kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,423
- 13,935
Mfumo wa udahili wa pamoja kwa njia ya mtandao ulitengenezwa kutokana na tafiti zilizofanyika kuhusu manufaa yake katika kuwapunguzia wanafunzi na wazazi gharama za kutafuta, kuomba, na kujiunga na vyuo hapa nchini. Kuutengeza mtandao huu ulitumia gharama kubwa hadi uweze kukamilika, kuutangaza na kuutumia. Kuutupa mfumo huu ghafla ni matumizi mabaya ya kodi.
Baada ya kuachana na mfumo huu hivi sana wanafunzi wameanza kuonja joto ya jiwe. Application form sasa ni sh. 50000. Ukitaka kuwa na uhakika wa kupata nafasi kwenye chuo kimoja huna budi ufanye applications kwenye vuo 3 au zaidi. Mwanafunzi lazima alipe hela hizo kwenye benki ambazo nyingine hazipo huko mikoani sembuse wilayani.
Inawezekana chanzo cha shida zote hizo kwa wanafunzi ni taasisi moja hodhi ya kidini.