumeru: Salaam kwa Edward Ngoyai Lowassa!

Nilimshauri hakusikiliza!. Pia nitamshauri aachane na ndoto za urais 2015, Chadema inachukua nchi!.
Hongera km kwel ulimshaur lkn hakukuskia.Ila atajafka mahal akuskie tu kwa kuona vitendo vya wananch wenyewe kumtapika km walivyomtapika Mkwewe!
 
Anguko la CCM Arumeru Mashariki na Mgombea wake Sioi Sumari aka Mkwe wa EL ni teke la mwisho la fisadi Edward N. Lowassa. Kwasasa sioni muujiza wowote wa kumnusuri EL hasa baa ya kulazimisha kupanda jukwaani kumuombea mkwewe kura! Pesa alizotumia kushinikiza na kununua ushindi, HAKIKA IMEDHIHIRISHA PESA SI KILA KITU.....

To make it short jamaa matokeo ya Arumeru yamemwachia majeraha makubwa sana kisiasa na hii itawapa nguvu sana maadui zake kuwa kumbe hala lolote zaidi ya pesa na michezo michafu.
 
Hongera sana CDM kwa ushindi wa arumeru, udiwani mbeya na mwanza. Kwa mtizamo wangu juu ya hii thread uko tofauti na wanaofikiri kuwa EL ndiyo sababu ya kushindwa kwa Ccm.
Sasa hivi watz wameuchoka utawala wa ccm ambao haujakidhi matakwa yao kwa muda mrefu. Hali ya maisha imekuwa mbaya siku hadi siku, na hakuna dalili zozote zinazoonesha yatakuwa bora siku za karibunim
Kibaya zaidi ni kuwa walioaminiwa kupewa dhamana ya raslimali zetu wamekuwa wakitoa majibu mepesi kwa maswali magumu ya namna ya kumfanya mTZ ajivunie utaifa wake na kufaidi raslimali zao.
Wanye nchi wameamka sasa, wanachotaka kuona ni changes na si kulalamika tena ndiyo maana kila nafasi sana ccm out! Watawala nao, (ccm) bado wana imani kuwa dola inaweza kuwasaidia ( polisi, usalama wa taifa nk) lakini nguvu ya umma ni kiboko! Ona yaliyotokea arumeru, watu wote influential walikuwa kule lakini nguvu ya umma ikawabwaga!
Hii ni salamu tosha kuwa 2015 wajiandae kuwa chama cha upinzani
 
Nimetopewa na furaha, yaani hadi kuchelewa kulala, itoshetu kusema USHINDI huu iwe chachu ya kuendeleza mapambano, maadam sasa tunahakika ya uungwaji mkono hadi ndani ya magamba wenyewe. Kazi inazidi kuwarahisi.

Hongera wote waliovuja jasho la haki katika mpambano huu. Mungu atawalipa kwakadili ya kipimo chake.

 
Hapana; hii ni salamu kwa CCM nzima. Hata hao wengine wameshindwa vibaya sana huko Kirumba, Kiwira na Songea. Msiwape moyo.

Nakubaliana na wewe Mkuu Kitila, lakini kwa kusema anguko la EL ndio anguka la CCM, maana yeye ndiye baba lao, kati ya wote yeye ana nguvu kubwa ndani ya CCM kuliko wengine na wengine wanadandia mambo kama wanaodandia hoja ya mapambano ya ufisadi lakini wanakula nao sahani moja kama Sendeka na wenzake waliokuwa wanahaha Arumeru. Ni salam kwa mafisadi na kwa sisi tusio na vyama tunasema popote walipo hata wakiwa upinzani, mafisadi wajue watamulikwa na wananchi wa sasa wako macho sana.
 
Hapo vp?hapo sawaaaa!hapo vp?hapo sawaaaa!hapo vp?sawaaa?sioi wangu vp?huyo sio !!mvi zangu vp?nazo sio! aligeuka Prof.J
 
Ni kweli Edfward Lowasa amekuwa mtu wa kufanya mambo ya aibu! Daima amekuwa akiongoza kundi lenye tamaa ya mali na madaraka,hata bila aibu kupata kamisheni ya ten pasenti kutoka kwa masikini wa Tanzania.Mtu huyu ni hatari sana wana JF! Tizama hata makapuni ya simu za mkononi hayali kodi ya ongezeko la thamani [VAT] kutokana na ukweli kwamba mtu huyu ana share kubwa kwenye hayo makapuni.Anataka kuwa Rais ili tukianza kuchimba mafuta achangamkie mapato.Jamani Watanzaia tukae chonjo-------------!!!?
 
