Matatizo ya Mirathi Tanzania Chanzo Chake Nini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matatizo ya Mirathi Tanzania Chanzo Chake Nini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by August, Jul 12, 2009.

 1. A

  August JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  Tukiwa bado na muwasho washo wa Kadhi Court, naomba ndugu zangu tujadilini chanzo cha matatizo ambayo Kadhi Court inataka kulipunguza kama sio kuliondoa kabisa.
  Mimi kwanza nijua avyo kuna Sheria kama tatu zinazo tawala mambo ya Mirathi
  1 Taratibu za asili za makabila yetu, ambapo huko nyuma mrithi anakuwa Kaka wa Marehemu au Mtoto Mkubwa wa Marehemu na kuna wengine Mtoto wa Mwisho wa Kiume, na zaidi ya hapo sheria hizi za kijadi zilikuwa rahisi kuzitekeleza kutokana na watu hao kuishi sehemu moja, huko kijijini.
  Lakini siku hizi au hata hizo zilileteleza mifarakano mingi katika jamii nyingi ikiwa msimamizi huyo ni mlevi au ana matatizo mengine.

  2. sheria hizi za Mkoloni , au zinazotungwa na Serikali kupitia Bunge
  3 Sheria au taratibu za Dini zetu iwe Ya Kikristo au ya Kiislamu, ya kipagani itakuwa kwenye taratibu zetu za asili.

  Sasa ukiachilia mbali mifumo hiyo tuio nayo kuna kitu kinacho itwa Wosia, ambacho kinasaidia saana katika kupunguza misuguano ya mirathi. lakini bado ipo kutokana na watu wengine kutoandika wosia au wengine kufikiria kwamba wosia lazima utamwachia kitu? hususana watoto wa kiume ambao mwenendo wao wa maisha haukumfrahisha marehemu.

  Sasa ili kutatua au kupunguza matatizo kama hayo ningependekeza serikali kuweka katika somo la uraia skipengele hicho cha wosia na taratibu mbali mbali za kuacha mirathi ili kila mtu ajue njia ipi inamfaa kama ni ya kijadi , taratibu za kidini au sheria za kiserikali wajibu wake wa kuacha wosia na kwa wale wanaoachiwa nao waelewe haki zao na wajibu wao.
   
 2. P

  Paullih Member

  #2
  Jul 12, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 85
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Napenda kuungana na August juu ya umuhimu wa somo la Uraia hususan kipengele cha Mirathi na haswa jinsi ya kuandika wosia na umuhimu wake kwa jamii.

  Matatizo mengi yahusuyo mirathi ambayo jamii nyingi hukumbana nazo yangeweza kupungua au kuisha kabisa kama kizazi kinachobaki baada ya mpendwa wao kuondoka, kingekuwa na mwongozo ambao huitwa wosia.

  Mifarakano, tamaa na machungu hutokea tu pale ambapo kuna ubinafsi na tashwishi ya watu kupenda kuvuna wasichopanda.
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Jul 12, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hapa naona unataka kutuingiza town, Mahakama za Kadhi, miundo yake na kazi zake yanafaa kujadiliwa na waislamu wenyewe, huko misikitini. Unavyolileta ni kama vile kila mtu suala la waislamu na mambo yao linamhusu. Ndio maana watu wasio waislamu wanataka mambo ya kadhi na uislamu wajadiliwe na kuendeshwa na wenyewe kwa faida yao wenyewe, kwa kuwa ni ibada yao! Kama unaona ni lazima yajadiliwe na kila mtu basi mimi naona hizo mahakama za kadhi zitaleta matatizo ya watu kupigwa mawe, kuchapwa viboko na serikali kuingilia mambo ya dini ambapo mwisho wake ni vurugu kwa kuwa dini moja itajiona kama imekandamizwa na dini nyingine, ie bunge litunge sheria inayohusu dini moja likiacha dini nyingine, it doesnt make sense at all!
   
