Matatizo Na Migogoro Ndani Ya Tfnc: Mheshimiwa Profesa Idrisa Mtulia

771004311

New Member
Sep 27, 2007
1
0
Kwa muda usiopungua miaka miwili Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) imekuwa moja kati ya Taasisi za Umma ambazo utendaji wake umekuwa ukilegalega na viogozi wake kuonyesha kila dalili ya kupoteza dira na mwelekeo katika utekelezaji wa majukumu yao. Matokeo ya hali hiyo yamepelekea TFNC ikijikuta inapoteza imani kwa wafadhili, ikishindwa kutumia fedha za Serikali zinazotolewa kupitia bajeti yake na kushindwa kuboresha maslahi ya wafanyakazi wake kiasi cha kukimbiwa na idadi kubwa ya wataalam ambao wamebobea katika masuala ya lishe. Aidha, ni katika kipindi hicho hicho na huenda ni kutokana na Taasisi kushindwa kutumia fedha za walipa kodi, Serikali iliamua kupunguza bajeti ya TFNC kutoka takriban shilingi bilioni 1.7 kwa mwaka hadi kufikia shilingi 375 milioni tu katika mwaka wa fedha 2007/2008.

Kumbukumbu nzuri za mafanikio katika Taasisi hii kongwe ilikuwa ni kisimamia na kuendesha miradi mbalimbali mikubwa ya kitaifa yenye malengo ya kupunguza tatiza la utapiamlo miongoni mwa Watanzania. Baadhi ya miradi hiyo ni kama ile ya Kupambana na tatizo la Upungufu wa Wekundu wa Damu (Anaemia), Mradi wa kupambana na tatizo la Upungufu wa Madani joto mwilini (IDD), Mradi wa Vitamin A na Mradi wa Lishe ya Watoto wachanga. Inasikitisha kwamba miradi hii sasa ama inasimamiwa na Taasisi nyingine au imekufa kabisa huku viwango vya utapiamlo vikiendelea kubaki juu sana.
Hivi karibuni matukio kadhaa yameendelea kutokea na kufanya hali hewa katika Taasisi ya Chakula na Lishe kuzidi kuchafuka. Hali hiyo ilisababisha Mwenyekiti wa Badi ya TFNC Mheshimiwa Profesa Mtulia Mbunge wa Rufiji kulazimika kukutana na wafanyakazi mara mbili katika kipindi cha mwezi mmoja tu. Katika ziara zake zote mbili shutuma kadhaa zilitolewa na wafanyakazi na hasa zikielekezwa moja kwa moja kwa uongozi wa Taasisi. Baadhi ya tuhuma hizo ni pamoja na ukabila, chuki, dharau na unyanyasaji wa wafanyakazi, dhuluma, kauli na tabia zilizo kinyume na maadili ya uongozi katika utumishi wa umma, ukiukwaji mkubwa wa taratibu za kisheria na hata ubadhirifu wa fedha za serikali. Aidha, kutokana na ubinafsi na maamuzi yasiyofaa ambayo yalifanywa na uongozi wa juu wa Taasisi, TFNC sasa imekumbwa na mgawanyiko mkubwa ambao umeathiri sana umoja na mshikamano miongoni mwa wafanyakazi katika ngazi zote.

Ukabila, chuki, dharau na unyanyasaji wa wafanyakazi, dhuluma na ukiukwaji wa maadili ya uongozi ni tuhuma nzito kwa kiongozi yeyote wa umma. Kwa upande mmoja inatia moyo kuona wafanyakazi wakibainisha udhaifu huu katika utendaji wa viongozi wao bila woga na kwa ushupavu na ujasiri mkubwa. Lakini kwa upande mwingine inasikitisha kwamba hata ilipobainika kuhusu kuwepo kwa ukosefu wa maadili kwa baadhi ya viongozi wa Taasisi hii Mwenyekiti huyi wa Bodi ya TFNC (Profesa Mtulia) hajawahi kutumia mamlaka yake kubainisha kukerwa kwake na jambo hili na hivyo kulikemea. Kwa bahati mbaya sana Mwenyekiti huyu amerudia tena na tena kuzihusisha shutuma hizi na tabia ya wivu, fitna na majungu kwa Kiongozi Mkuu wa Taasisi licha ya ukweli kwamba kiongozi huyo hawajawahi kuzikanusha waziwazi tuhuma dhidi yake au kukanusha kukithiri kwa matukio yenye harufu ya ukabila, chuki, dharau na unyanyasaji wa wafanyakazi, dhuluma au ukiukwaji wa maadili ya uongozi.
Mtaalamu mmoja wa menejimenti aliwahi kujisemea kuwa “Wajibu wa kwanza wa kiongozi ni kuwafafanulia anaowaongoza hali halisi.” Kwa mtazamo wangu Mheshmiwa Mtulia akiwa kama kiongozi amekosa ujasiri wa kuwaeleza ukweli viongozi wa TFNC wanaohusishwa na shutuma hizi kuhusu mapungufu yao na kukemea maovu yote ambayo yanaharibu taswira nzuri ya uadilifu katika utumishi wa umma. Hali hii ya Mwenyekiti wa Bodi kukosa ushupavu, ujasiri na kuwa mwoga kusimamia maadili inatosha kuthibitisha uwezo mdogo wa uongozi alionao na hivyo kutostahili kuendelea kubaki katika wadhifa wake katika Taasisi hii.

