Mateka na watumwa kwenye ulimwengu wa roho

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
374,370
Reaction score
866,947
Habarini za muda huu... Hii ni mada yangu ya kwanza kabisa kwa mwaka huu wa 2019..... Ni siku ya kwanza ya mwaka huu mpya! Tarehe 1.1.2019... Jana usiku dakika chache kabla ya kuuaga mwaka 2018 niliandika mada kwa title ya Ahera madukani lakini sikufanikiwa kuipost... Naona inataka ipostiwe mwaka huu...

Ni siku ya kwanza ya mwaka kwa hesabu hizi za kizungu.. Kila mmoja wetu ana matarajio makubwa, mipango na hata mawazo ya kufanya kitu fulani kikubwa zaidi, kizuri zaidi na cha mafanikio zaidi... Ni hulka na matamanio ya kiasili ya mwanadamu yoyote.... Lakini bila kufahamu kuna watu ama roho somewhere hapo ahera madukani na kwingineko wanapanga kukukwamisha ama kuvuna jasho na kazi za mikono yako...

Mateka na mtumwa hawana tofauti kubwa.. Mateka huchukuliwa kwa nguvu lakini mtumwa anaweza hata kuuzwa ama kutolewa zawadi... Wote hawa mwisho wa siku ni kumfaidisha anayewamiliki.. Mateka atatakiwa kulipa kikomboleo ili aachiwe huru... Mtumwa atatumikishwa ili alete faida..!

Tupo wengi tulio matekani, tupo wengi tulio utumwani lakini hatujifahamu... Tunaona tu mambo hayaendi, hatufanikiwi kama wengine, hatupati ziada kama wengine.... Tunapata tu inayotosha kula na kukidhi mahitaji ya siku...

Ikipatikana ziada kutatokea dharura itatumika yote... Mwisho wa siku unabaki pale pale hupati hukosi...
Kama umemaliza mwaka 2018 salama lakini huna hakiba bank wala kwenye kibubu, basi tambua wewe ni mateka na mtumwa...
Umefanya kazi kwa bidii mwaka mzima, umejituma sana lakini kila ulichopata kikapata matumizi mengine ya dharura, sio ujenzi, sio uwekezaji sio jambo la faida... Umepata nyingi lakini huna kitu mfukoni....

Umetekwa kiroho rafiki, wewe ni mtumwa... Unatumikishwa... Unawatumikia wengine..... Ndio maana hukukosa chakula wala mavazi nk... Lakini hukupata ziada.. Hukuugua, hukupata shida kubwa lakini huna kitu.... Wewe ni mateka....
Mtumwa ili azalishe sana inabidi awe na siha njema, ale ashibe... Hukuwahi kulala njaa na kila ilipotokea changamoto uliipatia fedha ya kutatua...

Wewe ni mtumikishwajj hivyo unasaidiwa changamoto zako bila kufahamu ili ukazalishe mali
Jiangalie upya maisha yako na ulikopitia... Umepata ngapi na umezifanyia nini na umebakisha ngapi.... Kama huna salio tafakari mada hii.... Nitarejea......!!!!!

Jr[emoji769]
 
Ilitakiwa Mshana Jr afupishe habari yake kwa maneno hayo tu.

By the way nimefurahi sana kuanza mwaka na bandiko hili, linatafakarisha, linafanya mtu ujichunguze na uone wapi pakurekebisha kabla mwaka haujachanganya.

Hata hivyo tunatarajia utatuwekea uzi unaoelezea jinsi gani sasa mtumwa/mateka anaweza kujikwamua kutoka kwenye huo mkwamo madhubuti.
 
Mshana unayajua haya?! Ni muhimu sana watu wakajua siri hii na nini cha kufanya.
 
Naonaga Mshana Jr ni mtu wa ulimwengu mwengine kabisa ,,

Nilkuwa nadhanigi wewe utakuwa mganga wa kienyeji au unauza uza dawa za upareni kariakoo maana waganga wengi wanasura kama ya kwako tu (Avatar yako ni picha yako halisi ulisemaga) , ,Kumbe hapana
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji120]

Jr[emoji769]
 
Habarini za muda huu... Hii ni mada yangu ya kwanza kabisa kwa mwaka huu wa 2019..... Ni siku ya kwanza ya mwaka huu mpya! Tarehe 1.1.2019... Jana usiku dakika chache kabla ya kuuaga mwaka 2018 niliandika mada kwa title ya Ahera madukani lakini sikufanikiwa kuipost... Naona inataka ipostiwe mwaka huu...
Ni siku ya kwanza ya mwaka kwa hesabu hizi za kizungu.. Kila mmoja wetu ana matarajio makubwa, mipango na hata mawazo ya kufanya kitu fulani kikubwa zaidi, kizuri zaidi na cha mafanikio zaidi... Ni hulka na matamanio ya kiasili ya mwanadamu yoyote.... Lakini bila kufahamu kuna watu ama roho somewhere hapo ahera madukani na kwingineko wanapanga kukukwamisha ama kuvuna jasho na kazi za mikono yako...
Mateka na mtumwa hawana tofauti kubwa.. Mateka huchukuliwa kwa nguvu lakini mtumwa anaweza hata kuuzwa ama kutolewa zawadi... Wote hawa mwisho wa siku ni kumfaidisha anayewamiliki.. Mateka atatakiwa kulipa kikomboleo ili aachiwe huru... Mtumwa atatumikishwa ili alete faida..!

