Poti,
Pamoja na kukubali "ushauri" wako wa ku-quote yote lakini siwezi kuzungumzia neno kwa neno kama ulivyojadili. Mimi nimejaribu kuzungumzia hoja mojawapo uliyoitoa na ambayo umeirudia tena hapa. Yaani ni kusema kwamba tuendelee tu kutokuwa na tume huru ya uchaguzi?kama kweli umesoma na unapenda maendeleo ya demokrasia huwezi kamwe kutetea kuendelea/kushikilia tume ya uchaguzi iliyo biased, tume isiyo huru kabisa, tume inayokitumikia ccm na kuhakikisha kuwa hakishindwi.
ushauri wa kususia kazi nao ni low(samahani kwa hilo) kwa kuwa unategemea hao wafanyakazi watajimudu vipi?unadhani wapenda mageuzi wote ni wafanyakazi wa serikali ya ccm kama unavyodhani?je ni wapi hiyo style ya kususia kazi iliwahi kufanyika na ikafanikiwa?
halafu poti wangu usipende ku-generalise mambo, mimi kuwa na mawazo tofauti na yako haimaanishi kuwa mimi ni mchadema kama wewe ulivyo m-ccm.Na kama huu mfumo dhalimu wa kuwa na tume ya uchaguzi isiyo huru unanufaika nao, basi waache wale wasionufaika nao waseme.Mimi nitakuunga mkono na mguu ikiwa kutakuwa na jukwaa lililo sawa kwa vyama vyote kuendesha siasa na mwisho wa yote kuwe na mwamuzi(tume ya uchaguzi iliyo huru) asiye na mahaba na chama chochote.
Mkuu vipi tena
Mimi nimewashauri hivyo baada ya wao wakereketwa wa chama chenu kupropose kumwaga damu,ndio nikaonelea ni bora kususia kazi maana wataendelea kuishi hata kwa mbinde kuliko kumwaga damu zao ,logic hiyo ni ngumu kueleweka mkuu.? Kuiona hiyo ni low na ukaisapoti ile nyingine itakuwa sio low tuu bali..........
Harafu mbona walia nani kaanza kugenalize kuwa mimi ni ccm ? hii ni tabia ya wafuasi wa chadema ,ukiona mtu anakuita ccm ama fisadi wewe hitimisha tu kuwa huyu ni chadema.
Poti mimi sina chama chochote ila sina hakika na wewe kuwa si mfuasi wa chadema, mawazo yangu ndiyo chama changu sifungamani na upande wowote ,tatizo kubwa lililoko hapa ni lile la mtazamo wa Ki-Bush Bush eti ya kwamba ili uwe great thinker ama mtu asiyeshusha plofile lake ama anayetowa point za uhakika lazima uisapoti chadema kinyume chake wewe fisadi ama unatowa low .
Hili ni tatizo kubwa kwa chama chenu ,tena linaenda mbali sana hata ktk hadi uongonzi wenu huko juu lakuona yanayofanywa na ninyi ni sahihi tu hivyo kwa vyovyote vile mtaungwa mkono tu na wengine hakuna kitu na kinyume chake kwa vyovyote vile mtakuwa mumeibiwa kura ama mmeonewa.
Mkuu vipi tena
Mimi nimewashauri hivyo baada ya wao wakereketwa wa chama chenu kupropose kumwaga damu,ndio nikaonelea ni bora kususia kazi maana wataendelea kuishi hata kwa mbinde kuliko kumwaga damu zao ,logic hiyo ni ngumu kueleweka mkuu.? Kuiona hiyo ni low na ukaisapoti ile nyingine itakuwa sio low tuu bali..........
Harafu mbona walia nani kaanza kugenalize kuwa mimi ni ccm ? hii ni tabia ya wafuasi wa chadema ,ukiona mtu anakuita ccm ama fisadi wewe hitimisha tu kuwa huyu ni chadema.
Poti mimi sina chama chochote ila sina hakika na wewe kuwa si mfuasi wa chadema, mawazo yangu ndiyo chama changu sifungamani na upande wowote ,tatizo kubwa lililoko hapa ni lile la mtazamo wa Ki-Bush Bush eti ya kwamba ili uwe great thinker ama mtu asiyeshusha plofile lake ama anayetowa point za uhakika lazima uisapoti chadema kinyume chake wewe fisadi ama unatowa low .