  Last edited: Jul 12, 2009
 4. A

  August JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  Muzee mimi nimeongelea mpaka mirathi zetu za asili nimeongelea hizi sheria zetu sijui za kithungu etc mpaka dhana ya mtoto wa kwanza au wa kiume kufikiria yeye ndio msimamizi wa mirathi, ni nao ndugu wengi tu ambao walibweteka wakisubiri mzee afe nao wawe warithi na hata kuna wadogo ambao wanabwia unga wakijua nyumba ya mzee ipo. Nafikiri tukiongelea kwa mlango huo tutaona tatizo letu ni elimu ya hayo mambo, mtu kuandika wosia anaona kama anajichuria, na hao warithi nao hawajui majukumu yao au njia zilizo muuafaka kupunguza matatizo yao. na haya mambo yapo pande zote iwe muuislam, mkristo mpagani etc etc. Ukienda Magomeni au mwananyamala hata kariakoo, unaweza kukuta familia nyingi tu za kiislamu, na sheria hizo hizo za kiislamu lakini migogoro ya mirathi ipo.
  na hata hizi mirathi zikaumuliwa kwa misingi au zilizo amuliwa kwa misingi ya kiislamu, bado migigoro ipo. Sasa unatakiwa uchimbe zaidi ili uelewe tatizo ni nini na jinsi ya kutatua. hasa kwenye hii Dunia yetu ya Sasa Muhaya kamuoa Muzaramo, Mzaramo kamuo Msukuma, Muislamu kao Mkristo nk nk .
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Jul 12, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  August,
  Mkuu swali zuri sana na hakika hili ndilo sababu kubwa ya matatiuzo tulokuwa nayo sasa hivi kuhusiana na hiyo Mahakama ya kadhi..

  Binafsi, kulingana na mawazo yangu, kosa kubwa la sheria zinazohusiana na Personal matters ni pale tunapoziweka kuwa ktk mtililiko wa nchi za Magharibi ambazo zinafungamana na imani ya dini fulani MOJA. Elimu yote ya sheria tunayoipata chuo kikuu au nje inatokana na mtungo wa mila na desturi za watawala wetu hivyo toka mwanzo sheria zetu hazikuzingatia mila na destuiri za Kiafrika au kwingineko..Hakuna elimu ya sheria iloschukua mila na desturi zetu na kuipa vifungu vya sheria ikatumika kuwaelimisha wasomi. Kwa sababu elimu ya asili yetu sii elimu ila ni ktk wigo kubwa la Uncivilization.

  Hivyo ukisikia msomi wa sheria ni yule aliyesomea elimu ya sheria kufuatia mila na desturi za wazungu..ambao pia walichukua mengi toka ktk dini na mila za waliowatangulia kuitwa civilized society, kiasi kwamba swala la mirathi pia limelenga kuamini zaidi mfumo, taratibu na sheria za mila, dini na kadhalika toka nchi hizo za nje..
  Na kama sisi ni nchi ilokuwa huru yenye mfumo wa secular hatuwezi kuwa na sheria tofauti kwa kila kundi au raia wetu, but at the same time ni makosa pia kuwapa uhuru waumini wa mila na dini hizi kufuata ibada za mila na mafundisho yao ambazo settlements zake ni kinyume cha imani zao. Vitu hivi viwili haviwezi kwenda pamoja yaani katiba inayowapa watu Uhuru kuabudu kisha kuna vipengele vya sheria vinavyopinga matumizi ya ibada hizo kisheria.

  Ndio maana kila siku mimi hupinga elimu yoyote ile isiyozingatia WATU na MAZINGIRA yao..hivyo matatizo ya Mirathi nchi chanzo chake ni Kuiga mila na desturi za wageni (Sheria) wakati tunawapa uhuru wananchi kuabudu dini zao kikatiba..

  Ni kutokana na elimu hii ya kununua ndio unaona watu wakifuga ng'ombe wa kizungu ktk mabanda wakiwakatia majani utafikiri sisi pia tuna season ya winter. Tunashindwa kujiendeleza na ng'ombe wetu wa Zebu na Ankole ambao wapo kwa mamillioni lakini kuna njaa kali nchini acha mbali kusafirisha nyama hiyo nje...Ni sawa na kumuuzia msukuma chapati au kujaribu kumhubiri Mzaramo kuhusu Ugali wa sembe na Parachichi..Mzungu hasomi elimu ya wala Historia ya Mkwawa kwa sababu hamhusu wala haimuwezi kitu chochote ktk maendeleo yake hivyoi hata huwezi kumuuzia elimu yetu iso fit ktk mazingira yake yake - Haihitaji.. Ila chochote kile kinachoweza kuwasaidia (WATU ktk Mazigira yao ndicho wataendelea kukusanya toka kwetu..

