Black Jesus
JF-Expert Member
- Mar 7, 2008
- 256
- 10
Ingawa matokeo rasmi hayajatangazwa, CHADEMA wameweza kuwashinda kwa karibu kabisa CCM kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Biharamulo hii leo.
Mpaka zinapatikana hesabu za mwishomwisho kukiwa bado kituo kimoja cha Nyabugombe B chenye wapiga kura 394 CHADEMA ilikuwa ikiongoza kwa 50.6% huku CCM ikiifuatia kwa karibu ikiwa na asilimia 48.8% ya kura zote na TLP ikiwa imejinyakulia 0.55% ya kura zote.
Matokeo yanatarajiwa kutangazwa rasmi punde
Lakini matokeo ambayo yamejumlishwa mpaka dakika hii ni haya:
CHADEMA: 17,313
CCM: 16,6682
TLP: 187
Turnout ilikuwa 39.24% (incredible!)
Hahaha,Hicho kituo kimoja ndicho kitaipatia CCM ushindi wacha tusubiri filimbi ya mwisho.
Nafikiri kutokana na ushindi huu wa CHADEMA na anguko kwa TLP, huu ni muda muafaka kwa Bw. Lyatonga Mrema kupumzika na kuwaachia vijana waendeleze TLP. Kama bado anahitaji kuendelea na siasa ni bora arudi SISIEMU alikotokea.
Mrema hata sasa hivi akiamua kugombea ukatibu kata kwa chama chake hawezi kupata kura za kumuwezesha kushinda huo uchaguzi.
Mrema, Kiraracha yakungojea, pumzika sasa.
Mkandara
Mambo ya wapinzani kwa kweli inabidi tuwe tunaongea kwa tahadhari kubwa sana. Mimi ndiyo maana nimeamua nifunge safari nije nione mwenyewe. kweli wapinzani wakiungana kuna nguvu kidogo itaongezeka lakini ukiwasikia maneno yao hutataka waungane tena hata kama ni kushinda uchaguzi kwani utajua kuwa wana malengo tofauti kabisa. nina baadhi ya crip za mrema itabidi niziweke hewani nikifika sehemu yenye speed kubwa ili mjionee wenyewe mliokuwa mnataka eti chadema wajiunge na na chama kama TLP
Hahaha,
Sawa Yesu Mweusi, jaribu kujumlisha uone CCM itafikia wapi!
Hongera sana CHADEMA kwa kuwagaraza CCM huko Birahamulo. Inaelekea kila jimbo wapiga kura wachache sana wanatumia haki yao, je hii ni kwanini?
Hili jambo la watu kuwa wachache kwenye hizi chaguzi limenitatanisha sana siku nyingi lakini pamoja na kuwa kwenye kumi na nane nimeshindwa kujua. swala la kununua shahada naona inakuwa ngumu kuliweka hapa kwani hata katika maeneo ambayo chadema wamefanya vizuri kwa mfano kituo cha Bisebo utaona kwenye kituo c wapiga kura waliotarajiwa ni 340 lakini walio jitokeza ni 192 na chadema wamepata 160 na ccm 32 na kwa mtizamo wangu hawa jamaa sizani kama wangeuza shahada.
nimejaribu kuwadadisi wenyeji nao hawajui kwa kweli na sababu wanazo hisi ni, vifo, movement za watu, watu kuona aibu kuwa hawajui kuandika na kusoma, uchaguzi mkuu kuwa na vinyang'anyiro vingi (uraisi,ubunge na udiwani) na baadhi ya watu bado hawaamini mfumo wetu ni kuwa ni huru hivyo kuhisi kuwa kura zao hazina maana
Mpambanaji hakati tamaa...nafikiri nitapiga kura miaka yote kwa mtu na chama ambacho naona ni afadhali katika zilizopo??Hata mimi siwezi kupoteza mda wangu kupiga kura kama unaamini wagomea wote ni feki,hiyo ndiyo sababu kuu.
Mfano 2010 kwanini nijisumbue kupiga kura kwa mgombea urais kama safu itakuwa hivi,JK,Mbowe,Mrema,Lipumba
Mpambanaji hakati tamaa...nafikiri nitapiga kura miaka yote kwa mtu na chama ambacho naona ni afadhali katika zilizopo??
Lazima kutakuwa na better evil in all evil (nakushauri piga kura mpaka kieleweka na tuhamasishe wengine wapige kura...that is the way we choose our future. kati ya JK,Mbowe, Lipumba, Mrema kuna better evil..go for that...
Uamuzi ni wako mwenyewe lakini mjahidini yeyote kama mimi hata kula nguruwe hata aje nani?? ndugu...lakini sijaona uhusiano wake na siasa....ungejua hasara ya kula nguruwe usingejisifia ujinga...pole sana kula kilo kumi kwa siku kama wewe bingwa! ...then utaandika huo upuuzi wako hapa!!!Aisi kwa safu hiyo ni vigumu kunihamasisha ,maana nikama unanihamasisha ili ni isaliti akili.
Hii ni sawa na mimi , mfano wewe ni mjahidina nikuhamasishe ule kama nyama ka nguruwe maana kanguruwe kenyewe kalikuwa kadogoooo tuuuu ,hivyo unajisi wake ni tofaute na lile libabayao la nguruwe.teh teh teh
Uamuzi ni wako mwenyewe lakini mjahidini yeyote kama mimi hata kula nguruwe hata aje nani?? ndugu...lakini sijaona uhusiano wake na siasa....ungejua hasara ya kula nguruwe usingejisifia ujinga...pole sana kula kilo kumi kwa siku kama wewe bingwa! ...then utaandika huo upuuzi wako hapa!!!
Uamuzi ni wako mwenyewe lakini mjahidini yeyote kama mimi hata kula nguruwe hata aje nani?? ndugu...lakini sijaona uhusiano wake na siasa....ungejua hasara ya kula nguruwe usingejisifia ujinga...pole sana kula kilo kumi kwa siku kama wewe bingwa! ...then utaandika huo upuuzi wako hapa!!!
InakuwajeTumaini anatumia lugha za dharau kwa mwana JF mwenzake?Please moderator nipe mwongozo kwa kauli kama hizi zikiingizwa hapa JF, huwa unachukuliwa uamuzi gani?Anatakiwa ama afute kauli yake au akae chini?
Kumbukeni JF haina dini,anayekula paka ni juu yake na kizazi chake,anayekula bundi ni uamuzi wake,na anayesali hata kwenye mapango ni haki yake.Hamna mpumbavu kwenye jamii iliyostaharabika kama hii,na KAULI hii imenishtua!
Nawasilisha hoja na JF mnilinde!
Nasikia TZ na Kenya kwa kubadirisha matokeo ya uchaguzi wamequarify kwa degree ya juu sana.
Kitu ambacho kilimpelekea Rais wa IRAN kabla ya uchaguzi wake kuja TZ na Kenya kuuchukuwa huo uzoefu na kwenda kui implementi nchi kwake. teh teh teh teh
Sasa mzee paroko... ulitaka tukunyamazie ili iweje?, udini unauona tu pale Muislam anapo kujibu... lol!Udini kijana unakutafuna, hapa hujatoa maoni ya maana kazi yako unatafuta tu pale uislamu ulipoguswa, lol! After all mimi nilikuwa na-quote statement ya mtu mwingine, sasa shehe mbona waniandama mie ati!