Hili ni tatizo kubwa kwa chama chenu ,tena linaenda mbali sana hata ktk hadi uongonzi wenu huko juu lakuona yanayofanywa na ninyi ni sahihi tu hivyo kwa vyovyote vile mtaungwa mkono tu na wengine hakuna kitu na kinyume chake kwa vyovyote vile mtakuwa mumeibiwa kura ama mmeonewa.
Sio lazima kuwe na tume huru wala nini wafanykazi wote wakiacha kazi na mtanzania yoyote akakataa kazi mpaka ccm itakapong'oka mbona ni tiba tena ya week tu
Ndugu yangu hadi hapo, kwakweli umechangia very low.
Kama unadai kwamba wazee wako vijijini walikutuma ukasome upate elimu kisha uje kuwasaidia kuondokana na hali duni, na hapo juu umeonyesha kuwa umesoma kama ulivyotumwa na wazee wako.
Lakini ghafla unapogeuka na kutoa hoja dhaifu kama hii, nabaki kuwaonea huruma hao wazee wako huko kijijini. Watakuwa wamekula hasara kama hali yenyewe ndio hii.Tangu mwanzo nilikuwa nasoma post zako naona kama una kitu cha maana unataka tukifahamu toka kwako, pamoja na mapenzi yako ya dhati kwa ccm, lakini kwa ushauri huu, umejishusha mno. Pole sana yego mwamba.
hata mtu mwenye elimu ndogo tu ya kujua kusoma na kuandika hahitaji ufafunuzi kama huu unaoutoa hapa.Kwasababu kwa akili yako mtu asiyekubaliana na madudu yanayofanywa na tume ya uchaguzi unajua kuwa ni chadema hapo sina la kukusaidia kwasababu we si msomi?
sisi wengine hapa hatuko kuisupport chadema wala ccm wala cuf wala tlp, bali tunasupport demokrasia ya kweli ili iweze kushamiri nchini mwetu.
hata kama ukisema wewe sio ccm mabandiko yako yanadhihirisha hivyo, ingawa si wana ccm wote wanaokubaliana na faulo zinazaochezwa na chama chao pamoja na tume ya uchaguzi, na katika hao wewe si mmoja wao.Ngoja tu nikuache uendelee kusherekea kwa ushindi wa tsunami mlioupata biharamulo.
Wewe ndugu una akili sana ..... yaani umegundua kuwa umwagaji damu ni kitu kibaya sana kabla ya wana chadema wote hawajagundua hili? Inabidi upewe nafasi ya ushauri mkuu hapa JF.
Kwani ni makosa kuwa mwana ccm? unaniangusha sasa!
Nilitegemea kuwa elimu kubwa uliyoipata ingekusaidia kufanya uamuzi wa kuwa na msimamo kwenye maisha.
Diagnosis tayari imeshatolewa ...... mhh ..... nimenyanyua mikono
wewe poiti zako nawe zinahitaji kuombewa si bure teh teh teh, msimamo upi unaongelea?
Mkuu angalia hapo palipokandamizwa ,hii ni post yako ya kwanza kabisa kati yako na yangu.
Tatizo mnapenda sana huruma ili kupata sapoti ,mtajitahidi kwa kila hali kujenga point zenu kwa kumuhusisha mhusika ama na ccm ama na ufisadi HAKIKA hili ni tatizo kwenu na limekuwa sugu.
Baraka Obama angefuata ushauri wako (wa kuongelea sera tu bila kuhusisha ubovu wa chama cha republican) angepata kura nyingi zaidi kuliko huo ushindi wa kiduchu aliopata.
Mkuu, my hat is off!
teh teh teh teh
Kweli kazi ipo, kwa hiyo kwa mtu yeyote aliyekuwa aki argue na Obama lazima alikuwa anataja Republican kujenga hoja yake teh teh teh teh teh teh .Huruma tupuu
I am royal to CHADEMA.
