Matatizo ya maji katika jamii kubwa na bajeti finyu iliyopitishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matatizo ya maji katika jamii kubwa na bajeti finyu iliyopitishwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kupelwa, Aug 25, 2012.

 1. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 866
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Katika taarifa ya habari ya leo ITV ni maeneo kadhaa nchini yameonyeshwa kuwa na adha kubwa ya upatikanaji wa maji safi na salama.

  Miji ambayo imeonyeshwa katika taarifa ya habari hiyo ni mkata, handeni na gairo. Ni ukweli usiopingika miji midogo na hasa vijijini kipindi hiki cha kiangazi wanapata adha kubwa kwa sababu upatikanaji wa maji huwa finyu.

  Ikumbukwe wakati wa kupitisha bajeti kuna wabunge kama mh kessi wa Nkansi alidiriki kushawishi wabunge wengi wasipitishe bajeti ya wizara ya maji, lakini bila kutegemea wabunge bila kujali wananchi wanavyopata adha walikubali kupitisha bajeti hiyo kwa mafungu ya ujumla bila mabadiliko.

  Je, kwa mstakabari huo, serikali ya CCM ipo kuwajali wananachi walio wengi hasa kwenye hii adha ya tatizo la maji?

  CHANZO: TAARIFA YA HABARI SAA MBILI USIKU ITV
   
Loading...