Matokeo kidato cha nne 2009

Baada ya kukubali shule moja, sasa imegoma:confused:....ngoja nipumzike nisubilie mechi ya Chelsea na Arsenal......

Hata mimi nahangaika matokeo hafunguki, sijui wenzetu mmefanikiwa kufungua? Na kama mmefanikiwa tuelekezeni. Maana hayafunguki kabisa.
 
wadau ebu nipeni msaada, nimejaribu kutumia broswers zote lakini nimeshindwa kufungua matokeo ya kidato cha nne, msaasa tutani
Samora, Mi nadhani subiri kesho maana naona servers za hawa jamaa zimekuwa overloaded.

Jana usiku nilikuwa napata vizuri matokeo kutokea www.moe.go.tz lakini baadaye nadhani walizima server yao maana haipatikani kabisa leo.

Hiyo ya necta ndio usiseme ni shida tupu. Haileti lolote la maana.

Naona Pale kwa Yusuf kwenye internet cafe kwenye mji unakoishi vijana wengi wamejaa wakichukua matokeo yao nadhani wao walifanya kazi ya kuya download na ku save.

Jaribu pale kama una haraka nayo.
 
Mbona haifunguki? Kama umefanikiwa hebu tutumie link ya page2 yenye list ya shule zote nchini.
Mkuu kwani results zilizo http://www.necta.go.tz

Na http://www.moe.go.tz/NectaResults/olevel.htm zina utofauti?

Mnahitaji tufanye kama tulivyofanya mwaka jana? Hawa jamaa tuliwambia tuwawekee results hapa kwa muda wakachomoa; wakiweka matokeo huwa siku ya kwanza na ya pili server ina-crash several times. Na hapo unaweza kukuta hits hazizidi laki 5
 
Wapendwa mie nimeshafungua hiyo website ya necta na nimeshapata matokeo ya wadogo zangu cha msingi kuwa na centre number na namba ya mtoto alafu unasearch unapata matokeo.
 
Mbona yananiletea ya A level!!!!???
Oh,

Pole kwanza; link niliyoweka kwanza ilikuwa na makosa, nimerekebisha hilo.

Pili, usitumie link ya NECTA katika nilizokupa, NECTA server yako iko chini kabisa, not accessible kwa sasa. Tumia link ya Wizara ya Elimu. www.moe.go.tz

Nimeuliza kama tuyahamishie JF yote kama yalivyo hamkujibu; wacha nikale kuku mie....
 
Sioni kwa nini hampati au hamfuati maelekeo sasa hivi nimepata matokeo ya mtoto mwingine ameomba nimtolee, mbona rahisi tu kwenye website ya NECTA weka center number na namba ya manafunzi aliyofanyia mtihani basi.
 
nakubaliana na wewe 100% yaweke yote hapa----anaipinga apinge haraka, jamani tangia jana tunahaha.....weka mkuu
 
Sioni kwa nini hampati au hamfuati maelekeo sasa hivi nimepata matokeo ya mtoto mwingine ameomba nimtolee, mbona rahisi tu kwenye website ya NECTA weka center number na namba ya manafunzi aliyofanyia mtihani basi.
Lily,

Website ya NECTA inachukua miezi (loading time) ndo maana wengi unaona wanashindwa. Wengine ambao tuna internet yenye speed kubwa tunaweza tusione hilo lakini mwenye kutumia internet ya kawaida inamkera SANA.
 
Back
Top Bottom