Matiti ya Bandia Yaokoa Maisha Yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matiti ya Bandia Yaokoa Maisha Yake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 4, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,770
  Likes Received: 4,912
  Trophy Points: 280


  [​IMG]
  Matiti ya bandia kama haya ya silikoni yaliokoa maisha ya Coranza Monday, March 01, 2010 3:37 AM
  Mwanamke wa nchini Marekani ambaye alitandikwa risasi ya kifua baada ya kujifanya amefariki, alinusurika maisha yake kutokana na matiti ya bandia aliyoyapandikiza kwa operesheni miaka kadhaa iliyopita. Lydia Carranza alikuwa kazini kwake kwenye zahanati ya meno mjini California wakati mume wa mfanyakazi mwenzake alipovamia kwenye zahanati hiyo.

  Mwanaume huyo alikuwa amebeba bunduki na alifika kwenye zahanati hiyo akiwa na lengo moja tu la kumuua mkewe ambaye alikuwa akidai talaka.

  Kaka wa mke wa mwanaume huyo ambaye naye anafanya kazi kwenye zahanati hiyo aliingilia kati akitaka kusuluhisha mambo lakini alitandikwa risasi ya tumbo na mwanaume huyo.

  Baada ya hapo mwanaume huyo alimgeukia mkewe na kuanza kumpiga risasi kadhaa mpaka alipohakikisha amemuua.

  Ndipo sasa zamu ilipomuangukia Coranza na wafanyakazi wenzake. Coranza alitandikwa risasi kwenye mkono wake wa kulia, alipojifanya amefariki mwanaume huyo alimsogelea na kumtandika risasi nyingine ya kifua.

  Coranza ambaye ni mama wa watoto watatu alinusurika maisha yake kutokana na matiti ya bandia ya silicone aliyojipandikiza miaka kadhaa iliyopita kuhimili kishindo kikubwa cha risasi hiyo.

  Miaka michache iliyopita Coranza alifanya operesheni ya kuongeza ukubwa wa matiti yake kutoka saizi B hadi saizi D.

  "Ana bahati sana, risasi ilibakia milimita chache sana kuufikia moyo wake na ogani zake muhimu, kama angekuwa hajafanya operesheni ya kuongeza matiti, tusingekuwa tunaongea hivi sasa", alisema Dr. Ashkan Ghavami wa zahanati hiyo alipokuwa akiongea na gazeti la Los Angeles Times.

  Jaime Paredes, mwanaume aliyefanya mashambulizi hayo ya risasi alikamatwa na anasubiria kupandishwa kizimbani akikabiliwa na mashtaka mbali mbali yakiwemo mashtaka ya mauaji ya mkewe.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=4155806&&Cat=2
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...