Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi (BRT) jijini Dar es Salaam, hasa barabara ya Posta/Gerezani kwenda Kimara, uliwahi kuonekana kama suluhisho la uhakika kwa adha ya usafiri. Hata hivyo, hali halisi kwa sasa ni ya kusikitisha. Safari zimekuwa mateso, msongamano ni wa kutisha katika mabasi haya kiasi cha kuhatarisha afya na maisha, na uchache wa mabasi umekuwa chanzo cha maumivu kwa maelfu ya watumiaji kila siku.
Je, huu ni mradi unaoendeshwa kwa hasara? Kama ndivyo, kwa nini? Kwa idadi kubwa ya abiria, ni dhahiri kuwa wateja wapo wengiii mno. Lakini bado huduma ni duni. Uchache wa mabasi — chanzo kikuu cha matatizo — unasababishwa na nini hasa? Ni ukosefu wa bajeti, uzembe wa usimamizi, ama hujuma? Na kwa nini tatizo hili limeachwa liendelee kwa miaka mingi pasipo suluhisho la maana?
Watumiaji wanalia kila siku. Wanafunzi, wafanyakazi, wazazi — wanakumbana na usafiri wa mateso. Je, kilio chao hakisikiwi? Au ni dharau tu kutoka kwa mamlaka husika? Kama huduma ya umma imegeuka kuwa “extreme sport”, basi tunapaswa kujiuliza: nani anafaidika na mfumo huu ulioshindwa?
Mradi huu ulikuwa wa matumaini. Sasa ni alama ya uzembe.
Kwani wanaosimamia mradi huu hawajisikii vibaya kuona watu tena wanaolipa kodi kwa ajili ya miradi kama hii wakisafiri kama mifugo?
Uwajibikaji wa makusudi tena wa haraka sana unahitajika kunusuru hali hii .