Kwa kiongozi hakuna fedheha kama ile ya mtu kujulikana kuwa “amewekwa mfukoni” maana jambo hilo ni sawa na utumwa. Katika hali hii mtu anafikia hatua ya kutetea hata ambacho hakiwezekani kutetea. Katika mazingira hayo hayo mtu mzima mwenye macho unakuwa haoni kwa kuhofu kumuudhi “mzee”. Wakati mwingine mtu wa namna hii pamoja na kuwa na masikio lakini hasikii la mtu kwa vile masikio yake yamezibwa na utamu wa maslahi anayopata kwa kutomkemea kiongozi mwenzake anayekiuka maadili. Sitaki kuamini kuwa Mheshimiwa Mbunge amewekwa “mfukoni” lakini kushindwa kwake kutimiza wajibu wake kama kiongozi kunatoa nafasi ya kuibuka kwa hisia kwamba ana maslahi fulani yanayomfanya ashindwe kukemea maovu. Aidha, hatua yake ya kuwafokea hata wale wanaobainisha maovu na mapungufu mengine katika Taasisi hii au kuziita shutuma dhidi ya viongozi wasio waadilifu kuwa ni wivu na majungu ni jambo la aibu kwa kiongozi anayepaswa kuilinda na kuitetea dhana halisi ya utawala bora. Kiongozi wa namna hii hatufai.

Kwa kutambua wadhifa alionao kwa mujibu wa Sheria iliyounda Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania na kwa kutambua imani aliyopewa na mtu aliyemteua katika wadhifa alionao ni wajibu wake yeye mwenyewe Mheshimiwa Mtulia kupima uzito wa mapungufu haya katika utendaji wake na kuchukua hatua zinazostahili.
 
Duh...hivi mkurugenzi wa TFNC ni nani siku hizi?

Hii taasisi mbona ilishadorora siku nyingi tu. Nakumbuka enzi hizo ilikuwa na wana sayansi waliobebea sana kwenye nutrition - Dr. Nduguru, Dr. Ny'ang'anyi, Dr. Mlingi, Dr. Kingamkono, Dr. Kavishe, Dr. Temalilwa, Dr..... Wengi wao walishaondoka baada ya kuona kuwa walikuwa wanazinguliwa mno.

Hii taasisi ilitumia hela nyingi sana miaka ya 80 - 90 kuwasomesha wafanyakazi wake wengi nje (Netherland na Sweden), lakini ikashindwa kuwapa job security na benefits za kuweza kuwashawishi wabaki kwenye taasisi. Matokeo yake, wengi walikimbia mara baada ya kupata phd zao.

Kama hii taasisi ingefanya kazi kisawasa, basi tatizo la utapiamlo Tanzania lingepungua sana. Lakini kwa sababu ya ubinafsi na kutoweka priorities straight, upendeleo na ufujaji wa fedha ulizorotesha sana hii taasisi. Yaani sasa hivi hii taasisi ni kama vile 'mfu anayetembea'
 
Anaitwa Dr Godwin Ndossi

Yeah.....I know this guy.

Ni jamaa mmoja smart sana, lakini majivuno meeengi! Nakumbuka kwenye mwanzoni mwa miaka ya 90, alipojiunga na TFNC alikuwa ametoka mtoni (sikumbuki nchi gani) baada ya kukaa huko muda mrefu. Basi TFNC alimpatia nyumba kule Mikocheni B (Lishe wana compound ya nyumba 5 kule), jamaa akakataa kisa eti aliona kuwa zile nyumba ni za hadhi ndogo, na kwamba yeye ni mtu special hawezi kukaa kwenye zile nyumba.
 
Back
Top Bottom