Still supporting CHADEMA
Awali:
Ingawa matokeo rasmi hayajatangazwa, CHADEMA inaelekea wameweza kuwashinda kwa karibu kabisa CCM kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Biharamulo hii leo.
Mpaka zinapatikana hesabu za mwishomwisho kukiwa bado kituo kimoja cha Nyabugombe B chenye wapiga kura 394 CHADEMA ilikuwa ikiongoza kwa 50.6% huku CCM ikiifuatia kwa karibu ikiwa na asilimia 48.8% ya kura zote na TLP ikiwa imejinyakulia 0.55% ya kura zote.
Matokeo yanatarajiwa kutangazwa rasmi punde
Lakini matokeo ambayo yamejumlishwa mpaka dakika hii ni haya:
CHADEMA: 17,313
CCM: 16,682
TLP: 187
Turnout ilikuwa 39.24% (incredible!)
========================================
UPDATE 1...
Matokeo ya kituo kwa kituo tuliyoyapata toka kwa mwakilishi wa JF jimboni humo yameambatanishwa hapa chini kama attachment:
========================================
UPDATE 2.
Tume ya uchaguzi imesema hivi:
CCM: 17,561 = 51%
CHADEMA: 16,670 = 48.4%
CHADEMA wameyakataa matokeo kwani wanadai matokeo ya kata 3 yamegeuzwa tofauti na walivyosaini wasimamizi wa matokeo na yalivyohesabika vituoni!
========================================
Update 3.
Tume ya Uchaguzi imemtangaza mgombea wa CCM kama mshindi kwa kura zinazoonyeshwa kwenye Update ya awali ingawa CHADEMA wameyakataa matokeo ya vituo 9 kati ya vituo 237 vya uchaguzi!
========================================
Invisible,
Kwa kutambua kuwa hii forum si ya kushabikia chama chochote cha kisiasa au kundi fulani, basi iko haja ya kutolea maelezo vyanzo vya habari vya takwimu ulizozichapisha hapo juu. Kitendo cha kuleta habari nyeti kama za matokeo ya uchaguzi huku zikuwa na upotoshaji wa hali ya juu nadhani ni kitendo cha kukiangalia kwa makini kiifanye forum hii kuwa ni ya kupigia debe makundi fulani ya kisiasa.
Ninasema hivyo kwani taarifa uliyoichapa hapo juu ina makosa makubwa ambayo unaweza kuona kuwa yametokana na kutokuwa makini kwa mpokea taarifa au mpokea taarifa alikuwa na agenda nyingine iliyojificha. Nia yangu si kukurushia lawama, bali nikuondoa na kupiga vita dhana zozote zile za upotoshaji wa jambo.
Kwa mfano kimahesabu haiwezekani hata siku moja katika mchakato wa kuhesabu kura namba ikahesabika kutoka kubwa kwenda ndogo, ni wazi kabisa huenda chanzo chako kili-doctor / manipulate figures hizo kwa nia ya kutaka kuleta mkanganyiko hapa jamvini. Kwa jinsi matokeo ya kura zilizopigwa pale Biharamulo, vyama vya CCM na CHADEMA vilikuwa na nafasi zinazokaribiana kabisa katika kutwaa ushindi wa kiti kile. Kushinda kwa CCM haiwezekani ionekane kuwa ni kitu cha ajabu au kutondwa kwa CHADEMA ionekana kuwa ni uonevu. CHADEMA imekwenda Biharamulo huku iktambua wazi kuwa CCM tayari inarekodi nzuri ya kupanga mikakati ya ushindi katika majimbo mawili ya Mbeya (V) na Busanda, kwa maana hiyo CCM ilikuwa inategemewa zaidi kushinda Biharamulo kuliko hata CHADEMA. Kitu ambacho CHADEMA watajivunia kwa sasa pale Biharamulo ni kuweza kupata kura nyingi kuliko walizozipata 2005 lakini si kulalamikia ushindi wa CCM.
Namalizia kwa kusema kuwa hizi habari za matumizi ya wananchi bila ya kujali itikadi ni vyema zikawa ni zile ambazo zimethibitishwa na mamlaka halali au la basi hii ingekuwa imetolewa na CHADEMA kama malalamiko halali kwa Tume ya Uchaguzi wakipinga matokeo.