  Kwa hiyo, binafsi nafikiri ni jambo la busara sana ktk maswala ya ndoa, mirathi, custody na mengineyo mengi tu yasiwe ktk sheria ya Taifa.. vyombo vya dini na makabila vipewe nguvu na uwezo wa kutoa suluhu ktk maswala haya kulingana na imani ya wahusika..Ila cha msingi zaidi ni lazima Magistarte Court Act itambue sheria hizi kwani ndizo sheria za mwafrika, Mtazania tofauti na sheria ambazo zinatumika au zingetumika Uingereza kwa Muingereza ambao wote wamejenga mila na desturi zaotoka kabila moja au dini moja.
  Kutambulika kwa sheria hizi ndogo za madai kutasaidia tu kuhalalisha maamuzi ya vyombo vinavyosimamia madai haya..Au jingine ni kwamba itungwe sheria ambayo itakubalika sehemu zote... jambo ambalo pia lina utata kwani tofauti za mila na desturi ktk dini na madhehebu yake ndizo zilizofanya sisi wote kuto amini mfumo mmoja. sasa tutaanzia wapi hilo ndio swali gumu na zito sana.

  Mwisho, nitachukua mfano wa Mzee Mwanakijiji kuhusiana na kanisa katoliki ambalo linakataza divorce by any means hadi kifo kiwatenganishe.. Sasa kuna madhehebu mengine hayakubaliani na agizo hilo lakini pia kama mahakama yetu itachukua uamuzi wa kutoa divorce kwa Wakatoliki wawili, bila shaka mahakama hiyo itakuwa imekiuka ibada kuhbwa ya Wakatoliki. Na ikiwa Wakatoliki wakisimama na kuomba sheria inayokataza kuvunjwa kwa ndoa zao, binafsi sioni kosa maadam wao wameridhia na wanataka kusimamisha ibada hiyo kwa waumini wake..

  Upande wa pili sintakubaliana na chombo au kundi la watu wanapotaka kuanzisha sheria hii au mahakama hii kuwahukumu wakristu (Wakatoliki) wasivunje ndoa zao wakati hawa watu sii wacha Mungu. hawafuati mafundisho ya Kikatoliki na ndoa zao zimefungwa kinyume cha misingi ya Kilkatoliki..Lakini pamoja na kutokubali kwangu bado naona uzito wa hoja ya Wakatoliki kutovunja ndoa zao kulingana na imani yao hata kama mimi sikubaliani na mfumo wao. Je, tuwawezesha vipi wapate kufanya ibada hiyo ndilo swala tunalotakiwa sisi kujadili lakini sii kukana haki hiyo kwa Wakatoliki kuitumia na ikakubalika kisheria.

  Na ndio maana nikasema kutobaliana kwangu na mfumo huo ndio maana sikuwa Mkristu..Hivyo madai yao hayanihusu ila naweza kuzungumza kwa njia ya kusaidia kimawazo.. Sina haki ya kusema Wakatoliki hawatakiwi wala hawaruhusiwi kuvunja sheria ya nchi ambayo inatukuza divorce..Somewhere tunahitaji kuwapa ruksa hao wakatoliki wapate kufanya ibada hii laa sivyo hatukuwapoa uhuru kamili wa kuabudu. Now, How can it be executed, that's a million dollar question! lakini hatuwezi kunambia ni upuuzi madai yao wakati naamini kabisa Wakatoliki wana uhuru wa kufanya ibada yao kikatiba..somehow, sisi na sheria yetu inatakiwa ku respect maamuzi ya kanisa inapofikia swala la hii ibada yao.
   
