Mateja ni Noma..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mateja ni Noma.....

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Bushbaby, Jun 9, 2011.

 1. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Ni jana majira ya jioni nikikatiza mitaa ya Msasani, nikakutana na mateja wako wachafu wamekaa kijiweni wakipiga soga. Mara akaijitokeza teja mmoja na kuanza kuniita kwa sauti ya mlegezo sauti ya mlegezo..., “Oyaa sister eee..hebu nisubiri basi nikuulize” mie sikumjibu wala kugeuka, niliendelea kuchapa mwendo.  Oyaa sister unajifanya uso wa mbuzi sio, niliendelea kuchapa mwendo bila kugeuka......


  Baada ya kuona simjibu wala kugeuka, akaanza kumwaga maneno ya kifedhuli…….

  Unajifanya mzuuuri kumbe huna lolote, uzuri wenyewe uko wapi? Sana sana unatumia mgorogo tu, we nini bwana ….. unadhani tuna shobokea mademu sisi,…… shika time yako, huna lolote mshamba tu wewe……

  Tena sikiliza…. Ukizeeka na kuwa bibi kizee usije ukaniomba ugoro, maana hamkawii nyie, ukizeeka na kimkongojo chako……(akainama kuonesha mfano wa bibi kizee na mkongojo) lazima utakuja tu …. Kisha akaanza kuigiza sauti ya bibi kizee na kusema, “Mzee naomba kaugoro hapo nitulize kiu yangu”

  Sitakupa ng’oooo…….. Ishia huko………

  Kwa hisani ya Dada Koero Mkundi...Vukani Blog
   
 2. Omukuru

  Omukuru JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Unamtumia teja kama kipazasauti kufikisha ujumbe kwa dada fulani, sio!
   
Loading...