Matibabu ya maana na ya haraka ni kwa madkatari wenyewe tu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matibabu ya maana na ya haraka ni kwa madkatari wenyewe tu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Avanti, Jun 29, 2012.

 1. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Picha gazeti la Mwananchi leo na hata taarifa nyingi ndani ya JF na kwingineko zinaonesha Muhimbili sasa wanamtibu Ulimboka tu. Machine inayosaidia kuangalia kila kitu kuhusu afya ya binadamu imefungwa kwake ikianzia kupima mapigo ya moyo na kadhalika na viungo vyote vya mwili. Ni adimu sana raia mwingine asiye Dokta, hata awe ameumia kiasi gani, iwe kwa ajali ama vinginevyo kufungiwa machine kama hiyo. Ilinichukua siku 6 kwa mama yangu kuchunguzwa tatizo lake la kuumia nyonga baada ya kudondoka, tulipomleta toka mkoani walipoturefer Muhimbili. Kwa kusaidiwa na wanakijiji wenzangu tulikodi gari ili kuweza kuwahi matibabu Muhimbili, lakini baada ya kufika tulisubirishwa siku 6 zingine na mpaka anapata huduma tulishakata tamaa tukijua atatuacha hasa tokana na uchovu ambao tayari alikuwa nao, kumbuka hapo hata mgomo haukuwepo. Pamoja na kuwa yawezekana madaktari wanadai haki lakini ubinadamu nafikiri wanadhani upo kwa wao wenyewe tu, wanatibiana bila masharti na pia wanatumia vifaa vya Serikali hiyo hiyo wanayoilalamikia. To hell you doctors and your cockroach government all the same!
   
 2. happiness win

  happiness win JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,478
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Hata hao Madaktari sio wasafi, wana makosa mengi tu. Kwa ujumla kila mahali kumeoza. Madaktari wanapaswa kusitisha mgomo ili kuokoa maisha ya wanyonge wengine.

  Huu si muda wa kuwatesa wanyonge, hakuna aliye na haki na asiyekuwa na haki. Watanzania wote tunapaswa kubadilika na kujipanga kwa manufaa ya wote. Mgomo wa Madaktari unachochea roho ya chuki kwa wale wanaoumia bila hatia.
   
 3. Dr. Wansegamila

  Dr. Wansegamila JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 1,233
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Sio kila mgonjwa anatakiwa awekewe hiyo mashine unayosema ulimboka amewekewa, kuna indications huyu ulimboka amepata multiple injuries so vitals zake zinahitaji kuwa monitored 24/7. Kama nimekuelewa vizuri mama yako alikuwa ameumia 'nyonga'(hip dislocation),hiyo sio mojawapo ya indications za kuwekewa hiyo mashine. Kuhusu shida ulizopata katika kupata matibabu ya mama,pole sana lakini hapo madokta hawana kosa,ni kutokana na msongamano wa wagonjwa na upungufu wa watoaji huduma,hata sisi madaktari hatufurahishwi na hali hiyo,na ni mojawapo ya sababu za mgomo,ulitakiwa uilalamikie serikali yako kwa ubovu wa huduma za afya,siyo madaktari.
   
 4. bishoke

  bishoke JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 276
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chonde chonde madaktari na serikali 'mchezo wenu ni mauti yetu',
   
 5. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,551
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Kama hataelewa hili jibu Avanti, basi ana matatizo... hivi kweli ni sawa na kusema kila mgonjwa anaye kwenda muhimbili basi apewe ARV.. ungekubali Avanti mama yako apewe ARV, au aongezewe damu kwa tatizo la hip dislocation?
   
 6. Micro E coli

  Micro E coli JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kwa hiyo hutaki au?
   
 7. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,567
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Naona hapa kuna ndege wa aina moja tu!

  NAPITA............
   
 8. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  save 1 doc to save 25000 patients
   
 9. Micro E coli

  Micro E coli JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kinachosumbua mkuu hapa kwetu ni doctors to patient ratio na ndicho kilicho mchelewesha mama yako kutibiwa wagonjwa ni wengi kuliko watoa huduma.
   
