Mateka waachiliwa baada ya miezi 18 Niger

Mateka waachiliwa baada ya miezi 18 Niger

carbohydates

Senior Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
138
Reaction score
246
Wanawake wawili raia wa Austria na Uswisi waliokuwa wakishikiliwa mateka nchini Niger kwa zaidi ya miezi 18 wameachiliwa huru na kuwasili katika mji wa Benghazi mashariki mwa Libya, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Libya na maafisa waliozungumza kwa sharti la kutotajwa majina.

Raia wa Austria, Claudia Abbt, mwenye umri wa miaka 69, na raia wa Uswisi, Eva Gretzmacher, mwenye umri wa miaka 76, walitekwa mwaka 2025 katika matukio tofauti nchini Niger.

Katika video iliyochapishwa na kituo cha televisheni cha Al-Masar, wanawake hao walionekana wakitoa shukrani kwa kiongozi wa kijeshi wa mashariki mwa Libya, Khalifa Haftar, na mwanawe Saddam Haftar kwa mchango wao katika kuachiliwa kwao.

Hadi sasa, haijafahamika wazi ni kundi gani lililokuwa linawashikilia wala masharti yaliyowezesha kuachiwa kwao. Niger imekuwa ikikabiliwa na changamoto za kiusalama zinazohusishwa na makundi yenye misimamo mikali katika ukanda wa Sahel.

Chanzo : Reuters , Dw swahili

WOMEN.jpg
 
Lkn swali kwanini Wazungu wanapenda kwenda nchi za Kislam
Uko kwao kwao wanakosa nini kiasi kuelekea kwa Wajuba wa Kislam!!

Japo Waafrika tunajua ni njaa inawapeleka Ulaya

Lkn Wazungu wanatafuta nini¿¿¿¿¿¿
 
Back
Top Bottom