Wengine tulishasema EL akigombea urais labda Monduli atashinda but sio kwengineko. Kauli yangu nimeishawahi kuitoa miaka mingi nyuma na narudia tena EL apumzike kwani watanzania isipokuwa Monduli wana hasira naye sana!!! Popote atakapojaribu CCM watashindwa tu. Hivyo Arumeru nilikuwa najua labda CDM wasitake hicho kiti but ushindi uko wazi kabisa. Pole sana mzee wetu soma alama za nyakati kama mwenzio RA yuko zake Switzerland anakula bata......

CCM wakati wa kuondoka madarakani unawadia kwani mshalewa na madaraka. Wengine tulishayaona miaka mingi tukajikalia pembeni na kuwaombea kila la kheri. Chadema itashinda sio kwakuwa ina sera nzuri bali watu wanahasira na CCM isiyokuwa inakubali kusikia maoni ya wananchi.
 
Jana katika mkutano wa Shukurani Leganga, laiti mngalikuwepo watu wamechoka na maisha na matusi ya baadhi ya wana CCM na uchu wao wa madaraka ambao wakipata hawakumbuki wananchi waliowapigia kura. Lakini hii ni LAANA YA MAREHEMU BABA WA TAIFA INAWATAFUNA.
 
MUNGU ni zaidi ya pesa..ukuta wa Jeriko zama za taifa la MUNGU Israel uliangushwa kwa kuimba na kuuzunguka mara saba siku ya saba.Natamani kutoa machozi wakuu,MUNGU tunakushukuru kwa kuwa upande wetu.Mashetani hawa CCM wameshindwa kwa uwezo wako.Thanx God!! Okoa Taifa hili.

Only83
Post yako ni moja ya post nzuri...... ambazo nimewahi kuzisoma hapa JF....MUNGU akubariki Mkulu....maneno yako YAMENICHUKUA SANA...Asante
 
Hakuna kutafuta mchawi hapa, CCM wamechokwa kwa sera zao mbovu za kuuza nchi, wakati wa mabadiliko umefika, mengineo ni uzushi tu.
 
Hakusoma halama za nyakati,hakupaswa kabisa kusimama jukwaani,angefanya kapmeni za chinichini,amekuwa unpopular ghafla all over Tanzania
 
Asiyekubali kushindwa si mshindani. Mbona nyie CHADEMA hAMCHOKI MKISHINDWA?????????? bASI WAKATI ULE WA IGUNGA SLAA, MBOWE WANGEJIUZULU. Acheni umbea. 2015 tunamtaka mtu mwenye maamuzi na mchapakazi kama LOWASSA.
 
Hapana; hii ni salamu kwa CCM nzima. Hata hao wengine wameshindwa vibaya sana huko Kirumba, Kiwira na Songea. Msiwape moyo.

Ukisema hizi ni salamu kwa ccm nzima you are assuming kuwa chama hiki ni homogenous ambapo ukweli ni kwamba hiki chama kiko vipande vipande; Kipande kimoja cha kundi la mafisadi [ Lowassa & co] na kipande kingine ni hao wanaojidai wanapinga ufisadi[ Sitta &co]. Kundi la sitta limefurahi CCM kushindwa Arumeru kwani kunalipunguzia nguvu genge la Lowassa!Hata kule Mwanza pia Kundi la Masha linaumoja na kundi la Lowassa.The whole party is split between these two main factions.
 
Nimeona siredi moja humu kwamba Chief fisadi anatafakari uwezekano wa kutimkia CDM. Kama ni kweli na kama CDM wakimkubali Lowasa (fisadi mkuu) ndiyo utakuwa mwisho wao katika siasa za Tz kabisaa. Mimi binafsi nitaikabidhi kadi yangu ya CDM chama chochote hata kama ni PPT Maendeleo.

Wasimkubali Lowassa mwizi,CDM wakifanya hivyo mimi natimkia Sauti ya Uma (SAU)
 
Naungana na Jasusi. tusimshambulie EL. Kwa maoni yangu MCC nzima watu wameichoka wanahitaji mabadiliko ya kweli. Hata yenyewe ikijirekebisha ikawa na nia ya that ya kutumikia wananchi watu wataipa kula.
Mpamba KK
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom