Mateo Qaresi: CCM hakuna anayefaa kuwa rais

Mateo Qaresi: CCM hakuna anayefaa kuwa rais

Mateo ni mchuvu kama lilivyo gazeti lenyewe lilivyopoteza heshima kwa kusikiliza maoni ya mchovu amesahau aliyoyafanya alipokuwa mbeya
That maye be the effect of alchohol....the effect is tremendous when you haven't tested for years.
 
hana lolote alitoswa kwa ulevi alikuwa analewa mpaka alfajiri na bungeni ni mtu wa kulala mpaka linaahilishwa

Kwa hili yuko sasahi, kwani kwa waliotangaza nia so far hakuna mwenye vision mpya ya kuikwamua nchii hii. Sasa hivi wako bize kufunika kombe ili maha.ramia wa escrow wapone, kuna rais hapo?
 
Mateo ni mchuvu kama lilivyo gazeti lenyewe lilivyopoteza heshima kwa kusikiliza maoni ya mchovu amesahau aliyoyafanya alipokuwa mbeya

Kwa hiyo wewe unam judge mtu kwa anachokisema au muonekano wake? Ningekuelewa kama ungejikita kwenye alichoandika.Again gazeti ni barabara tu ya kufikisha ujumbe.
 
Alichosema ni sahihi kabisa ila akumbuke alipokuwa kiongozi wa umma kama alitekereza hayo ayasemayo. Nakumbuka akiwa RC wa mbeya aliwai tembelea kijijini kwetu sijui alikuwa amekunywa ama vipi mana alipiga usingizi toka mwazo mwa mkutano mpaka mwisho. Kali zaidi ni pale lisala iliposomwa akiwa bado amelala na baada ya mkutano hata hakuijibu isala wala nini na kuonoka.
 
Nini kilichomzuia kutimiza malengo yake kipindi akiwa madarakani? huyu Mwehu tu!

Unajua ndugu yangu siyo kila jambo ni la kudandia na kujibu jibu tu. Kuna mengine unatakiwa unayasoma kisha unayatafakali halafu kama kichwani uko timamu unayafanyia kazi.

Na huu kama ungekuwa mtihani basi ujue division 5 unastahili sababu umekosa kuyaelewa maudhui kamili ya habari na kisha wewe unaanza kumzungumzia mtu tabia zake zilizopita.

Ndiyo maana wamagharibi wanasema watu wenye akili ndogo huwa wanaongelea watu sababu uwezo wao wa kuchambua jambo ni mdogo sana.

Hivi hujui kuwa watu hubadilika tabia kadri muda unavyooenda na pia huchangiwa na mazingira yanayowazunguka.
 
huyu mbunge wa babati vijijini kaongea point ila enzi zake alikuwa hakai bungeni,kuna wakati aliitwa kwenye mkutano wa kijiji akaulizwa sasa huu ni mwaka wa saba kwenye uongozi wako,hutembelei tena jimbo,hujaleta umeme unawaza nini?
akawaambia kama hamkujenga nyumba za maana niwafungie umeme kwenye masikio?watu kimya
 
Pinga maneno yake usimpinge yeye, ndivyo watu wenye akili na hoja wanavyofanya.

Mateo ni mchuvu kama lilivyo gazeti lenyewe lilivyopoteza heshima kwa kusikiliza maoni ya mchovu amesahau aliyoyafanya alipokuwa mbeya
 
Labda ndiyo maana amesisitiza sana umuhimu wa kiongozi kuwa mkweli. Alikuwa mkweli kuwa hakukuwa na nyumba bora.

Pinga maneno yake usimpinge yeye, ndivyo watu wenye akili na hoja wanavyofanya.
 
Nani kakudanganya kuwa mwaka huu kuna mazao mengi kuliko mwaka wowote tangu uhuru? Utakuwa unaota wewe. Angalia takwimu za exports za kahawa, pamba, korosho, chai, pareto, tumbaku, halafu linganisha na export za sasa; halafu husisha na population ya siku za nyuma na ya leo.

Huyu nae ajichukulie pensheni yake atulizane huko.

Ingekuwa wakulima hawajaliwi wangelima kuliko mwaka wowote ule tokea tupate uhuru?
 
Nani kakudanganya kuwa mwaka huu kuna mazao mengi kuliko mwaka wowote tangu uhuru? Utakuwa unaota wewe. Angalia takwimu za exports za kahawa, pamba, korosho, chai, pareto, tumbaku, halafu linganisha na export za sasa; halafu husisha na population ya siku za nyuma na ya leo.

Wacha porojo, labda hiyo ni kabla ya mwaka 1967, baada ya '67 tulitoka kutoka wasafirishaji wa kwanza mazao Afrika mpaka kuwa omba omba wa kwanza wa chakula Afrika. Cheza na Nyerere wewe?
 
mgombea.jpg


Waziri wa zamani katika Serikali ya Awamu ya Pili na ya Tatu, Mateo Qaresi.PICHA|MAKTABA

Na Joseph Lyimo, Mwananchi
Posted Jumapili,Novemba23 2014 saa 10:38 AM

Kwa ufupi

Kauli hiyo ya Qaresi imekuja wakati makada mbalimbali wa CCM wameshatangaza nia, wengine wakitajwa kutaka kuwania nafasi hiyo ya juu zaidi katika uongozi nchini.