  Last edited: Jul 12, 2009
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Tatizo kubwa nnaloona mimi ni watu kuzaana nje ya ndoa na watu kutokuwa na tabia ya kuwacha wasia za mirathi zilizo wazi tukiwa hai.
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Jul 12, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Dar Es Salaam,
  Mkuu wangu hata ikiwa kuzaana ndani ya ndoa.. Wanasayansi kitengo cha DNA wamesha sema -Kati ya watoto wanaozaliwa nchini 100, 60 sii wa baba wa ndoa hapo mkuu maamuzi ya mirathi yachukue mkondo gani?
   
 8. P

  Paullih Member

  #8
  Jul 12, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 85
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu hizo data ni za nchi gani?
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  KiIslam hatuna shida na hilo, wa nje ya ndoa, harithi. wa ndani ya ndoa anarithi. Na ikifikia mpaka wanandoa wanakwenda kupimana dna, hiyo ndoa haina amani.
   
 10. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu hizo data ni za Tanzania, nchi nyingine au dunia nzima in general? Tunaweza kupata source ya hizo data? Maana nilikuwa silijui hili na nipo very interested.
   
 11. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Hapo kweli mkuu. Baba au mama hawezi kudai DNA kama kuna kuna kuaminiana ndani ya ndoa. Ikifika hatua hiyo jua hao wanandoa basi hawa aminiani. Mtu hawezi kuomba DNA test out of no where.
   
 12. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  pamoja na hiyo statistics
  mrithi wako sio lazima awe mtoto wako wa kuzaa bali ni mtu yeyote yule ambaye uamua akurithi

  kuhusiana na watz kuiga sheria, kwa ujumla watz tumeiga vitu vingi mpaka dini ya ukristu na uislamu
  lazima uwelewe zamani watu wa eneo moja na kabila moja ndio walikuwa wanaoana lakini leo che nkampa anatoka kusini anaenda kuoa kaskazini nchi yetu bado ilikuwa haijajiandaa kwa hili (kwa hiyo hatuwezi kufata sheria za jadi wala dini inabidi tuwaangalie watu ambao wametutangulia kwenye maswala haya wanafanyaje) tumekubali kuiga elimu, technologia na hivyo maisha na kila kitu kinakuja na sheria zake....

  huu ugomvi hausabishi na watoto wa nje ya ndoa sana kama watu wengi mnavyodai, bali ndugu wa marehemu wanapokuwa na wao wanataka mkato
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Jul 12, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Semilong,
  Mkuu walioiga mila na Desturi za nje ni wewe na mimi, wapo wasiokubali kuiga na hawataki kuiga..Sote hatukuchagua kuiga sheria ila sheria imetulazimisha kuishi hivyo kinyume cha mazingira yetu..Tulichochagua ni elimu ambayo kweli ina sheria zake lakini kibaya ni kwamba tumechagua sheria moja.
  Hivi kweli wewe unaamini mimi naweza kumrithisha mtoto wa nje nikamwacha mwanangu wa damu simply because nimechagua kufanya hivyo?
  Matatizo ya mirathi nchini ni zaidi ya ndugu mkuu wangu, Ugonvi mkubwa ndugu huingilia kwa sababu kuna zaidi ya nyumba moja zinazotaka urithi mmoja na mgawanyo wake kisheria haujulikani kwa sababu bado tunatumia sana mila zetu ktk ndoa...
  Kisha swala la DNA ni utafiti ulofanywa, leo hamuoni tatizo lakini kesho mtakuja nambia..
   
 14. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Huu ni uonevu mkubwa, kwani wakati baba na mama mnaenjoy huyo mtoto mnaye mnyima haki hakuwepo, iweje nyie raha zenu zimuandame mtoto asiye na makosa?

  Kwa vile mli enjoy one day akatokea, ni halali apate haki kama watoto wengine!
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Jul 12, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Tatizo sii mtoto wala wazazi, Tatizo ni sheria ambazo hatuzifuatwi ila siku ya urithi..ndio maana wenzetu kutembea nje ya ndoa ni chaguo la mhusika huwezi kumshitaki na he/she is responsible kwa matokeo (outcome) ya maamuzi yake.
   
Loading...