Tupo wengi tulio matekani, tupo wengi tulio utumwani lakini hatujifahamu... Tunaona tu mambo hayaendi, hatufanikiwi kama wengine, hatupati ziada kama wengine.... Tunapata tu inayotosha kula na kukidhi mahitaji ya siku... Ikipatikana ziada kutatokea dharura itatumika yote... Mwisho wa siku unabaki pale pale hupati hukosi...
Kama umemaliza mwaka 2018 salama lakini huna hakiba bank wala kwenye kibubu, basi tambua wewe ni mateka na mtumwa... Umefanya kazi kwa bidii mwaka mzima, umejituma sana lakini kila ulichopata kikapata matumizi mengine ya dharura, sio ujenzi, sio uwekezaji sio jambo la faida... Umepata nyingi lakini huna kitu mfukoni....
Umetekwa kiroho rafiki, wewe ni mtumwa... Unatumikishwa... Unawatumikia wengine..... Ndio maana hukukosa chakula wala mavazi nk... Lakini hukupata ziada.. Hukuugua, hukupata shida kubwa lakini huna kitu.... Wewe ni mateka....
Mtumwa ili azalishe sana inabidi awe na siha njema, ale ashibe... Hukuwahi kulala njaa na kila ilipotokea changamoto uliipatia fedha ya kutatua... Wewe ni mtumikishwajj hivyo unasaidiwa changamoto zako bila kufahamu ili ukazalishe mali
Jiangalie upya maisha yako na ulikopitia... Umepata ngapi na umezifanyia nini na umebakisha ngapi.... Kama huna salio tafakari mada hii.... Nitarejea......!!!!!

Jr[emoji769]
Namshukuru Mungu muweza wa yote kwani sipo kwenye makundi yote uliyoyataja.

Ila umenifundisha jambo kubwa kwa mara ya kwanza ndani ya 2019.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.......ajabu yetu binadam tunashughulika sana na mambo ya mwilini na kusahau kuwa hata matokeo mengine tuyaonayo dhahiri ni mambo yaliyokwisha fanyika katika ulimwengu wa roho,.matokeo mengi ya mwilini ni mambo ambayo yalishatendeka rohoni...

"Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama;bali ni juu ya falme na mamlaka,juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho" Waefeso 6:12
 
Habarini za muda huu... Hii ni mada yangu ya kwanza kabisa kwa mwaka huu wa 2019..... Ni siku ya kwanza ya mwaka huu mpya! Tarehe 1.1.2019... Jana usiku dakika chache kabla ya kuuaga mwaka 2018 niliandika mada kwa title ya Ahera madukani lakini sikufanikiwa kuipost... Naona inataka ipostiwe mwaka huu...
Ni siku ya kwanza ya mwaka kwa hesabu hizi za kizungu.. Kila mmoja wetu ana matarajio makubwa, mipango na hata mawazo ya kufanya kitu fulani kikubwa zaidi, kizuri zaidi na cha mafanikio zaidi... Ni hulka na matamanio ya kiasili ya mwanadamu yoyote.... Lakini bila kufahamu kuna watu ama roho somewhere hapo ahera madukani na kwingineko wanapanga kukukwamisha ama kuvuna jasho na kazi za mikono yako...
Mateka na mtumwa hawana tofauti kubwa.. Mateka huchukuliwa kwa nguvu lakini mtumwa anaweza hata kuuzwa ama kutolewa zawadi... Wote hawa mwisho wa siku ni kumfaidisha anayewamiliki.. Mateka atatakiwa kulipa kikomboleo ili aachiwe huru... Mtumwa atatumikishwa ili alete faida..!

Tupo wengi tulio matekani, tupo wengi tulio utumwani lakini hatujifahamu... Tunaona tu mambo hayaendi, hatufanikiwi kama wengine, hatupati ziada kama wengine.... Tunapata tu inayotosha kula na kukidhi mahitaji ya siku... Ikipatikana ziada kutatokea dharura itatumika yote... Mwisho wa siku unabaki pale pale hupati hukosi...
Kama umemaliza mwaka 2018 salama lakini huna hakiba bank wala kwenye kibubu, basi tambua wewe ni mateka na mtumwa... Umefanya kazi kwa bidii mwaka mzima, umejituma sana lakini kila ulichopata kikapata matumizi mengine ya dharura, sio ujenzi, sio uwekezaji sio jambo la faida... Umepata nyingi lakini huna kitu mfukoni....
Umetekwa kiroho rafiki, wewe ni mtumwa... Unatumikishwa... Unawatumikia wengine..... Ndio maana hukukosa chakula wala mavazi nk... Lakini hukupata ziada.. Hukuugua, hukupata shida kubwa lakini huna kitu.... Wewe ni mateka....
Mtumwa ili azalishe sana inabidi awe na siha njema, ale ashibe... Hukuwahi kulala njaa na kila ilipotokea changamoto uliipatia fedha ya kutatua... Wewe ni mtumikishwajj hivyo unasaidiwa changamoto zako bila kufahamu ili ukazalishe mali
Jiangalie upya maisha yako na ulikopitia... Umepata ngapi na umezifanyia nini na umebakisha ngapi.... Kama huna salio tafakari mada hii.... Nitarejea......!!!!!

Jr[emoji769]
Kuwa mateka ama mtumwa ni jambo moja ila kupata ukomboz ni jambo jingine na ni zito na kubwa sana kwa sababu kumjua mkweli ambaye atakupatanisha na Muumba wako si jambo jepesi, matapeli wengi sana siku hizi + agents ambao watakufanya uzame kabisa.

By the way, kinga ni bora zaidi kuliko tiba, hivyo bora ujiimarishe mapema kiimani kuliko kuja kusaka tiba baadae.
 
Back
Top Bottom