 10. b

  big niga Member

  #10
  Jun 29, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ...they are more than cockroach my friend
   
 11. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Utaokoa vipi maisha wakati hakuna vifa vya matibabu kama vile sindano za kuwekea dripu, vacuum pump za kuwatolea vichanga maji machafu wanayomeza wakati wa kujifungua, hamna dawa n.k ilihali fedha zote zinzpelkwa Usiwisi
   
 12. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Sasa kwa matatizo ya mama yako unamlalamikia nani, mathalni katika bajeti hii inayojadiliwa bungeni Wizara ya Afya imeomba Bilioni 198 kwa ajili ya kununulia dawa na vifaa vya matibabu na imetengewa Bilioni 78 tu. Hapo makosa ya madakatari yako wapi? Hata wao ni binadamu wameshasema wamechoka kuona watanzania wenzao walipoteza maisha kwa kukosukana vifaa vya matibabu na dawa vya gharama nafuu. Mara nyini hufikia hatua madakatari kutoa fedha zao mfukoni ili kununua baadhi ya vifaa vya kuokao maisha.
   
 13. T

  Twigwe Member

  #13
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani hili jambo liko mahakamani msiongele!!!, ugonjwa nao utaahirishwa na spika usije kwa vile jambo liko mahakamani, with no end, tumekwisha
   
 14. T

  Talklicious Member

  #14
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uwiano wa mkoa wa Rukwa wa daktari na wagonjwa na 1:132000 kwa mwezi, kwahiyo kusave doctor mmoja itawaokoa wagonjwa 100000 na ushee hasa sehemu nyingi. Dar tu ni 1:64000.
   
 15. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  nimeipenda hii
   
 16. w

  wakuziba Senior Member

  #16
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  madaktari wenye visasa, uanaharakati, hasira na uadui...... hawawezi kutufikisha mbali! EWE MUNGU tusaidie kuwabadilisha viumbe wako. mnategemea nini hivi vyama vya wanaharakati kwa mfano LHRC cha mama bisimba, vinapokua msitari wa mbele kuunga mkono wa madaktari ili watanzania wafe!?

  legal and human rights centre (LHRC) kuna neno human right hapa. haki kuu ya mwanadamu ni KUISHI. anaejiita mtetezi wa haki za binadamu kisha akawa anapuuzia haki ya msingi ya KUISHI kwa kuhamasisha madaktari wagome, inaonesha jamii yetu imepotoka.  pana jambo hapa. mgomo huu una siri nzito sn! MADAKTARI WOTE MUNGU AWALAANI!!!!!!!!!!!!!!!!! AMEEN
   
 17. P

  Pulpitis Senior Member

  #17
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuziba ulaaniwe wewe mnafiq unayechukulia mambo kijuu juu bila kutafuta ufumbuzi wa muda mrefu, Na kunyoishea vidole wenzio na kushindwa kujitambua.
   
 18. N

  Nambombe Senior Member

  #18
  Jun 29, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo wewe hautaki kuelewa,na sisi madaktari mungu hata tulaani,mpaka kieleweke na lolote na liwe
   
 19. G

  Gilly Member

  #19
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mkuu, heshima yako. Madaktari wanailalamikia Serikali kwamba vifaa kama anavyofungia Dr Ulimboka havitoshi ukilinganisha na idadi ya wagonjwa wanaohudumiwa na vingine kukosekana kabisa. Sasa vile anavyotumia Dr Ulimboka vimetoka wapi? Si ndiyo swali lako? Vimetokana na mgomo ambao umewakimbiza wagonjwa wengi kutoka Muhimbili na vitanda viko wazi. Kama Dr Ulimboka angepata mkasa huu kabla ya mgomo angelazwa chini kukwepa kuambiwa ma-Dr wanajipendelea. Na hii ndiyo ma-Dr hawataki. Kwa nini wagonjwa wao walazwe chini na wakose dawa au kulazimishwa wakanunue kwenye ma"Duka la Dawa Muhimu" ili hali nchi yetu ni tajiri sana tu? Serikali wanajua kwamba kwenye hospitali zetu hakuna vitanda wala dawa wala miundombinu mizuri (k.v. Umeme wa uhakika) ndiyo maana wanakimbilia India. Nani anataka kufa kwa sababu tu kwamba pamoja na juhudi ya Dr kukufungia mashine ya kupulia na kumwacha nurse akuangalie, TANESCO wakakata umeme na mashine ikazima? Dr alitaka kukuokoa, TANESCO na ufisadi wao wakakumaliza?
   
 20. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #20
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,335
  Likes Received: 2,659
  Trophy Points: 280
  vilevile hakuna movie inayomuua "steringi", la sivyo movie itaishia hapo hapo...so the guy must survive at all costs
   
Loading...