Babati. Waziri wa zamani katika Serikali ya Awamu ya Pili na ya Tatu, Mateo Qaresi amesema kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa sasa hakina mgombea mwenye sifa ya kuwa rais wa awamu ya tano wa Tanzania.


Qaresi ameyasema hayo hivi karibuni mjini Babati katika mahojiano maalumu na gazeti hili, ambapo alidai kwamba CCM kwa sasa imepoteza sifa zote za kutawala kwa sababu hakina tena misingi ya kuwatetea wafanyakazi na wakulima bali sasa ni chama cha matajiri.


Mwanasiasa huyo ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa Babati kwa tiketi ya CCM, alisema kuwa chama hicho hakiwezi kutoa rais bora anayeweza kuwavusha Watanzania walipo sasa na kuwapeleka mahali pazuri zaidi kwa sababu ina viongozi wasiojiamini, hawawezi kutoa uamuzi mgumu katika kuendesha nchi.


“Mpaka sasa kwa watu wanaotajwa tajwa kuwa watawania urais kwa CCM, mimi naona hakuna mwenye sifa kwa sababu CCM haiwezi kumpitisha kiongozi mzuri na mwadilifu kwa kuwa watu wanatumia fedha na huwezi kupata kiongozi mzuri kwa kutumia fedha,” alisema Qaresi na kuongeza:


“Kuna ambaye ameshatangaza kwamba mwakani atagombea urais na ameshatenga fedha za kufanyia kampeni kwani ameanzisha kampuni yake na hana tatizo, fedha anazo za kutosha. Maana yake nini? Kwamba ana uwezo wa kuwahonga watu, sasa mtu wa namna hiyo anafaa kuwa rais?”


Kauli hiyo ya Qaresi imekuja wakati makada mbalimbali wa CCM wameshatangaza nia, wengine wakitajwa kutaka kuwania nafasi hiyo ya juu zaidi katika uongozi nchini.


Baadhi ya waliotangaza nia ni January Makamba ambaye ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mbunge wa Nzega, Dk Hamisi Kigwangallah.



Pia, wanaotajwa yumo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, Stephen Wasira ambaye ni Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Dk Asha Rose Migiro, Waziri wa Sheria na Katiba na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.

Hata hivyo, Qaresi alisema kazi ya urais ni ngumu na siyo ya mchezo kama wanavyodhani baadhi ya watu ndio maana utaona kuwa mtu hajamaliza hata miaka mitano katika ubunge, anatangaza nia ya kutaka kugombea urais.


“Miaka mitano hajaimaliza anataka kugombea urais, wakati hana historia kubwa ya uongozi. Wengine wanajulikana kuwa wana kashfa nyingi, lakini bado wanataka nafasi hiyo,” alisema.


Alisema kwamba nchi ikipata rais legelege, haitachukua muda mrefu itachafuka, kwani ataendeleza mambo ya kilegelege yanayoendelea na kuacha watu wenye fursa waifisidi nchi hii kwa kuwa hakuna mtu anayewachukulia hatua.


“Hivi sasa tangu juu mpaka chini, hakuna kinachoendelea. Watendaji wengi wamekata tamaa, uwajibikaji umekuwa duni, kwani watu wanakwenda tu kazini, ili mradi wanapokea mshahara. Tukimpata rais legelege, hatuna miaka miwili nchi itachafuka,” alisema Qaresi na kuongeza:



Qares: CCM hakuna anayefaa kuwa rais - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
Huyu mzee kaongea kweli kabisa. Watumishi wengi na watendaji wakuu wamekata tamaa. Hasa baada ya hili sakata la iptl. Yaani wanafanya kaZi katika mazingira magumu hata stahili zao tu halipwi, maisha yao na familia ni magumu. Huku kuna watu wanazawadiana fedha za serikali.

Kama hali hii itaendelea I'm telling you watu watafanya kitu mbaya.
 
Siasa za Tanzania ni za visasi, huyu jamaa alikuwa na bifu kubwa sana na mwenzake... mpaka leo.
 
CCM na miccm sio imepoteza sifa ya kutoa mgombea Uraisi bali imepoteza hata uwezo wa kutawala kwa haki na amani kwa maana hiyo imepoteza haki ya kuwa chama cha siasa na pia haki ya kuiongoza nchi hii imeshapoteza,imebakia ubabe tu. Ila kwa ukweli haswa CCM haina uhalali wa kuitawala na kuiongoza Tanzania.
 
namkubali sana qares, 4 sure ni jembe, alisha wahi kua mkuu we2 wa mkoa (mbeya), alkuwepo pia front line wakat wa G55
 
...lakini alichosema ni kweli, hakuna yeyote ndani ya chama chenu cha wahuni na mafisadi mwenye sifa ya kuwa Rais 2015.

Siasa za Tanzania ni za visasi, huyu jamaa alikuwa na bifu kubwa sana na mwenzake... mpaka leo.
 
Siasa za Tanzania ni za visasi, huyu jamaa alikuwa na bifu kubwa sana na mwenzake... mpaka leo.
Qaresi katema quinin -- bitter pill -- swallow it or stay with your cerebral malaria! Ni aibu hata kuvaa mavazi ya kijani!!
 
Ndio zao hawa pimbi Mkuu, wao wameshajimilikisha hati miliki ya kuamua nani ni Mtanzania na nani si Mtanzania kwa kauli nyepesi nyepesi tu bila ya kuwa na vithibitisho vyovyote.

Yeye siyo mtanzania?
Acheni ubaguzi
 
Back
Top Bottom